Pre GE2025 Mpasuko wa CHADEMA tatizo ni Asali, Ukabila na Uenyekiti Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa muda mrefu sana, CHADEMA wamekuwa wakilaumu kukwama kwa maridhiano kwa sababu ya CCM kutokukubaliana na madai yao mengi. Jambo hili liliwashangaza Watanzania wengi wanaofuatilia siasa, kwani ni CHADEMA wenyewe waliotamka kuwa moja ya masharti ya kuanza maridhiano ilikuwa ni kuachiliwa kwa Mwenyekiti wao, Mbowe, kutoka mahabusu. CCM imefanya juhudi nyingi kuhakikisha mchakato wa maridhiano unaanza, hivyo wengi wetu tulisita kuamini kuwa CCM ilikataa mawazo yote ya CHADEMA.

Kuna msemo mmoja usemao, “Wakati uongo unachukua lifti, ukweli huchukua ngazi.” Msemo huu unamaanisha kwamba daima uongo husambaa kwa haraka zaidi kuliko ukweli. Hatimaye, uchaguzi wa ndani wa CHADEMA, hususan wa uenyekiti wa Kanda ya Nyasa kati ya Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi (Sugu), umefichua mengi yaliyokuwa yamejificha ndani ya chama chao na kuyaweka wazi mbele ya umma.

Cha kwanza ni kuhusu maridhiano. Kuna tetesi za kuaminika zikionesha kwamba wengi waliowachwa nje ya kamati ya maridhiano ya CHADEMA, akiwemo Msigwa, wanaamini kwamba Mbowe pamoja na kamati hiyo walipewa "asali" na serikali ya awamu ya sita. Sote tunajua hilo sio kweli, lakini ndio imani ya wale ambao hawakujumuishwa kwenye kamati hiyo. Hapo ndipo tulipoanza kuona baadhi ya viongozi wa CHADEMA aidha wakikubaliana na maridhiano au wakiyapinga. Ni dhahiri sasa kuwa waliokuwa wakiyapinga waliamini kwamba kuna fursa fulani wamelikosa.

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi uliopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, alifanya kikao na wananchi kufafanua masuala kadhaa. Moja ya mambo aliyotoa ufafanuzi ni kuhusu maridhiano na kwamba sababu kuu ya CHADEMA kujitoa ilikuwa ni kwa sababu hawakutaka vyama vingine vya upinzani vishirikishwe. Hii inanipelekea kuamini kwamba yawezekana CHADEMA walihisi vyama vingine vikishirikishwa basi watapoteza nguvu ya kudai pesa kutoka CCM. Inasikitisha sana kuona viongozi wakubwa wakiamua kuua mchakato wenye maslahi mapana kwa umma kwa ajili ya maslahi binafsi, lakini ndio uhalisia uliokuwepo.

Hizo pesa zinazodhaniwa kutolewa katika mchakato wa maridhiano pia ndizo chanzo cha kutokuelewana kati ya viongozi wakuu wa CHADEMA. Hivi sasa, CHADEMA imegawanyika katika makundi mawili, moja likimuunga mkono mwenyekiti na jingine likimpinga. Wanaompinga Mbowe wanaamini kuwa mwenyekiti huyo ana kundi lake la watu ambao ndio pekee wanaofaidika na chama. Ingawa wengi wanakana kuendeshwa na maslahi binafsi, ushahidi wa kimazingira unaonyesha wazi hali hiyo. Kumbuka Msigwa alishutumu kwamba Sugu ni mtu wa Mbowe na kwamba kulikuwa na pesa nyingi sana zilizotumika kuhakikisha yeye, Msigwa, anatupwa chini. Msigwa pia alimshutumu John Mrema, msemaji wa chama, kwa kuja Iringa na kunywa pombe na wagombea na wanachama waliokuwa upande wa Sugu.

Kwenye magrupu ya mazungumzo ya WhatsApp ya CHADEMA, kuna vita kubwa ya maneno inayoendelea. Inasemekana kwamba Msigwa anamshutumu mwenyekiti wa chama chao, Freeman Mbowe, kuwa ni mwizi, mhuni na kibaka—maneno mazito sana kutamka kuhusu kiongozi mkuu wa chama. Msigwa hamchukulii Mbowe kama bosi wake ndani ya chama, bali anamchukulia kama mfanyakazi mwenzake. Hii inatosha kuonyesha mpasuko uliopo. Ndio maana Msigwa anapigana vita na “mfanyakazi mwenzie” ambaye anahisi anafaidika zaidi na chama kuliko yeye.

