Mpasuko CCM 2010

Mpasuko CCM 2010

kasyabone tall

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2009
Posts
254
Reaction score
63
  • Vita ya ufisadi yaijeruhi CCM
na Mwandishi Wetu

UCHAGUZI mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani, umegubikwa na sintofahamu kubwa, hasa kwa wagombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba, kuonekana akimpigia debe Spika wa Bunge na Mbunge wa Urambo, Samuel Sitta.

Hatua ya Makamba imetafsiriwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa kuwa ni kulipasua na kulivuruga kundi la wanamtandao ambalo lilifanikiwa kumpigia kampeni na hatimaye kufanikisha ushindi wa Rais Jakaya Kikwete, lakini hivi sasa limeonekana kwenda tofauti na Spika Sitta.

Sitta amekuwa akionekana mwiba mchungu kwa serikali na kundi hilo kutokana na namna anavyoruhusu mijadala mikali ya kuishambulia serikali na CCM, kiasi cha kutishiwa kupokonywa kadi ya uanachama katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM iliyoketi hivi karibuni mkoani Dodoma.

Kundi la wanamtandao, ambalo pia linawahusisha wanasiasa mbalimbali akiwamo Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Edward Lowassa (Monduli), katika siku za hivi karibuni limezidi kuzorota kutokana na kashfa mbalimbali za ufisadi zinazowakabili baadhi ya vinara wake.

Uzorotaji wa kundi hilo umechagizwa zaidi na taarifa za ushawishi alionao Lowassa na Rostam katika Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kiasi cha kuwafanya baadhi ya wanasiasa wenzao kuwa na wasiwasi wa Lowassa kuwania kiti cha urais mwaka 2010 kama akitaka kufanya hivyo.

Tetesi hizo zilikanushwa vikali na Lowassa ambaye mwanzoni mwa wiki hii alizungumza na baadhi ya vyombo vya habari na kubainisha kutokuwa na mpango wa kuwania kiti hicho kwa mwakani na kuongeza kuwa taarifa hizo zina lengo la kuwakosanisha na Rais Jakaya Kikwete ambaye ni rafiki yake wa siku nyingi.

Kuibuka kwa Makamba akiwa na Sitta katika mkutano huko Urambo, kumezidi kuimarisha kundi la wabunge waliojipambanua kuwa ni wapiga vita ya ufisadi, ambalo kwa muda mrefu lilikuwa likiangaliwa kwa jicho la uchochezi, huku kukiwapo taarifa za kupandikiziwa watu ili wasiweze kupata ubunge.

Kundi hilo linawajumuisha Lucas Selelii (Nzega), Dk. Harisson Mwakyembe (Kyela), Christopher ole Sendeka (Simanjiro), James Lembeli (Kahama) na Fred Mpendazoe (Kishapu).

Makamba ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipata shinikizo la kujiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kukigawa chama katika makundi na kumuunga mkono Spika Sitta hivi sasa, anaonekana kuwa na ajenda nzito moyoni kuhusu uamuzi wake huo uliowashangaza watu wengi, licha ya wadhifa wake kumpa fursa ya kushiriki mikutano mbalimbali na wabunge.

Baadhi ya wanasiasa waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili, wamesema hatua hiyo huenda ikawa ni kutokana na upepo wa wapambanaji wa ufisadi kuilemea CCM ndiyo maana Makamba na viongozi wengine wameamua kubadilika.

“Unajua asilimia kubwa ya watu wangependa vita ya ufisadi isambae nchi nzima, sasa wanapotokea viongozi au chama kinakwaza mpambano wa vita hiyo kuna hatari ya kukosa kura za wananchi, ndiyo maana CCM wameamua kujisafisha,” alisema kada wa CCM ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Wengine wametafsiri hatua hiyo kuwa huenda ni mbinu za kuwaziba midomo wabunge hao ili ionekane vita hiyo ni ya chama badala ya inavyoonekana hivi sasa ni ya wabunge wachache ambao wamejizolea sifa kemkemu, kiasi cha kuwaogopesha viongozi wa juu wa chama hicho.

Hofu hiyo ya watu imetupiliwa mbali na Makamba, ambaye alidai kuwa rushwa ni adui wa haki na CCM imeapa kupambana nayo, hivyo yeyote mwenye kupambana nayo anatekeleza wajibu wake na sera za chama.

