- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Hivi kuna mpapai dume ambao watu wanasema ni ule ambao hauzai ila unatoa maua tu!?!
(b) Kufunga gunzi la mhindi lina maana gani kwa mmea kama mpapai usio zaa ili uzae??
(b) Kufunga gunzi la mhindi lina maana gani kwa mmea kama mpapai usio zaa ili uzae??
- Tunachokijua
- Mpapai ni mti wa familia Caricaceae ambao unazaa mapapai. Mti huo unatoka Meksiko lakini siku hizi hukuzwa kila mahali katika ukanda wa tropiki kwa sababu matunda yake hupendwa sana.
Mpapai dume ni mti wa mpapai ambao ukikomaa hutoa maua pekee na kuishia hapo, hauendelei kufikia hatua ya kutoa matunda, wakati mpapai jike wenyewe ukikomaa hutoa maua na kuendeleza hatua ya kutoa matunda.
Kufunga gunzi la mhindi lina maana gani kwa mmea kama mpapai usio zaa ili uzae?
Katika mimea inayoweza kubadili jinsia yake ‘sex labile plant’ mojawapo ni mipapai na inabadilika pale mazingira yatakapokua magumu kwa yenyewe kuishi, ili kuendeleze kizazi chake ni lazima ubadilike kutoka dume kuwa jike ile uweze kuacha kizazi chake.
Katika baadhi ya jamii ni suala la kawaida kufunga gunzi kwenye mpapai dume. Mipapai hiyo baada ya kufungwa gunzi hubadilika kuwa jike na kuanza kuzaa. Mingine ukiiondolea gunzi hurudi kuwa dume na kutoa maua badala ya kuzaa kama mwanzo.
Kufunga bunzi/gunzi ni watu wameaminishwa, ila unaweza kufunga chochote kile hata ukipigilia misumari ilimradi mmea upate shuruba ‘stress’ hapo mmea utahisi kuwa upo kwenye mazingira magumu na unaweza kufa muda wowote. Hapo mmea utachukua hatua ya kubadili jinsia na kuzaa matunda haraka sana kabla haujafa ili uache kizazi chake.
Kwa baadhi ya mimea kama miembe na miparachichi ukiipa shuruba, kwa kugongelea msumari au vinginevyo, miti hiyo ili kuacha kizazi huzaa matunda mengi sana.
Hivyo basi, hakuna mahusiano yoyote kati ya mpapai na gunzi au bunzi la mhindi bali kinachofanyika ni mpapai kupewa shurba(stress) na lile gunzi lililofungwa ndio hufanya mpapai uweze kuzaa kwa kuhisi utakufa, hivyo unaweza kufunga kitu chochote na si gunzi pekee.