Kwa upande mwingine, wale walioko upande wa Mbowe wamemtuhumu Msigwa kuwa amepokea pesa kutoka kwa Abdul, mtoto wa Rais Samia, ili kukivuruga chama chao. Kama mnakumbuka vizuri, wakati wa uchaguzi wa Kanda ya Nyasa, Makamu Mwenyekiti wao, Tundu Lissu, alitoa madai hadharani kwamba kuna watu waliolipwa ili kuivuruga CHADEMA kutoka ndani. Ajabu ni kwamba kila upande kwa sasa inadai upande wa pili umepokea hela kutoka CCM kupitia mtoto wa rais. Wameamua kwamba kwenye kupakana matope wao watahakikisha wanampaka matope na rais wa nchi.

Kwenye magrupu hayo ya WhatsApp ya CHADEMA, pia kuna shutuma za ukabila, huku Msigwa akidai kuwa kuna Wachagga ndani ya chama ambao wapo upande wa Mbowe kwa sababu ya kabila tu. Sio siri kwamba CHADEMA siku zote imekuwa na taswira ya chama cha kaskazini na cha Kikristo. Ikiwa shutuma hizi za ndani ni za kweli, basi ni hatari sana kwa ustawi wa nchi yetu. Ukweli ni kwamba CHADEMA siku zote imekua chama cha kikanda ambacho kwa njia za ulaghai wa kisiasa umeweza aminisha umma kuwa ni chama cha Watanzania wote. Ni wakati sasa Watanzania wafungue macho waone kitu ambacho kiko mbele yao.

Inaonekana wazi kwamba kwa sasa Msigwa hana nafasi tena ndani ya CHADEMA. Hii ni dhahiri kutokana na tukio la uchaguzi wa kanda ya Nyasa, ambapo vijana wa CHADEMA walitumika kumshambulia na kumchafua mbele ya umma. Vijana hao ni wale ambao mara nyingi huitwa askari wa kulipwa, wanaojulikana kufanya kazi kwa upande wowote unaotoa malipo ya kutosha. Hata katika magrupu yao ya WhatsApp, kuna kampeni za kumchafua Msigwa na kumshinikiza aondoke. Wanamuita mamluki na wanamshutumu kupokea fedha ili kuidhoofisha CHADEMA, lakini kwa kushangaza, hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi yake ndani ya chama.

Lakini ujumbe kwa Watanzania uko wazi: CHADEMA hawafai kuongoza nchi na kusimamia vyombo vya ulinzi, usalama, na fedha za nchi hii. Itakuwa kosa kubwa sana kwa Watanzania kuiamini bucha hii kwa watu ambao wameonyesha kuwa hawana maadili. Ni wazi kwamba CHADEMA wakichukua madaraka, vyombo vya ulinzi na usalama vitaanza kutumiwa kisiasa, hazina ya nchi itageuzwa kuwa pochi binafsi ya viongozi wakuu wa CHADEMA na washirika wao, na maeneo ya kaskazini yatapewa kipaumbele huku yakipendelewa kuliko maeneo mengine nchini.

CCM ina mapungufu yake kama ilivyo kwa kila chombo kilichoumbwa, lakini ukweli nilio nao ni kwamba CCM inawajibika kwa ustawi wa wote na maslahi ya taifa zima. Katika miaka zaidi ya 60 ya utawala wa CCM, hakuna eneo lolote nchini lililopendelewa au kupuuziwa kwa makusudi. Mfumo huu umethibitisha kuwa nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa muda wote huo. Tujumuike kwa pamoja kukataa wote wanaotishia mfumo huu wa utulivu ambao umekuwa msingi wa maendeleo kwa Watanzania.

