Mpenzi wa Uwoya achanwa visu

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

Msanii wa kike wa filamu za bongo ambaye pia aliwahi kuolewa na mcheza mpira kutoka Rwanda, mlimbwende Irene uwoya, amesema mpenzi wake wa sasa ana ngeu nyingi mwilini za kuchanwa visu.

Akipiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Irene amesema watu kama hao ndio anaowataka yeye kwani inaonyesha uanaume halisi, na sio mwanaume anakuwa laini kama mtoto wa kike.

"Sijasema napenda wanaume wenye sura mbaya nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume, mwanaume uwe na ngeu, mimi bwana wangu ana ngeu, kachanwa visu yani", alisikika Irene Uwoya akimfungukia Big Chawa.

Irene uwoya kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake tangu kuwe na habari za kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Msami, na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi kwenye mitandao.


Muungwana
 
Aisee inaonesha anapenda wanaume ngangari ngangari sio lainilaini
 
Kila mmoja anataste yake wasimshangae.
 
Hii dunia ina sarakasi nyingi sana. Hii nayo naona ni ngeni kabisa kwenye huu uwanja wa amani.

Vijana, jitieni ngeu (ngewo) ili mpate fursa hapo kwa Uwoya.
 
Kwa lugha nyepesi anapenda wale masela wa uswahilini kwenye mnanda
 
Ulivosema amechanwa nikajua ana hali mbaya,,, Kumbe
 
Basi sawa ikikiki hii kutakua hakuna namna vijana itabidi wakahangaike kutafuta ngeu kama wanavyohangaika na mavumbi ya kongo!
 
Dah! Alipokuwa mwali katumika sana na maHB Leo tena anawatunuku wagumu. Baada ya kuona Wauza sura si lolote si chochote, wagumu hapa wanaambulia makinikia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…