Mpenzi wako haogopi kuchepuka, anaogopa ukijua kuwa anachepuka

Mpenzi wako haogopi kuchepuka, anaogopa ukijua kuwa anachepuka

Mambo yote yanaanza na UPENDO.....

UPENDO ni kapu lililobeba mambo yote kwenye maisha ya wapenzi na unasimama kama dira yenye kuyaongoza maisha yao.....

Kitu kilichokosekana siku hizi ni UPENDO na kuchukuliwa mapenzi kama fursa ya kujiinua kiuchumi
 
Hii ni kweli kabisa. Wahudumu wa Guest house na lodge wanatunza siri za watu sana.
Nilivyokuja kugundua siishi maisha yangu sina woga tena na usiishi na mtu ndani ukamchukulia kakamilika watu wanakula mibondo vibaya hasa waajiriwa acha kabisa.
 
Hiyo ni asili ya Wanyama wote tukiwemo na sisi watu.
Ebu acheni kupingana na nature mnafanya maisha yaonekane magumu.
Kula/liwa pale unataka kwa muda ulonao kama una uwezo.
 
Mahusiano ya siku hizi yamekuwa kama vita vya mashambulizi ya kushtukiza. Hofu kubwa kwa watu wengi haipo tena kwenye kuchepuka, bali ipo kwenye kujulikana kwamba unachepuka.

Mtu anaweza kuwa na mahusiano ya pembeni kwa muda mrefu bila kuona tatizo, mradi tu usije ukagundua. Kwa lugha nyingine, tatizo si kile anachokifanya, tatizo ni wewe kujua kile anachokifanya.

Na ukifikiria kwa undani, utaona kwamba siku hizi watu wengi wamekuwa very strategic kwenye mahusiano. Wanajua namna ya kufuta message, kubadilisha majina kwenye simu, kutengeneza sababu za kutokuwepo na hata kupanga muda wa kukutana bila kuacha ushahidi.

Kwa hiyo kama mtu anaweza kuwa "smart" kiasi cha kuhakikisha mazingira hayamruhusu mwenza wake kugundua, anaona kama ana amani kabisa.

Na hili si suala la wanawake pekee wala wanaume pekee.

Siku hizi kila mmoja anataka kuwa na mchezaji wa akiba. Hakuna mtu anataka kuanza msimu akiwa hana usajili wa kutosha.

Ukimwona mpenzi wako anaanza kuona kwamba kwenye kikosi chako kuna majeruhi wengi, anaanza kutafuta mbadala mapema. 😂

Leo hii unaweza kuwa kwenye relationship nzuri kabisa, lakini nyuma ya pazia mwenzako tayari ana mtu anayemuweka "standby", just in case mambo yakiharibika.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba hali hii imeanza hata kuingia kwenye ndoa.

Taasisi ya ndoa kwa sasa inapitia kipindi kigumu sana. Watu wengi wanaingia kwenye ndoa kwa sababu ya kutimiza taratibu za dini, mila, familia au jamii, lakini ndani yao dhamira ya kweli ya kujenga maisha na mtu mmoja haipo kwa kiwango kilekile.

Ndio maana unaweza kukutana na mtu ana miaka 10 kwenye ndoa, lakini bado ana mahusiano ya pembeni kama vile hajawahi kuoa.

Na wakati mwingine kinachowafanya watu waendelee kuwa pamoja si uaminifu tena, bali ni kutokujua ukweli.

Mume akiamini mke wake ni mwaminifu, anaendelea na maisha.

Mke naye akiamini mume wake ni mwaminifu, anaendelea na maisha.

Lakini ukweli ukiwekwa mezani, ndipo kila kitu kinabadilika.
Aiseeeeeee sawa kiongozi
 
Back
Top Bottom