Tanzania ina sifa ya kukataa vyama vya aina kama CHADEMA. Sote tunatambua jinsi historia ilivyoathiri chama cha CUF, ambacho kilikuwa chama cha upinzani pekee kilichokuwa na ushawishi pande zote za Muungano. CUF ilikabiliwa na shutuma za kuwa chama cha Kiislamu na kilichopata nguvu kubwa katika ukanda wa Pwani. Ingawa ilichukua muda mrefu, mwishowe wananchi walikataa madai hayo. Matokeo yake yanafanana na yale tunayoyaona sasa, ambapo viongozi wakuu wamegawanyika katika kambi mbili tofauti, hali ambayo imepelekea kufifia kwa chama hicho.

View attachment 3014526
Source:Wamachinga News, za moto moto!!!
 
Mbowe akigombea 2025 na uchaga wake watapta 0.5% wasisubutu afadhali hata ys Lissu wajaribishe. Tanzania ina allergy na uchaga kumbukeni ya kauli ya Ridhiwan 2015
 
Wakuu sana Waungwana JF, Amani ya Bwana ikae Nanyi

Sina nia ya Kuwa Mdini, ila kuna Fact moja lazima isemwe.

Kuna Ndugu zetu ambao kila Uchwao wamekuwa wakipiga Propaganda Mfu ya Kukihusisha CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) Kuwa ni chama cha Ki Kabila (Chaga) na Chama cha Kidini (Ki Kristo)

Nimewa Observe kwa Karibu sana hawa ndugu zangu, hasa wanaobeba Propaganda Mfu kuwa CHADEMA ni Cha Ki Kristo tangia tukio la Kuuawa Kinyama na watu wenye roho za Ibilisi Mzee Ally Mohamed Kibao

Watu hawa waliokuwa wanabeba Propaganda kuwa CHADEMA ni chama cha Kikristo kwa sasa wako Njia Panda.

Wanashindwa kulaani tukio la Mauaji ya Kinyama ya Ally Kibao na pia wanashindwa kukejeli kuwa CHADEMA Wanatekana na Kuuana wenyewe kwa wenyewe.

RIP Mzee Ally Kibao
Waliokuua (Kuanzia waliopanga, waliofadhili na watekelezaji)Mungu atakulipizia, kuanzia wao Mpaka Uzao was wao Saba
 
Hatuwezi kuongozwa na CHADEMA ..Ally kibao kauliwa wala hamna uhusiano maana ni sehemu ya CHADEMA.
 
Chadema ni chama cha kifamilia ndio maana halima mdee kushtukia mchongo akakaba lof hakuna kuachia ukoo wapeane nafasi za uongozi wakati yeye chama amekijenga kwa machozi jasho na damu huku akikatwa posho yake kila mwezi mil 2!
Mke wa profesa j nae amepewa uweka hazina!
Kwa hiyo hawa wanaoitafuna nchi kama fisi anakula mifupa na kuendelea kurithishana na kupeana posts sio wa kifamilia.

Kakojoe then ukalale wananchi wanahitaji mabadiliko.
 
Chadema ni chama cha kifamilia ndio maana halima mdee kushtukia mchongo akakaba lof hakuna kuachia ukoo wapeane nafasi za uongozi wakati yeye chama amekijenga kwa machozi jasho na damu huku akikatwa posho yake kila mwezi mil 2!
Mke wa profesa j nae amepewa uweka hazina!
Kwahiyo Kikwete, Salma na Ridhiwani, ndugu zako? Mwinyi, Husen, Saa 100 nao je? Karume family je? Nauye family je?. Jiongeze kwenye koo hizo. Hicho chama unachoshabikia ndo saccos yao. Wengine mnasindikiza
 
Mods hamna maana hata kidogo uzi huu kuunga na huu uzi mfu unafananaje mauzui yake upuuzi ndio mwingi mnachosha siku hizi bora mngeufuta tu kuliko kuunga mnajifanyia tu ili mtu achoke uhanithi mumfungie!
 
Kwa muda mrefu sana, CHADEMA wamekuwa wakilaumu kukwama kwa maridhiano kwa sababu ya CCM kutokukubaliana na madai yao mengi. Jambo hili liliwashangaza Watanzania wengi wanaofuatilia siasa, kwani ni CHADEMA wenyewe waliotamka kuwa moja ya masharti ya kuanza maridhiano ilikuwa ni kuachiliwa kwa Mwenyekiti wao, Mbowe, kutoka mahabusu. CCM imefanya juhudi nyingi kuhakikisha mchakato wa maridhiano unaanza, hivyo wengi wetu tulisita kuamini kuwa CCM ilikataa mawazo yote ya CHADEMA.

