Mpenzi wako alikwambia au alifanya nini ukasema kimoyomoyo huyu hawezi kuwa mke/mume wangu

Nilikua kwenye kagari kangu mwenyewe ka kwanza, nimempakia tunaenda kuenjoy weekend, kwenye foleni pembeni ilikuja evoque nyeupe, akaiangalia kinoma alafu nikasikia anasema ".. hii ndio gari sasa..."

Alinichanganya sana nikajikuta nimepandwa na hasira nilimuangalia kinoma alafu sikumwambia chochote Ila moyoni nikasema wewe hutakuja kuwa mke wangu kamweee. Toka siku hiyo nikapunguza uhusiano nae nikampotezea
 
Hahaha oyaaaa ilo ni lijini man kimbiaa mwendo wa kasongoooo
Hapa nimeliacha nna week sasa sirudi nyuma man af lime hitim degree chuo cha uhasibu .... hapa litaanza kujileta karibu na kipindi cha graduation ila sitoweza enda

Af kipimbi hiki kinapenda kunengua ticktock ukikikataza hakiskii

It's enough man she is a pretty girl but not on my type natakiwa nimwache apate wa kufanana nae .....

Ana vimbwanga vingi sana ila vya Chin chin sio rahisi kuviona ila ukitulia ndio unaona upo na kenge mwenye madoa
 
Hilo kalai kama langu tu shenzi. Af ukili rekebisha sasa haliskii linakua bishi shenzi.
 
Kwamba akiolewa na mwingine...... Maana yake mlikuwa wengi!
 
Unaonekana Una very sharp mind hasa kwenye reasoning. Hongera Sana!
 
🤣🤣🤣
 
Mada nzuri lakini punguza kuweka neno ''bhana'' bila umuhimu wowote. Mimi nilikuwa na girl friend ambaye kila wakati ninapomtania kwa kumwambia ''mbona jana sikukuona, au ulikuwa na mwingine?'' Yeye alikuwa anajibu ''na hili joto lote la mchana la Dar jamani?'' Nikawa najisema kama hamna joto ina maana anaweza kufanya lolote.
 
Mimi mwanamke yeyote akisha niambia "mwanaume ndio unapaswa kuhudumia" Tuna achana on the spot.

Hiyo ni Red flag ya kwamba huyo ni parasite.

Akahudumiwe na babake.
Kuna ile mwanamke anakuja kwenye maisha yako kwa kufosi mwsho wa siku unaamua kukaa nae gheto anakuwa mke,unashangaa siku umepinda labda unajisemesha kwake unamwambia nina magumu hata sjui nitafanyaje lakin ajabu anakujibu kuwa " kwani ulilazimishwa kuoa,mwanaume pambana" sasa unawaza kuwa keshasahau kuwa alikuja kwenye maisha yako kwa kung'ang'ania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…