Mpango wa Minara ya UCSAF kunufaisha Watu Milioni 8.5, Wilaya ya Kibondo Wanufaika

Mpango wa Minara ya UCSAF kunufaisha Watu Milioni 8.5, Wilaya ya Kibondo Wanufaika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MPANGO WA MINARA UCSAF KUNUFAISHA WATU MILIONI 8.5, WILAYA YA KIBONDO WANUFAIKA

Waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye amesema kuwa wananchi milioni 8.5 watanufaika na kuunganishwa kwenye mawasiliano ya simu za mkononi na vifaa vingine vya mawasiliano kupitia mpango wa uwekwaji minara 758 sehemu zisizo na mvuto kibiashara kupitia Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF)

Nape alisema hayo akianza ziara ya mikoa mitano ya kuzindua minara ya mawasiliano ambapo alifanya kazi ya kuzindua minara miwili katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma ambapo alisema kuwa ujenzi wa minara ukaleta tija katika upatikanaji wa huduma na kuchochea maendeleo kwenye maeneo yao vijijini.

Hata hivyo Waziri huyo wa habari amewataka wazazi kuwaonya na kuwasimamia watoto wao ambao wamekuwa wakitumia vibaya uwekwaji wa minara hiyo ya mawasiliano kuzua taharuki, kuwatukana viongozi na kuharibu taswira ya nchi na viongozi.

Awali Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba alisema kuwa serikali imetenga fedha kwa ajili ya uwekaji wa minara 758 maeneo ya vijijini ambayo hayana mvuto wa kibiashara kwa makampuni na kufikia Juni mwaka huu tayari minara ya mawasiliano imewashwa na inafanya kazi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Meneja wa kanda ya Magharibi airtel, Isack Kijuu alisema kuwa uzinduzi wa mnara huo unaifanya taasisi hiyo kufikisha minara 86 ambayo imewashwa na airtel katika mpango huo chini ya UCSAF.
IMG-20240715-WA1271.jpg
WhatsApp Image 2024-07-15 at 20.56.04.jpeg
WhatsApp Image 2024-07-15 at 20.56.03.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-07-15 at 20.55.59.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-15 at 20.55.59.jpeg
    196.3 KB · Views: 3
  • IMG-20240715-WA1272.jpg
    IMG-20240715-WA1272.jpg
    51.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-07-15 at 20.55.53.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-15 at 20.55.53.jpeg
    143.4 KB · Views: 2
Back
Top Bottom