Kuna msemo mmoja usemao, “Wakati uongo unachukua lifti, ukweli huchukua ngazi.” Msemo huu unamaanisha kwamba daima uongo husambaa kwa haraka zaidi kuliko ukweli. Hatimaye, uchaguzi wa ndani wa CHADEMA, hususan wa uenyekiti wa Kanda ya Nyasa kati ya Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi (Sugu), umefichua mengi yaliyokuwa yamejificha ndani ya chama chao na kuyaweka wazi mbele ya umma.

Cha kwanza ni kuhusu maridhiano. Kuna tetesi za kuaminika zikionesha kwamba wengi waliowachwa nje ya kamati ya maridhiano ya CHADEMA, akiwemo Msigwa, wanaamini kwamba Mbowe pamoja na kamati hiyo walipewa "asali" na serikali ya awamu ya sita. Sote tunajua hilo sio kweli, lakini ndio imani ya wale ambao hawakujumuishwa kwenye kamati hiyo. Hapo ndipo tulipoanza kuona baadhi ya viongozi wa CHADEMA aidha wakikubaliana na maridhiano au wakiyapinga. Ni dhahiri sasa kuwa waliokuwa wakiyapinga waliamini kwamba kuna fursa fulani wamelikosa.

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi uliopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, alifanya kikao na wananchi kufafanua masuala kadhaa. Moja ya mambo aliyotoa ufafanuzi ni kuhusu maridhiano na kwamba sababu kuu ya CHADEMA kujitoa ilikuwa ni kwa sababu hawakutaka vyama vingine vya upinzani vishirikishwe. Hii inanipelekea kuamini kwamba yawezekana CHADEMA walihisi vyama vingine vikishirikishwa basi watapoteza nguvu ya kudai pesa kutoka CCM. Inasikitisha sana kuona viongozi wakubwa wakiamua kuua mchakato wenye maslahi mapana kwa umma kwa ajili ya maslahi binafsi, lakini ndio uhalisia uliokuwepo.

Hizo pesa zinazodhaniwa kutolewa katika mchakato wa maridhiano pia ndizo chanzo cha kutokuelewana kati ya viongozi wakuu wa CHADEMA. Hivi sasa, CHADEMA imegawanyika katika makundi mawili, moja likimuunga mkono mwenyekiti na jingine likimpinga. Wanaompinga Mbowe wanaamini kuwa mwenyekiti huyo ana kundi lake la watu ambao ndio pekee wanaofaidika na chama. Ingawa wengi wanakana kuendeshwa na maslahi binafsi, ushahidi wa kimazingira unaonyesha wazi hali hiyo. Kumbuka Msigwa alishutumu kwamba Sugu ni mtu wa Mbowe na kwamba kulikuwa na pesa nyingi sana zilizotumika kuhakikisha yeye, Msigwa, anatupwa chini. Msigwa pia alimshutumu John Mrema, msemaji wa chama, kwa kuja Iringa na kunywa pombe na wagombea na wanachama waliokuwa upande wa Sugu.

Kwenye magrupu ya mazungumzo ya WhatsApp ya CHADEMA, kuna vita kubwa ya maneno inayoendelea. Inasemekana kwamba Msigwa anamshutumu mwenyekiti wa chama chao, Freeman Mbowe, kuwa ni mwizi, mhuni na kibaka—maneno mazito sana kutamka kuhusu kiongozi mkuu wa chama. Msigwa hamchukulii Mbowe kama bosi wake ndani ya chama, bali anamchukulia kama mfanyakazi mwenzake. Hii inatosha kuonyesha mpasuko uliopo. Ndio maana Msigwa anapigana vita na “mfanyakazi mwenzie” ambaye anahisi anafaidika zaidi na chama kuliko yeye.

