Mpenzi wangu anajikojolea kitandani nifanyaje?

Du
 
Mwambie asinywe vimiminika kiasi kingi baada ya saa 10 jioni. Kama bado, basi asinywe kiminika chochote baada ya saa 10 jioni. Afanye hivyo na kufurahia usingizi mnono.

Kumbuka, sijasema asile chakula.
 

Habari!

Ili kupata usaidizi wa hali hii, ni mambo mengi yanatakiwa kufatiliwa juu ya mhusika.

Tatizo hili laweza kuwa la kimaumbile, kurithi, kisaikolojia, kimfumo au tabia.

Hivyo kuna mambo mengi yatahitajika:

1: Kama alishawahi kuweza kuzuia mkojo hapo kabla/kulala bila kukojoa kitandani au tangu azaliwe anakohoa kitandani.

2: Hali hii kama inatokea na mchana au usiku tu.

3: Historia yoyote ya kutendwa kimaumbile au kisaikolojia.

4: Kama alishawahi kupata ajali yoyote.

5: Historia ya wazazi pamoja na nduguze kuhusiana na shida husika.

6: Kujifunza juu ya uwezo wake wa kupata usingizi na kuzinduka.

7: Kuelewa ukubwa/size ya kibofu chake cha mkojo kulingana na umri.

8: Mwenendo wa upataji wake wa haja kubwa.

9: Kuondoa wasiwasi wa vitu/magonjwa mengine kama: Sukari vs UTI vs ADH(utoaji vs ufanyaji kazi).

10: Matumizi mengine ya dawa ambazo huweza kuleta athari chanya kwenye utoaji mkojo.

11: Matumizi ya vinywaji ambavyo huweza kuwa na athari chanya kwenye utoaji mkojo.

12: Kufahamu BMI ya mgonjwa kama inaendana na urefu wake.

NB: Hivyo, suala hili ni mtambuka linahitaji kuhusisha nyanja tofauti za wataalamu wa afya. La sivyo, itakuwa ni kubahatisha ambayo huweza kuleta hali ya kuona unashindwa kupata suluhisho.

Suluhisho litaambaatana na kusahihisha linalopatikana au yanayopatikana kama chanzo husika.
 
Fistula hiyo ndugu yangu, inatibika kabisa nenda hospitali, mirija au njia ya mkojo zimeshalegea
Fistula no tofauti na hilo . Kwani Fistula anatokwa haja ndogo hata mchana lakin huyo ni kikojozi usiku kitandani.
Nakuomba ndugu ukuje pm tafadhali Dada atapona hakika
 
Jesus, 😱
Barua yote nasoma mimi
Mwambie asinywe vimiminika kiasi kingi baada ya saa 10 jioni. Kama bado, basi asinywe kiminika chochote baada ya saa 10 jioni. Afanye hivyo na kufurahia usingizi mnono.

Kumbuka, sijasema asile chakula.
Sauwa
 
Fistula no tofauti na hilo . Kwani Fistula anatokwa haja ndogo hata mchana lakin huyo ni kikojozi usiku kitandani.
Nakuomba ndugu ukuje pm tafadhali Dada atapona hakika
Mmmh
 
Acha utoto

Itakuwa hujaishi ushagoo wewe...

Sisi wa miaka hiyo enzi za mwalimu, mtoto akizidisha ukojozi alikuwa anafungwa chura kiunoni, anakimbizwa mtaani huku akisindikizwa na nyimbo za kebehi kama huu, "kindumbwe ndumbwe chalia, kindumbwe ndumbwe chalia, kikojozi na nguo kaitia moto na ndani kuna viroboto, hilooo". Hapo mtoto kabebeshwa jamvi, nguo, mashuka au godoro alilolikojolea...
 
aisee!
 
du
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…