Mpango wa Mungu si mpango wa mwanadamu, yeye anapanga yake na sisi yetu

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
23,234
Reaction score
28,473
Ni vizuri tukakumbuka kwamba aliyeasisi unyama huu (udikteta uliopitiliza) wa kiwango cha akina Benito Mussolin, Joseph Stalin, Augusto Pinochet ni Magufuli akilindwa na Katiba ya 1977 iliyoandikwa na CCM chini ya maelekezo ya Nyerere.

Naonya: ikiwa hayatafanyika marekebisho ya dharura ya katiba ya 1977 kabla ya 2030, utawala huu unaandaa mazingira ya kumpata Adolph Hitler!

Turudi kwa Magufuli.

Magufuli alipoingia madarakani akasema yeye hajaribiwi!

Kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuvunja misingi yote ya kidemokrasia na haki.

Yote mema (ukiwemo mchakato wa kuandika Katiba mpya) yakafutwa, likabaki jina moja tu la MAGUFULI.

Magufuli alifanya machafu yote hayo huku umma ukimshangilia! Umma haukujua kwamba Magufuli alikuwa anawachimbia kaburi la halaiki ambalo leo limewazika watanganyika wote wakiwa hai!

Maana yake ni kwamba, ikitokea likamtokea mama kama lile lililomtokea Magufuli, kabwana mdogo kataukwaa urais wa Jamhuri kiulaniii mno! (hapo ni lazima katiba ibadilishwe)

Kwa wale tuliowahi kuiona hii muvi tunajua itakavyoisha.

Chadema walikimbia nchi,lakini baadae walikaribishwa kwa upendo mkubwa wenye utu,lakini haya yote wameyasahau.

Ad hoc!
 
Kabwana mdogo wamesema ni kapole, kanyenyekevu, hakapigishi watu shoti. Wamesema ni kazuri hakana makundi. Wakaache kaendelee mpaka kawe rais kapitishwe bila kupingwa chamani. Katiba isipobadilishwa na kenyewe katarithi mwendo huu huu kulinda regime yake. Wamekasifu ni kanyenyekevu, katiifu, basi watulie hivyohivya wakaache chenyewe tu ndio kachukue fomu ya kugombea urais awamu ijayo
 
Chadema walikimbia nchi,lakini baadae walikaribishwa kwa upendo mkubwa wenye utu,lakini haya yote wameyasahau.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kwa sasa kutokana na madaraka aliyonayo, na kwa kujipendekeza kwa watanzania, tarajia atasalimiwa shikamoo mpaka na watu waliomzidi mbali kiumri.

Hivyo alikuwa bwana mdogo zamani lakini sasa ni bwana mkubwa.
 
Sidhani kama mchakato ujao wa kumpata mgombea urais kama huyu dogo ataacha kuchukua fomu na kupitishwa agombee. Ishu ni katiba mpya isipokuja na kenyewe katageuka kakatili kubonda wanaompinga, kataendeleza na kurithi siasa za kibishi hakatataka mabadiliko
 
Hii nchi inaendeshwa by chance sio kwa mifumo, hii loop haitaisha hadi tukiweka katiba mpya mezani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…