Kwa upande mwingine, wale walioko upande wa Mbowe wamemtuhumu Msigwa kuwa amepokea pesa kutoka kwa Abdul, mtoto wa Rais Samia, ili kukivuruga chama chao. Kama mnakumbuka vizuri, wakati wa uchaguzi wa Kanda ya Nyasa, Makamu Mwenyekiti wao, Tundu Lissu, alitoa madai hadharani kwamba kuna watu waliolipwa ili kuivuruga CHADEMA kutoka ndani. Ajabu ni kwamba kila upande kwa sasa inadai upande wa pili umepokea hela kutoka CCM kupitia mtoto wa rais. Wameamua kwamba kwenye kupakana matope wao watahakikisha wanampaka matope na rais wa nchi.

Kwenye magrupu hayo ya WhatsApp ya CHADEMA, pia kuna shutuma za ukabila, huku Msigwa akidai kuwa kuna Wachagga ndani ya chama ambao wapo upande wa Mbowe kwa sababu ya kabila tu. Sio siri kwamba CHADEMA siku zote imekuwa na taswira ya chama cha kaskazini na cha Kikristo. Ikiwa shutuma hizi za ndani ni za kweli, basi ni hatari sana kwa ustawi wa nchi yetu. Ukweli ni kwamba CHADEMA siku zote imekua chama cha kikanda ambacho kwa njia za ulaghai wa kisiasa umeweza aminisha umma kuwa ni chama cha Watanzania wote. Ni wakati sasa Watanzania wafungue macho waone kitu ambacho kiko mbele yao.

Inaonekana wazi kwamba kwa sasa Msigwa hana nafasi tena ndani ya CHADEMA. Hii ni dhahiri kutokana na tukio la uchaguzi wa kanda ya Nyasa, ambapo vijana wa CHADEMA walitumika kumshambulia na kumchafua mbele ya umma. Vijana hao ni wale ambao mara nyingi huitwa askari wa kulipwa, wanaojulikana kufanya kazi kwa upande wowote unaotoa malipo ya kutosha. Hata katika magrupu yao ya WhatsApp, kuna kampeni za kumchafua Msigwa na kumshinikiza aondoke. Wanamuita mamluki na wanamshutumu kupokea fedha ili kuidhoofisha CHADEMA, lakini kwa kushangaza, hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi yake ndani ya chama.

Lakini ujumbe kwa Watanzania uko wazi: CHADEMA hawafai kuongoza nchi na kusimamia vyombo vya ulinzi, usalama, na fedha za nchi hii. Itakuwa kosa kubwa sana kwa Watanzania kuiamini bucha hii kwa watu ambao wameonyesha kuwa hawana maadili. Ni wazi kwamba CHADEMA wakichukua madaraka, vyombo vya ulinzi na usalama vitaanza kutumiwa kisiasa, hazina ya nchi itageuzwa kuwa pochi binafsi ya viongozi wakuu wa CHADEMA na washirika wao, na maeneo ya kaskazini yatapewa kipaumbele huku yakipendelewa kuliko maeneo mengine nchini.

CCM ina mapungufu yake kama ilivyo kwa kila chombo kilichoumbwa, lakini ukweli nilio nao ni kwamba CCM inawajibika kwa ustawi wa wote na maslahi ya taifa zima. Katika miaka zaidi ya 60 ya utawala wa CCM, hakuna eneo lolote nchini lililopendelewa au kupuuziwa kwa makusudi. Mfumo huu umethibitisha kuwa nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa muda wote huo. Tujumuike kwa pamoja kukataa wote wanaotishia mfumo huu wa utulivu ambao umekuwa msingi wa maendeleo kwa Watanzania.

Tanzania ina sifa ya kukataa vyama vya aina kama CHADEMA. Sote tunatambua jinsi historia ilivyoathiri chama cha CUF, ambacho kilikuwa chama cha upinzani pekee kilichokuwa na ushawishi pande zote za Muungano. CUF ilikabiliwa na shutuma za kuwa chama cha Kiislamu na kilichopata nguvu kubwa katika ukanda wa Pwani. Ingawa ilichukua muda mrefu, mwishowe wananchi walikataa madai hayo. Matokeo yake yanafanana na yale tunayoyaona sasa, ambapo viongozi wakuu wamegawanyika katika kambi mbili tofauti, hali ambayo imepelekea kufifia kwa chama hicho.

