Mpendane mkiwa hai

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Nimeona tukumbushane hili

najua n tatizo la kila ukoo hivi karibuni pale mtu anapopata shida tunashindwa kusaidiana

anapokufa ama kuteseka ndio tunaanza kukimbizana

Leo nilikuwa kwenye msiba mmoja tegeta rip dada..huyu dada aliumwa kwa mda lakini ndugu hawakuwa wanamsaidia waka kumjali hata kidogo

hata palle ilipoanzishwa grp la wana ndugu jama namarafiki mwitikio ulikuwa mdogo sana sana

Leo hii Judy amelala zimepaki gari nzuri za kila aina ndugu wanapishana kuandika
200000
400000
300000
mmoja ambae n ndugu yao kabisa na ana hela mbaya na biashara kadhaa alichanga 50000 kwenye whatsup

Leo katangaza atanunua jeneza atalioia special hire mbili kwenda moshi na kurudi..na kaburi atajenga yeye

nawaza wakati anaumwa hizo hela wangemsaidia si zingemwongezea hata siku kadhaa..

NARUDIA TENA TUPENDANE TUKIWA HAI MUNGU NDIE ANAJUA UHAI WETU

BWANA YESU ASIFIWE
AASSALHAMALLEIKHUM
 
Leo hii Judy amelala zimepaki gari nzuri za kila aina ndugu wanapishana kuandika
200000
400000
300000
mmoja ambae n ndugu yao kabisa na ana hela mbaya na biashara kadhaa alichanga 50000 kwenye whatsup
Ni huzuni😔😔
 
HATA YESU KRISTO ANATUSISITIZA SANA TUPENDANA HAUWEZI KUSEMA UNAMPENDA YESU USIE MUONA WAKATI UNAMCHUKIA BINADAM MWENZIO UNAE MUONA NI UNAFIKI

NA HAMNA SEHEMU ZENYE UNAFIKI KAMA MISIBANI

YANI UKIWA MSIBANI LAZIMA UWE CHAWA KWA MUDA KILA STORY WEWE LAZIMA UWE UNAJIBU NDIO AU NI KWELI HATA KAMA NI UNOKO 😂
 
Komasava

What you reveal you can heal
Rip the beloved one .

Kuna kitabu cha four Agreement kimeelezea kuhusu Ku love each other.
 
Kulinda afya yako ni jukumu lako, ila kukupeleka futi sita ni jukumu letu......
Waiter ongezaaa balimi mbili za motroooooooooooooooooooo
 
Ni huzuni😔😔
Sana ndugu

Nakumbuka bibi yangu aliumwa nikamhudumia sana aghakan dual alikuwa anatumia Kadi ikafika hara wanae wako mbeya mwanza arusha hata kusema tutume kiasiflan kimsaidie mamayao...

Hgal ndio anakesha nae mwanzo mwisho...

Amekufa msiba nikapeleka kwangu..na alitamka wanangu hata kuja kunionaa nikifa nkamwambia hufi bibj akaomba akifija azikwe alipozikwa mama mbweni

Huwezi amini usiku ndugu wakijazana wanapishana kuandika mil..laki...nkasema hizihela mngekuja kumsaidia bibiyenu akiwa hai angewapenda sana

Mmoja wa wajomba bababke na bibi yangu baba mama mmoja..nilizidiwa cash ikawa hovyo nikampigia unaweza nisapoti hata laki nirudishe mwisho wa mwezi hahah akajibu kwani huyo bibi si ana wajukuu zake na watoto wake wapigie

Sikuya msiba anaandika lak 5 hahahaa akasema atalipia na jeneza woi nkasimama bibi nishalipiai gari jeneza na hivi naongea wanamalixia kujenga kaburi

Kaja wanae watatu oooh mamayetu anazikwa moshi nkawajibu amesema akazikwe alipozikwa mwanae na atakaejaribu kumpeleka moshi atakachokutana nacho asilaumiwe

Ukawamzozo chuki ooh sababu alikuwa anakaa kwake nkawajibu wala ķukaa kwangu kwa bibi n wajibu wangu.........

