Hebu tuambie ulishawahi kusikia kwa mtu yeyote yule anakuzungumziaje anapokuwa na watu wengine? anakuelezea kama mtu wa future yake au napo huuchuna tu. Ama ana uwezo mkubwa wa kutambua kuliko wewe..kwamba inawezekana unaigiza ili apate wivu kumbe yeye anakuchora tu unavyopiga drama!
Fumbo lipo kwenye moyo wake, wakati mwingine mioyo ya watu wengine huwa migumu kuruhusu hisia za wivu kutoka nje.Au anakuamini kupita kiasi hivyo hana mashaka yeyote ingawa na hili gumu kutokea kwa wasichana wengi.
Nakupa tip,hebu jaribu kumchunia kumpigia simu ili utengeneze ka-distance fulani (akikupigia simu unamjibu dry kiasi) halafu uone reaction yake halafu rudi jamvini kutujuza, me nilishawahi kufanikiwa kwa hilo. Mapenzi yanahitaji vitimbi kidogo ili yanoge, Ila ukiona nae anauchuna - wafwaaaaaaaaaaaaaaaaaa.