View attachment 3014526
Unaandika issues Nyingi upuuuzi tuu
 
Mods hamna maana hata kidogo uzi huu kuunga na huu uzi mfu unafananaje mauzui yake upuuzi ndio mwingi mnachosha siku hizi bora mngeufuta tu kuliko kuunga mnajifanyia tu ili mtu achoke uhanithi mumfungie!
Tuliza mshono hujapona sawasawa
 
Tukisema Kuna watu wapumbavu hii nchi mnakua wakali.Chadema Iko mbeya,Tanga,kigoma,kagera ,mtwara nk nk nk nk kote huko ni wachaga???Ficheni ujinga basi
 
Mimi sio mwanasiasa wala mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, na wala sio social scientist bali nipo kwenye natural sciences. Kwa mujibu wa research nazofanya mojawapo ni qualitative ambayo haihitaji empirical data, tunapata conclusions kwa human perceptions, feelings, thoughts, says, mitazamo, mazungumzo, reactions, nk nk.

Kwa ujumla utafiti wangu usio rasmi qualitatively, naona Chadema ni lidude moja kubwa mno na linalotisha sana kwa kutazama namna reactions, na qualitative data zilizopo humu JF, radioni, social media zingine, TV, blogs, Polisi, jeshini, mitaani, magengeni, chats, groups za chawas etc. hamna siku chadema haijatajwa mara 10 hadi 20! Kuanzia mama yao/yetu akilala, akiamka, akiongea, akiwaza, chadema inazunguka kichwani kwake, makondeko kule kwa landrover kila akiamka, makalai kwenye mizunguko yake ya perdiem, joni nchambi, tulizo kule dom, mcheza kiduku wa daslam, hapi, mkumbwa, cc yote ya ccm, machawa wazoefu na wapya kote mitandaoni, mwashamba, talalalah, choicevariable, yohana mbatizaji, na wengine lukuki. Polisi ndio wakisikia kuanzia kaka yao mkubwa anayevaa official dress na buti hata kwenye sherehe ikulu kama yupo vitani ndio wanapagawa kabisa na kuitana nchi nzima, na kuwasha mazimamoto yao ya kipigaji. Hili dude linawatisha sana kisaikolijia.

My conclusion kwa haya naona chadema sasa niifananishe na maji kwa kweli, yani ni lazima uyatumie tu ili uishi, kuna watu kwa kuitajataja tu wamepata uwaziri, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa, ubunge, uchawa rasmi, ukatibu-kata na uenezi wa ccm, wengine wakapigwa na pesa, wengine ubalozi, wengine ucovid-19 sasa hii si sawa na maji tu wandugu??

Yani utake usitake utayanywa, usipoyanywa utayaoga, usipoyaoga utafulia, usipoyafulia utapikia, usipopikia utaoshea hata tongotongo. Ili tumbo lako lisitirike kwa sasa we andika, taja, waza, ongea kuhusu chadema, ukiongelea mwengine unafutika tu kama upepo. Relavance yako itakuja kwa kusema chademaaaaa, chademaaaa hata kama huna logic km mwashamba.

Yani kuna watu wasipotaja chadema wanapotea so ili wawe relevant lazima kila siku waje na uzi kuhusu chadema tu, gosh!! Wengine hata spelling hawajui lkn chadema ipo midomoni mwao kutwa kucha.

No offence hii ni perception ya jamii ya watanzania kuanzia mama yetu shuka chini hadi kwa machawa wa level za chini kbs kama hapa nilipo cholesamvula.
 
Kwa muda mrefu sana, CHADEMA wamekuwa wakilaumu kukwama kwa maridhiano kwa sababu ya CCM kutokukubaliana na madai yao mengi. Jambo hili liliwashangaza Watanzania wengi wanaofuatilia siasa, kwani ni CHADEMA wenyewe waliotamka kuwa moja ya masharti ya kuanza maridhiano ilikuwa ni kuachiliwa kwa Mwenyekiti wao, Mbowe, kutoka mahabusu. CCM imefanya juhudi nyingi kuhakikisha mchakato wa maridhiano unaanza, hivyo wengi wetu tulisita kuamini kuwa CCM ilikataa mawazo yote ya CHADEMA.