Nkakusanya yale mashekeli yao nkaenda nunua kreti za soda bia zakutosha tyu kukawa kama harusi vuta mbuzi wawili China mpaka bibi anazikwa amani

Sijui zinakuwaga pesa za kurujuwani??
 
Leo sio tu huzuni Imenikumbusha mbali sana kuhusu bibiyangu

Ndugu hawapendan te na wakiwa hai wanataka uondoke waonyeshane michango yaooo

kuna vifo watyu wanakufa sababu tu ya pesa kama kuwakimbia

Nikiwaza nilichokuwa nikisaini kwa bibiyangu nahisi kama sio kadi angekuwa miaka 10 iliopita ashakufa.....
 
Waafrica tuna phobia ya kuogopa na kuheshim maiti sana kuliko uhai!na hii inachangiwa na Dini zetu hizi dhaifu zinafundisha kujali na kusalia /kuswalia maiti kana kwamba inathamani kuliko uhai wa mtu!!

Huu ujinga ulipandikizwa na kumea na ngumu kuondoka huko mbeleni!
 
Sijui zinakuwaga pesa za kurujuwani??
Watu Wana Siri na pesa zao kaka,muhimu Kila mtu awe na pesa zake ,japo kushikana mkono kunatakiwa sema Kwa ss watu wamebadilikaa..

Na maishà yamebadilika pia
 
Sana RK
TUmeshakengeuka na hatuwezi kubadilika anyway...Allah atusitiri

Kama bibiyangu walitaka ati tuanzishe grp la michango ya msiba whatsup nkajibu nilianzisha akiwa hai hamkumsaidia mnataka kuoneyshanaa mnakimbilia maiti...
Haponshashtua mbilitatu walinimaindi
 
Mpendwa ; iko hivii: Mtu wakati akiwa katika Uhai na Afya yake nzuri labda anakuwa hajali anachoambiwa au kushauriwa, na pengine akiambia au kushauriwa anatoa maneno ya kashfa na kejeli. Sasa kama ikitokea Afya yake imetetereka na ikawa imetetereka katika yale yale waliyokuwa wanamshauri; basi wale watu waliokuwa wanatoa ushauri na maonyo kwake hukaa pembeni na kuwa ni miongoni mwa watazamaji. i.e. Ni kama vile wanasema "ngoja hapo sasa tuione jeuri yake"
Ikitokea jamaa amefariki; wale waliokuwa wanatazama ili "kuiona jeuri yake" wanafika msibani kinafiki ili wasionekane wamesusa.
Lakini wapo waliostushwa na msiba huo ila hawakupata taarifa za ugonjwa mapema na kwa wakati ili wasaidie kutetea Uhai wa Marehemu. Watu hao hutoa michango hiyo kwa lengo la kuipunguzia mzigo na kuiliwaza Familia ya marehemu ukizingatia kwamba msiba ni gharama. Hao huja kwa roho safi, upendo na huruma.
Lakini lipo kundi la ajabu Kundi No.3: hawa ni wale wakisikia kuna msiba wanajiuliza Nikienda msibani nitapata nini huko? Kama msiba ni kwa Familia inayojiweza; watahudhuria lakini lengo litakuwa ni chakula na vinywaji na hawachangii chochote kifedha ila labda ni katika kuchimba kaburi au kuteka maji. Wengine baadhi yao hufika wakati wa Ibada ya mazishi (kama ni Mkristo) na kama ni Muislamu hawa huhudhuria kusindikiza maiti eneo la makaburini.
 
Inahuzunisha ule upendo wa agape haupo tena
 
Kama Marehemu angeshuhudi idadi ya watu walio kuja msibani kwake kipindi anaumwa angepona bila dawa
 
Anyway tuliohai tukumbushane wapendwa hata huko misiban semeshaneni mpendane mkiwa hai
 
kuitana bar kutumia hata laki kadhaa simple ngoja uwe na shida loh
 
Maiti hawezi kujizika acha azikwe tu,kujitibu ni jukumu la familia yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…