Mpenzi wako alikwambia au alifanya nini ukasema kimoyomoyo huyu hawezi kuwa mke/mume wangu

Mpenzi wako alikwambia au alifanya nini ukasema kimoyomoyo huyu hawezi kuwa mke/mume wangu

Niliamua kumtoa out huko sehemu za starehe tule tunywe na kulala hoteli kubwa .
Tukiwa pale akaingia bwana mmoja ana kakitambi ka kiasi hakijafika kwangu si demu anadai simpendi mwanamume mwenye tumbo tumbo Kama huyo baba .

Anaongea huo ujinga wake ilihali na Mimi namiliki tumbo kubwa kuliko hata huyo bwana ,Basi nikajua hapa sipendwi ,ikawa njia ya kukaacha ka sharifa
Hahahahahfa
 
Nilikua kwenye kagari kangu mwenyewe ka kwanza, nimempakia tunaenda kuenjoy weekend, kwenye foleni pembeni ilikuja evoque nyeupe, akaiangalia kinoma alafu nikasikia anasema ".. hii ndio gari sasa..."

Alinichanganya sana nikajikuta nimepandwa na hasira nilimuangalia kinoma alafu sikumwambia chochote Ila moyoni nikasema wewe hutakuja kuwa mke wangu kamweee. Toka siku hiyo nikapunguza uhusiano nae nikampotezea
Na wew ungemshusha pale pale au jeuza gari yako ifate hyo vogue kisha msimamishe JAmaaa mshushe demu wako mpandishe kwenye hyo vogue
 
1.Jion moja nilikuwa natembea na huyu dem tunaelekea gheto tukiwa tumekaribia kama mita 50 tu hv namuona anaingia kwenye vichaka anachuchumaa na kukojoa i was so dissapointed sikutegemea sista du kama yeye akojoe vichakan kirahisi rahis tu mahali pasipo na maji na hata tishu haikuwepo
2. Mwingine alikuja mji ninaoishi alikuwa na ishu zake binafsi so nikawa naishi nae kwa muda ule alokuwa mji ule , tatizo likawa kila muda anazungumzia jinsi maisha ya nyumban kwao yalivyo ya shida huku akionesha ni mtu anaetafuta sababu ya kuondoka home muda wowote ule , nikasema mi mwenyewe bado nina matatizo yangu kibao nibebe yako ya nini ?
3. Huyu alifanyiwa opereshen ya uzaz so kuna kipindi tukawa hatuwezi kuamshiana popo , siku ananitext ananiambia kama nimezidiwa sana atanipa nyuma ilihali hata sikumwambia kuwa nimezidiwa, nikaona hapa sipo ndo mambo zake itakuwa huyu
Kesi ya kwanza siyo shida mtu kukojoa vichakani kama ni usiku, mm nakunya kbsaa vzr tu
 
Ndio nilikuwa nimeshaivua tayari kwa mashambulizi, Ile ameona trako na ips akanambia hivo mbn nilivaa haraka haraka nikaondoka mm
Alimaanisha hata yeye akikuoa atafaidi. Wewe ulielewa nini?

Alafu ni kwa nini akuache uvue chupi mwenyewe? Alipaswa akuchezee mpaka ukose nguvu za kujivua umuombe akuvue.
 
"Mimi sijali kuhusu matatizo yako, wewe ni mwanaume, wewe ndio inabidi ujali kuhusu matatizo yangu",
Kauli kama hii Mimi ndio ilinikimbiza tofauti yeye hakuongea kama wako , wangu alikuwa anafanya kwa vitendo ,yeye hajali mm napitia nini anachotaka yeye awe na furaha na atimiziwe mahitaji yake bila kujali furaha yake itanicost kiasi gani .... Nikajisema moyoni sijaja dunian kukufurahisha wewe Mimi niumie nikaamua kufanya maamuzi magumu
 
Mke wa ukweli ni bahati, kwa kweli huyu niliye naye Mungu anibariki tu nizeeke naye. Ni mpambanaji mno na very caring indeed, najikuta kwa raha zilizonazo juu yake namlipa mshahara kila mwezi kwa kuwa tu mke wangu na kumshukuru kuzaa watoto tulionao. Thank you Mungu, ni haya tu jamani na samahani kama nimewaudhi. Mwenzenu niko kwenye furaha ya hajabu na mke wangu.
Hongera kwa kupata mke mkuu, sisi wenzako tulioa ila kuna kipindi inafika unaona kabisa mkeo anakulazimisha kuvunja ndoa.
 
Habari za weekend!

Kuna baadhi ya maneno watu wetu wa karibu wakiongea huwa yanatuumiza sana, sometimes inapelekea kupoteza interest ya kujenga maisha na huyo mtu.

Kuna mwanamke flani nilikuwa naye kwenye mahusiano takribani miaka 2, kuna siku bhana akaniuliza "hivi baby hata nikiolewa na mtu mwingine si tutakuwa tunakutana kisirisiri tunafanya mambo yetu?"

Kwa harakaharaka nikamjibu nikamjibu "ndio", ila ile kitu haikukaa vizuri kichwani mwangu, nilimwona kama mtu mwenye roho ya usaliti, kama anaweza kumfanyia mume wake hivyo si anaweza hata kunifanyia mimi.

Siku nyingine huyohuyo mwanamke akanambia maneno haya "Mimi sijali kuhusu matatizo yako, wewe ni mwanaume, wewe ndio inabidi ujali kuhusu matatizo yangu", baada ya hapo nikiwa simchukulii serious kabisa, wala sikutegemea mahusiano yetu yafike stage za kuoana.

Mwingine bhana alikuwa akiniomba hela afanye biashara, kuna siku alinieleza vizuri kabisa kuhusu hio biashara nikaipenda, nikamuahidi ntampa hela aanze, ilikuwa ni 1.5M.

Hio hela nilimpa kama baada ya wiki moja hivi, siku zilizofata nikawa nafatilia maendeleo yake na amefikia wapi, akawa tu ananiambia anasubiri vibali na issue zingine, mimi ilifika kipindi nikapotezea, kuna siku sasa mama ake akanipigia, ndio akaniambia kila kitu, ile hela bhana aliitumia kununua nguo, viatu, vipodozi, kabati la nguo na vikorokoro vingine,

Halafu ukizingatia sio mtu ambaye alikuwa hana nguo au anavaa vibaya, lahasha, hii kitu ilinifanya nipoteze interest kabisa na huyu mwanamke, nikawa namuona sio wife material kabisa, nilivoongea nae akasema sijui mambo hayakukaa sawa sijui kuna hela alizulumiwa, sababu kibao alitoa, nilimshangaa sana, hadi leo nikikumbuka nabaki nacheka tu.
Tukafungie Ndoa kanisani. Kanisa lenyewe sasa🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom