Niaje wazeiyaaah...
Mko Bwaxx...
EBANA SAWA:
Kawaida yangu ku expose maisha yangu nipate kushauriwa bana.. Maana unaweza kujifanya much know (kama asemavyo King Crazy GK kwenye wimbo wa Piga Manati Piga ya kichwa) mambo yakienda kombo unaambiwa "uwe Unauliza, fala wewe"
SASA ISSUE NI HIVI :
I am 26 (bila shaka mnajua jinsia yangu ni ME) na girlfriend wangu (yule niliwaambia hapendi kabisa kunipiga mizinga....kuna cku nilimpiga mashine dakika 47 nonstop na mengine mengi ambayo nilishaweka hapa jukwaani) she is 26.5
Key problem here ni age difference kati yetu. Amenizidi miez mitatu kuzaliwa. Nahitaji awe mchumba later on mke wa ndoa halali....
Nasomaga na watu pia wanasemaga kuwa mwanaume inatakiwa umzidi mkeo miaka kuanzia miwili upwards..
Swali kwa wanaume waliooa wake almost same age JE changamoto zipi mmekutana nazo..
Hii imekaaje mazee mchumba wangu kanizidi Miezi mitatu???? Is there any problem...
#Chief Eng
Heshima Mkuu,Chief Eng!!
Kwanza hongera sana kwa kuwa na Mpenzi mwenye sifa ulizozitaja.Nb;Siyo wote wana wapenzi wenye sifa kama hiyo hapo juu.Msalimu sana.
Niende kwenye Mada moja kwa moja,Suala hapa la kuzingatia,Ni wapi ulipotoka,Ulipo na utakapokwenda.Usifikirie ulipo tu na kusahau ulipotoka na utakapokuwa.
Wengi wameshauri mambo ya msingi hapo juu ila mtizamo wangu ni tofauti kidogo,Kwa asili ya wanawake wengi walivyo inakubidi uwazidi vyote kuanzia Umri,Uwezo wa kufikiri,Elimu,na hata kiuchumi.Ukioa mwanmke mlio sawa kiumri nadhani hujangamua utakapokuwa kwa baadae (Uzeeni) kwakuwa utafika wakati wewe ukionekana kijana wakati yeye akionekana kashezeeka,Waliosema ni vizuri labda niseme tu kuwa hawajafikiri upande wa pili wa picha.
Umri-Katika ukuaji wanawake wanakuwa mapema mno kutuzidi sisi wanaume na kuzeeka mapema,Ni kinyume cha wanaume.Sisi hatukui mapema kama wao na hata kuzeeka hatuzeeki mapema vilevile.
Hoja yangu ni hivi,Ukioa mwanamke mlio sawa kiumri utafika wakati ataonekana ndiye mkubwa kuliko wewe tofauti na kama ungemuoa uliyemzidi umri walau miaka mitano na kuendelea.Hapa ni ku-look beyond the present,Usifike wakati ukamchoka mkeo kisa anaonekana mkubwa zaidi yako.
Nb;Kati ya makosa makubwa utakayoyafanya katika maisha yako ni pamoja na kukosea kuoa.
Uwezo wa kufikiri-Hapa naomba tuelewane kidogo kuwa ninapozungumzia uwezo wa kufikiri nina maana kuwa uwezo wa kungamua mambo mbalimbali,Kutatua matatizo kwa uweledi mkubwa nk.Mara nyingi wanawake wanaokuwa na uwezo huu hawadumu katika ndoa na wenza wao kwakuwa hakuna mwanaume popote anayekuwa na amani pale mkewe anapokuwa na uwanda mpana wa mambo,Die or Live but that is the reality.
Elimu-Ni vigumu sana kwa Mwanamume aliyeishia STD 7 kumuoa mwanamke mwenye Phd ila ni Rahisi zaidi kwa Mwanamume mwenye Phd kumuoa mwanamke wa STD 7.Hii haina tofauti kuubwa sana kimaelezo kama nilivyoelezea hapo mwanzo katika Uwezo wa kufikiri.Ni mara nyingi sana kwa mwanaume mwenye elimu kubwa kuishi na amani pamoja na furaha katika ndoa ambayo mkewe hana Elimu kubwa ila ni kasheshe sana pale Mwanamke anapokuwa na Elimu kubwa kumzidi mumewe,Hili kila mtu ni shuhuda.
Nb;Kadiri mwanamke anavyosoma ndivyo anavyozidi kupunguza idadi ya watu wa kumuoa.Kadiri Mwanaume anavyozidi kusoma ndivyo anavyozidi kuongeza idadi ya watu wa kuwaoa.
Uwezo wa kifedha-Ukioa mwanamke mwenye Kampuni 5 nchi za Nje wakati wewe mwanaume ni Fukara kama mimi basi jiandae kuwa Shamba boi katika nyumba ya mkeo.Mwanamke mwenye uchumi mkubwa kifedha huwa anayasahau majukumu yake kama mwanamke kwa mumewe na hii hupelekea ndoa kunasa katika tundu bovu jambo ambalo siyo zuri.Ni vyema mwanaume uoe mtu ambaye hajakuzidi kifedha,inakaa poa zaidi kuliko uzidiwe.
Yapo mengi unayoyafahamu na ume-experience katika miaka mingi uliyoishi humu Duniani.Kiimani wanawake wamechorwa kama wasaidizi,Sasa kama wewe ni Mtemi wa mtaa mpe Msaidizi wako akae katika nafasi yako na wewe uikaimu nafasi yake halafu matokeo utayaona.
Nb;Ieleweke kuwa zipo Ndoa ambazo zimefaulu kuishi kwa Amani na Furaha,huku zikikinzana na sababu zangu nilizoziorodhesha hapo juu.Fikara zangu hazina maana kuwa Usioe mwanamke ambaye kakuzidi Umri,Elimu,Uwezo wa kufikiri,Uwezo wa kifedha nk kwakuwa
SERIKALI YA MTU NI KICHWA CHAKE MWENYEWE.