Mpenzi wako alikwambia au alifanya nini ukasema kimoyomoyo huyu hawezi kuwa mke/mume wangu

Mpenzi wako alikwambia au alifanya nini ukasema kimoyomoyo huyu hawezi kuwa mke/mume wangu

Habari za weekend!

Kuna baadhi ya maneno watu wetu wa karibu wakiongea huwa yanatuumiza sana, sometimes inapelekea kupoteza interest ya kujenga maisha na huyo mtu.

Kuna mwanamke flani nilikuwa naye kwenye mahusiano takribani miaka 2, kuna siku bhana akaniuliza "hivi baby hata nikiolewa na mtu mwingine si tutakuwa tunakutana kisirisiri tunafanya mambo yetu?"

Kwa harakaharaka nikamjibu nikamjibu "ndio", ila ile kitu haikukaa vizuri kichwani mwangu, nilimwona kama mtu mwenye roho ya usaliti, kama anaweza kumfanyia mume wake hivyo si anaweza hata kunifanyia mimi.

Siku nyingine huyohuyo mwanamke akanambia maneno haya "Mimi sijali kuhusu matatizo yako, wewe ni mwanaume, wewe ndio inabidi ujali kuhusu matatizo yangu", baada ya hapo nikiwa simchukulii serious kabisa, wala sikutegemea mahusiano yetu yafike stage za kuoana.

Mwingine bhana alikuwa akiniomba hela afanye biashara, kuna siku alinieleza vizuri kabisa kuhusu hio biashara nikaipenda, nikamuahidi ntampa hela aanze, ilikuwa ni 1.5M.

Hio hela nilimpa kama baada ya wiki moja hivi, siku zilizofata nikawa nafatilia maendeleo yake na amefikia wapi, akawa tu ananiambia anasubiri vibali na issue zingine, mimi ilifika kipindi nikapotezea, kuna siku sasa mama ake akanipigia, ndio akaniambia kila kitu, ile hela bhana aliitumia kununua nguo, viatu, vipodozi, kabati la nguo na vikorokoro vingine,

Halafu ukizingatia sio mtu ambaye alikuwa hana nguo au anavaa vibaya, lahasha, hii kitu ilinifanya nipoteze interest kabisa na huyu mwanamke, nikawa namuona sio wife material kabisa, nilivoongea nae akasema sijui mambo hayakukaa sawa sijui kuna hela alizulumiwa, sababu kibao alitoa, nilimshangaa sana, hadi leo nikikumbuka nabaki nacheka tu.
Huyo mama wa mwanamke wa pili alikua na roho ya kinabii.
 
Kuna mwanamke bhana ni mke wa mtu ila waliachana so akawa single maza. Nikaja kutana nae tukaanzq mahusiano nikawa nampa hela ndogo ndogo ef 30,50 zangu kazila nyingi tu. Kuna kipindi hadi nikampa 100k alipo nililia kuhusu shida yake flani. Ajabu ni kwamba nilipo Sogea karibu naye ambapo ndio ilikuwa mda mzuri ata wa kusuuza rungu kwa mara ya kwanza (wkt tunakutana nilikuwa mkoani) matukio yakaanza sasa.

Tukio la kwanza akaniambia J naomba tuachane naona siko sawa kuna mambo yananichanganya. Nikamuuliza mambo gani hayo na mbona gafla hivo majibu yakawa hayaeleweki ila akasimamia msimamo wake tu kuwa nimuache hayuko sawa kwa sasa na kwamba pindi akiwa sawa atanitafuta yeye mwenyewe 😂😂

Baada ya kuchunguza nikagundua kumbe amerudiana na mtu wake bhana dah niliumia sanaa... Sasa ikabidi nimchane ukweli kwa kumwandikia msg maana cm zangu alikuwa hapokei tena. Sasa baada ya kuisoma ile msg ndio akaanza kupokea cm zangu tena na hapo sasa ikabidi anichane live bila chenga kwamba kama niko tayari kushea na mtu wake basi fine ila kama sipo tayari nipite kushoto 😂😂 NB:- kumbuka hapo hata mzigo sijaonja ndugu msomaji na plan ilikuwa kumuweka ndani kabisa la haulaaa....

Itaendelea...
Wewe hauna akili pole sana
 
Sifa ya mwanaume kamili ni kuwa na kifua. Kwa matatizo yake na mwanamke wake pia. Ni sahihi wote kuwa na kifua ila it matters alot kwa mwanaume
Ujinga huu siku watu hawautaki. Wazee wetu walikua na vifua kwakua mama zetu waliwastahi sana na waliwapa heshima na walikua na maadili mnoo sio kama ngiri hiz za leo nguruwe pori kabisa
 
Mke wa ukweli ni bahati, kwa kweli huyu niliye naye Mungu anibariki tu nizeeke naye. Ni mpambanaji mno na very caring indeed, najikuta kwa raha zilizonazo juu yake namlipa mshahara kila mwezi kwa kuwa tu mke wangu na kumshukuru kuzaa watoto tulionao. Thank you Mungu, ni haya tu jamani na samahani kama nimewaudhi. Mwenzenu niko kwenye furaha ya hajabu na mke wangu.
Mtaachana tu.
Ni suala la muda kidogo
 
Ujinga huu siku watu hawautaki. Wazee wetu walikua na vifua kwakua mama zetu waliwastahi sana na waliwapa heshima na walikua na maadili mnoo sio kama ngiri hiz za leo nguruwe pori kabisa
🤣🤣🤣 Unaongea kwa hisia sana mkuu we jamaa si ulikuwa unasifia ndoa yako ina miaka 18 🤣🤣 vipi mbona vilio kila nyuzi humu
 
Back
Top Bottom