Sisemi kwa wanaume kwani ni mara chache mwanamume husema "Naondoka" hasa katika tamaduni zetu. Lakini wapo wale wanaoishi katika nyumba ya mke, wanaweza kusema hivyo. Au wale ambao kwa kuwa hawataki mwanamke au watoto wao wataabike, wanaweza kusema "Naondoka" na wakaondoka.
Lakini hapa hasa kauli hiyo hutolewa na wanawake, na mwanamke haamki na kusema naondoka bila sababu yoyote. Kwa kawaida, huwa wamechoshwa na visa vya mume; wachache husema hivyo ikiwa wamepata wanayemhisi bora kuliko waliyenao. Kwa upande wangu kama mwanamume, kwanza nimejifunza kuheshimu NO/HAPANA ya mwanamke. Mwanamke akiniambia HAPANA, ninaheshimu neno lake.
Mwanamke ananiambia naondoka, ikiwa nimemkosea nitamwomba samahani kwa kosa langu na kuhakikisha ninajirekebisha, lakini katu sitomzuwia kuchukua maamuzi yake. Na ikiwa sioni kama nimemkosea, nitakachokahikisha ni kuwa hasau chochote chake ndani ili asije akajidai kurudi eti "nilisahau upawa wangu". Anaondoka na kuchuka mpaka sindano yake; kubwa nitakalohakikisha ni kumsindikiza mpaka pale nilipokwenda kumchukua. Ikiwa ni kwa wazazi/jamaa zake, nitahakikisha ninawakabidhi mikononi.