Makamba alisema hana ugomvi wowote na Sitta, ndiyo maana amekwenda Urambo kuwasisitiza wananchi wa huko wamchague spika huyo, kwa kuwa amefanya kazi nzuri, licha ya kupata wakati mgumu kutoka ndani na nje ya chama.

Amebainisha kuwa propaganda zinazoenezwa na watu kuwa wana ugomvi zina lengo baya, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu na mkuu utakaofanyika mwakani.

Wakati hatua hiyo ya Makamba ikizusha maswali, chanzo kimoja cha habari kimeidokeza Tanzania Daima Jumapili kuwa hivi sasa kundi la wanamtandao limekuwa likifanya jitihada za kujisuka upya, hasa baada ya kupata majeraha ya kashfa ya Richmond, ambayo ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu, akifuatiwa na mawaziri wawili, Dk. Ibrahim Msabaha na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.

Kuanza kujisuka upya kwa wanamtandao kumetabiriwa kutoa wakati mgumu kwa uchaguzi mkuu wa mwakani, hasa katika ngazi ya ubunge, kwa kuwa tayari kuna madai kwamba baadhi ya watu wanatembeza fedha majimboni ili wabunge wanaopambana na ufisadi wasiweze kurejea bungeni.
 
Nimejitahidi kuutafuta huo unaoitwa mpasuko ndani ya hii habari nimeshindwa kuuona. Ninachokiona ni kujipendekeza kwa Makamba tu na sidhani kama kitendo hicho tunaweza kukiia mopasuko ndani ya CCM. Unless kungekuwa na uthibitisho kuwa alichofanya Makamba kulitokana na kutumwa na chama chake...
 
Mwandishi ameandika makala ambayo haiendani na kichwa. Lakini ni fact kuwa Makamba ameona kuwa njia anayoifuata haitamfikisha mbali, na ni kaburi lake kisiasa, ameona ni vema kujipendekeza kwa Sitta kuliko kuendelea kuwatetea mafisadi.
Mpasuko CCM ni obvious na utaonekana zaidi 2010, sasa hivi kuna theory ya mpasuko, naona 2010 kutakuwa na practical ya mpasuko. Naona Makamaba ametumia busara, hata kama ameambiwa na wengine naona Motto ameuona. Amehisi kuwa it is very possible kuwa Six anaweza kuwa magogoni 2010.
 
Hata hivyo ni mwanzo mzuri kwa kuwa Mafisadi wanaendelea kupigika.
 
mi nilishasema kuwa kumkomalia sitta ni kukosea kwa kiwango kikubwa na kujiumbua zaidi kwa ccm hii ni kutokana na sababu hasa zilizoifanya nec kumsulubu sitta kwani kila ambaye alikuwa hajui atatafuta ajue tatizo liko wapi na baada ya kujua inadhihirika kuwa kumbe ccm ni kifupi cha chama cha mafisadi na watetea ufisadi........wameumbuka na sasa wanatapatapa.Siku zote penye ukweli uongo hujitenga wenyewe.........
 
..habari nzuri sana hii hata kama haina ukweli,lakini anything bad kwa CCM ni nzuri kwa Taifa letu!
 
Mwandishi ameandika makala ambayo haiendani na kichwa. ....
Nimejitahidi kuutafuta huo unaoitwa mpasuko ndani ya hii habari nimeshindwa kuuona. ......

Wakuu,
Vilaza na wavivu wa kufikiri hawapo CCM na serikalini tu, kona zote wamejaa, na waandishi wengi wa magazeti mara nyingi wametuonesha hivyo! Nadhani mara nyingi wanaandika kitu na hata wao wenyewe ukiwauliza wameandika nini wanaweza washindwe kukueleza
 
..habari nzuri sana hii hata kama haina ukweli,lakini anything bad kwa CCM ni nzuri kwa Taifa letu!

Wishful thinking, ni sawa na yule fisi aliyengojea mkono wa binadamu uanguke huku mate yakimtoka!!
CCM under JK imeruhusu kila mtu atoe mawazo yake na tunashuhudia pumba ni ipi na mchele ni upi.
Kwa wale waliopitia DS tunashuhudia class struggle ndani ya CCM lakini kamwe haianguki!!
 
Back
Top Bottom