Kuna msemo mmoja usemao, “Wakati uongo unachukua lifti, ukweli huchukua ngazi.” Msemo huu unamaanisha kwamba daima uongo husambaa kwa haraka zaidi kuliko ukweli. Hatimaye, uchaguzi wa ndani wa CHADEMA, hususan wa uenyekiti wa Kanda ya Nyasa kati ya Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi (Sugu), umefichua mengi yaliyokuwa yamejificha ndani ya chama chao na kuyaweka wazi mbele ya umma.

Cha kwanza ni kuhusu maridhiano. Kuna tetesi za kuaminika zikionesha kwamba wengi waliowachwa nje ya kamati ya maridhiano ya CHADEMA, akiwemo Msigwa, wanaamini kwamba Mbowe pamoja na kamati hiyo walipewa "asali" na serikali ya awamu ya sita. Sote tunajua hilo sio kweli, lakini ndio imani ya wale ambao hawakujumuishwa kwenye kamati hiyo. Hapo ndipo tulipoanza kuona baadhi ya viongozi wa CHADEMA aidha wakikubaliana na maridhiano au wakiyapinga. Ni dhahiri sasa kuwa waliokuwa wakiyapinga waliamini kwamba kuna fursa fulani wamelikosa.

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi uliopita, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, alifanya kikao na wananchi kufafanua masuala kadhaa. Moja ya mambo aliyotoa ufafanuzi ni kuhusu maridhiano na kwamba sababu kuu ya CHADEMA kujitoa ilikuwa ni kwa sababu hawakutaka vyama vingine vya upinzani vishirikishwe. Hii inanipelekea kuamini kwamba yawezekana CHADEMA walihisi vyama vingine vikishirikishwa basi watapoteza nguvu ya kudai pesa kutoka CCM. Inasikitisha sana kuona viongozi wakubwa wakiamua kuua mchakato wenye maslahi mapana kwa umma kwa ajili ya maslahi binafsi, lakini ndio uhalisia uliokuwepo.

Hizo pesa zinazodhaniwa kutolewa katika mchakato wa maridhiano pia ndizo chanzo cha kutokuelewana kati ya viongozi wakuu wa CHADEMA. Hivi sasa, CHADEMA imegawanyika katika makundi mawili, moja likimuunga mkono mwenyekiti na jingine likimpinga. Wanaompinga Mbowe wanaamini kuwa mwenyekiti huyo ana kundi lake la watu ambao ndio pekee wanaofaidika na chama. Ingawa wengi wanakana kuendeshwa na maslahi binafsi, ushahidi wa kimazingira unaonyesha wazi hali hiyo. Kumbuka Msigwa alishutumu kwamba Sugu ni mtu wa Mbowe na kwamba kulikuwa na pesa nyingi sana zilizotumika kuhakikisha yeye, Msigwa, anatupwa chini. Msigwa pia alimshutumu John Mrema, msemaji wa chama, kwa kuja Iringa na kunywa pombe na wagombea na wanachama waliokuwa upande wa Sugu.

Kwenye magrupu ya mazungumzo ya WhatsApp ya CHADEMA, kuna vita kubwa ya maneno inayoendelea. Inasemekana kwamba Msigwa anamshutumu mwenyekiti wa chama chao, Freeman Mbowe, kuwa ni mwizi, mhuni na kibaka—maneno mazito sana kutamka kuhusu kiongozi mkuu wa chama. Msigwa hamchukulii Mbowe kama bosi wake ndani ya chama, bali anamchukulia kama mfanyakazi mwenzake. Hii inatosha kuonyesha mpasuko uliopo. Ndio maana Msigwa anapigana vita na “mfanyakazi mwenzie” ambaye anahisi anafaidika zaidi na chama kuliko yeye.

Kwa upande mwingine, wale walioko upande wa Mbowe wamemtuhumu Msigwa kuwa amepokea pesa kutoka kwa Abdul, mtoto wa Rais Samia, ili kukivuruga chama chao. Kama mnakumbuka vizuri, wakati wa uchaguzi wa Kanda ya Nyasa, Makamu Mwenyekiti wao, Tundu Lissu, alitoa madai hadharani kwamba kuna watu waliolipwa ili kuivuruga CHADEMA kutoka ndani. Ajabu ni kwamba kila upande kwa sasa inadai upande wa pili umepokea hela kutoka CCM kupitia mtoto wa rais. Wameamua kwamba kwenye kupakana matope wao watahakikisha wanampaka matope na rais wa nchi.

