Mpenzi wangu amenipiga mkwara wa kuangalia au kushika simu yake

Mpenzi wangu amenipiga mkwara wa kuangalia au kushika simu yake

Marahaba

Member
Joined
Nov 23, 2010
Posts
33
Reaction score
1
Jamani wadau hii imekaaje katika mahusiano?Eti ukiwa na mpenzi wako(she) halafu kwa hali isiyo ya kawaida ikatokea maporomoko ya hapa na pale ,then yeye akaanza kukupiga mkwara usiiguse simu yake na akiwa home muda wote ameishikilia mkononi(yaani akiwa anapika,akiwa sebuleni ,mkiwa chumbani muda wa kulala na hata akienda chooni), halafu kingine mkiwa naye kwenye gari labda yenu ya private ikitokea ameiweka mahali basi itafunikwa na leso au hata kuweka pochi juu yake,Je kwa hili ni hatua gani bora za kufuata au kuchukua?????

Sasa wewe simu yake ya nini? Unaitafuta presha kwa garama nafuu hivyo?

Oya Dogo,huyo sio,timua mbio fasta!

Mimi mwanaume akinitongoza interview ya kwanza huwa namuambia anipe simu yake nikae nayo siku mbili.hizo mbio utadhani wako olympic unadanganyika

Nimeipenda mbinu yako,ngoja malaika akishuka akaibadili akili yangu,nikimpata mdada nitamwambia tubadilishane simu wiki nzima!!!!

wewe nawe si una yako??
mie nitataka kupekua nikiwa suspicious tu kuwa mambo hayaendi inavyotakiwa.....
km kila jambo kati yenu lipo kny mstari sasa simu yake wewe ya nini?........
anyway nahisi labda ana mwingine anajaribu kucover up matendo yake...mpe ultimatum ni wewe au simu baaasi

nimeipenda mbinu yako,ngoja malaika akishuka akaibadili akili yangu,nikimpata mdada nitamwambia tubadilishane simu wiki nzima!!!!
eeeeeeeh na kubipu kutaisha

Kweli e! hapa ni kutimua,maana kumbuka ya kwangu huwa anaishika tu akitaka kumpigia mama yake au dada zake ,lakini ya kwake mmm!hapa mmenifungua macho maana nitakufa kwa presha bure kwa kweli

Kwa maoni yangu hiyo ni dalili mbaya! Kuna mawasiliano ambayo ni threat kwenye rlnship yenu hataki uyatambue.

hapo sepaa haupo kwenye 1st eleven yake ila we ni SUB. wewe ni part of the list!

mbona jibu tayari liko wazi,au unaukataa ukweli?huyo dada ana mtu,anajaribu kuwapima na mmojawapo ni spare tyre wake,kwa nini awe na wasiwasi kwenye simu yake kiasi hicho?

Mimi mwanaume akinitongoza interview ya kwanza huwa namuambia anipe simu yake nikae nayo siku mbili.hizo mbio utadhani wako olympic unadanganyika

kadri unavyombana bana mwanaume na yeye anazidi kukutaftia mbinu za uongo. Peaneni uhuru.

Mambo mengine sio ya kuomba ushauli kabisa,unashindwa kuongeza na kutoa?hapo ujue kuna mkamuaji tena anakamua kisawa sawa.

piga chini, tafuta ustaraabu mwingine. hapo utaingia choo cha kike ushindwe pa kutokea

Kwa cc 2liosoma hesabu za 4m 2,2naweza 2kaiita hyo kama SUBSTUTION METHOD..so toka nduki mkuu.

Naamini kuwa kwenye mahusiano kuna 'vitu vyetu' na 'vitu vyangu', and the two are immiscible.

Ukielewa hili, mambo rahisi tu.

kwa habari ya simu mie namuunga mkono huyo dada, wewe una simu yako yakwake ya nini tena, tena mkianza biashahara za kukaguana kwenye simu zenu huo uhusiano ndio umefika mwisho, peaneni uhuru! hata mie sipendi na sitaki tabia ya kupekua/kupekuliwa kwenye simu

mi nna mke muda mrefu tu, kabla simu hazijatapakaa. Sijawai kupokea sim yake wala kusoma sms. Yangu anaitumia lakini. Sipati presha wala nini. Kama kuna tatizo mjadiliane mtatue, sio kutafuta mchawi kwenye simu

Back
Top Bottom