MPENZI WANGU BAADA YA KUPONA MATATIZO YA AKILI SIMUELEWI

Nashukuru sana mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasaikolojia wabobezi katika tabia na hulka za bin adam wanadhana ijulikanayo kwa lugha ya umombo kama "moody disorders" (sina hakika kama ndio moody swing).
Hii ni hali ya kubadilika badilika kwa moody ya binadamu husika ndani ya muda mfupi sana. Mfano ndani ya dakika ana furaha saana, dakika chache zijazo ana huzuni kuu, mara aanze kucheka mara kulia na vitu vya aina hiyo. Kutegemea na uzito au (magnitude) ya tatizo kwa muhusika madhara ya hali hii pia hutofautiana kati ya muathirika mmoja na mwingine.
Aidha wanazuoni wabobezi wa tabia wamedadavua vyanzo anuai kwa makumi vya tatizo hilo, na mojawapo ya chanzo kikubwa ni matatizo ya akili katika uzania wowote ule.
Mpenzi wako ana uwezekano mkubwa wa kuwa na tatizo hilo, kwa vile wewe si mtaalamu wa afya ya akili ya mwanadamu yapo mambo kadha wa kadha unayoweza kufanya wakati akiendelea na matibabu ya kutaalamu.
Moja, muonyeshe upendo wote kama yupo kawaida, usionyeshe kushangazwa na mabadiliko yake ya mood ya mara kwa mara, msupport sana kama ana dalili za kuwa na tatizo la kumbukumbu kwa kumkumbusha vitu muhimu kwa upendo na upole, usimkaripie wala kumtolea lugha ya ukali hii huzidisha tatizo jingine liitwalo sonono au (depression) kwa lugha ya umombo.
Na yote katika yote kuwa karibu nae mara kwa mara kwani matatizo ya akili huathiri kwa asilimia kubwa sana uwezo wa mwanadamu katika kufanya maamuzi sahihi.
Mungu wetu aliye muweza wa kila kitu amjaalie katika kipindi hiki yabisi kwake na kwako na akutie nguvu na ujasiri wote unaohitajika kulibeba hilo.
 
Yeah hapo kuna data concussion boss kazi.
 
Ba mkwe acha tu mm nikupe pole tu tena pole sana Mungu azidi kukupa tu moyo huohuo wa kumvumilia mpenzi wako ndio mapenzi hayo unampenda mtu kwa kila kitu chake
 
Kama humuelewi bado hajapona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…