Kwenye magrupu hayo ya WhatsApp ya CHADEMA, pia kuna shutuma za ukabila, huku Msigwa akidai kuwa kuna Wachagga ndani ya chama ambao wapo upande wa Mbowe kwa sababu ya kabila tu. Sio siri kwamba CHADEMA siku zote imekuwa na taswira ya chama cha kaskazini na cha Kikristo. Ikiwa shutuma hizi za ndani ni za kweli, basi ni hatari sana kwa ustawi wa nchi yetu. Ukweli ni kwamba CHADEMA siku zote imekua chama cha kikanda ambacho kwa njia za ulaghai wa kisiasa umeweza aminisha umma kuwa ni chama cha Watanzania wote. Ni wakati sasa Watanzania wafungue macho waone kitu ambacho kiko mbele yao.

Inaonekana wazi kwamba kwa sasa Msigwa hana nafasi tena ndani ya CHADEMA. Hii ni dhahiri kutokana na tukio la uchaguzi wa kanda ya Nyasa, ambapo vijana wa CHADEMA walitumika kumshambulia na kumchafua mbele ya umma. Vijana hao ni wale ambao mara nyingi huitwa askari wa kulipwa, wanaojulikana kufanya kazi kwa upande wowote unaotoa malipo ya kutosha. Hata katika magrupu yao ya WhatsApp, kuna kampeni za kumchafua Msigwa na kumshinikiza aondoke. Wanamuita mamluki na wanamshutumu kupokea fedha ili kuidhoofisha CHADEMA, lakini kwa kushangaza, hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi yake ndani ya chama.

Lakini ujumbe kwa Watanzania uko wazi: CHADEMA hawafai kuongoza nchi na kusimamia vyombo vya ulinzi, usalama, na fedha za nchi hii. Itakuwa kosa kubwa sana kwa Watanzania kuiamini bucha hii kwa watu ambao wameonyesha kuwa hawana maadili. Ni wazi kwamba CHADEMA wakichukua madaraka, vyombo vya ulinzi na usalama vitaanza kutumiwa kisiasa, hazina ya nchi itageuzwa kuwa pochi binafsi ya viongozi wakuu wa CHADEMA na washirika wao, na maeneo ya kaskazini yatapewa kipaumbele huku yakipendelewa kuliko maeneo mengine nchini.

CCM ina mapungufu yake kama ilivyo kwa kila chombo kilichoumbwa, lakini ukweli nilio nao ni kwamba CCM inawajibika kwa ustawi wa wote na maslahi ya taifa zima. Katika miaka zaidi ya 60 ya utawala wa CCM, hakuna eneo lolote nchini lililopendelewa au kupuuziwa kwa makusudi. Mfumo huu umethibitisha kuwa nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa muda wote huo. Tujumuike kwa pamoja kukataa wote wanaotishia mfumo huu wa utulivu ambao umekuwa msingi wa maendeleo kwa Watanzania.

Tanzania ina sifa ya kukataa vyama vya aina kama CHADEMA. Sote tunatambua jinsi historia ilivyoathiri chama cha CUF, ambacho kilikuwa chama cha upinzani pekee kilichokuwa na ushawishi pande zote za Muungano. CUF ilikabiliwa na shutuma za kuwa chama cha Kiislamu na kilichopata nguvu kubwa katika ukanda wa Pwani. Ingawa ilichukua muda mrefu, mwishowe wananchi walikataa madai hayo. Matokeo yake yanafanana na yale tunayoyaona sasa, ambapo viongozi wakuu wamegawanyika katika kambi mbili tofauti, hali ambayo imepelekea kufifia kwa chama hicho.

View attachment 3014526
Hypocrisy at it's finest, kwa unafiki tu saluti nyingi kwako.
Hearsay, thana na kujaribu kujifanya kama unafanya uchambuzi huku uki-push your own stupid agenda kana kwamba wote watakaosoma bandiko lako ni mbumbumbu wasio na uwezo wa kubaini unafiki wako.
Pathetic.
 
Back
Top Bottom