Mpenzi wangu hana wivu na mimi wala hayuko 'romantic' nifanyaje?

Mpenzi wangu hana wivu na mimi wala hayuko 'romantic' nifanyaje?

Drake- Doing it wrong We live in a generation of, not being in love, and not being together
But we sure make it feel like we're together
'Cause we're scared to see each other with somebody else
So cry if you need to, but I can't stay to watch you
That's the wrong thing to do
Touch if you need to, but I can't stay to hold you
That's the wrong thing to do, oh (oh)
Talk if you need to, but I can't stay to hear you
That's the wrong thing to do
'Cause you'll say you love me, and I'll end up lying
And say I love you too
But I need someone different
You know it, oh-ho, you know it
Oh-ho, you know it, we both know it
I need someone different
You know it, oh-ho, you know it
Oh-ho, you know it, we both know it
Something's been missing
You know it, oh-ho, she knows it
Oh-ho, I know it, we all know it
I need someone different (oh-ho, oh-ho)
 
Hasomi, yupo home since 2018, huo uchakarikaji veepe[emoji848][emoji848]
 
Hata mm niko hvyo kwa mtu nisiempenda.. yaan hvyo hvyoo.. ila nakua nae tuu mtu huyo kwasabab fulan.. ila kumpenda .. noo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji28][emoji28]
 
Jamani kama nilivyotangulia kusema hapo juu kwenye heading, naombeni Ushauri wenu kwenye Hili. Iko hivi nina mpenzi wangu ambaye tuna mda wa miezi 6+ kwenye mahusiano, japo tumekua karibu tangu 2020, ila mahusiano rasmi ni hiyo miezi 6.

Huyu mpenzi wangu nilipanga kumuoa mwishoni mwa mwaka huu au mwakani mwanzoni. Ila amekua akinichanganya kwenye baadhi ya mambo kama ifutavyo.
1. Amekua ni mtu wa kutoa sababu nyingi sana hasa pale ninapohitaji kuonana naye. NB hatukai pamoja ila ni karibu, kwa maana umbali wake ni mwendo wa masaa machache tu.

2. Kwa mda wote huu hajawahi kuniambia ananipenda. Nikimhoji, anasema mtu anaweza kukuambia hizo romantic words na bado asikupende. HIVYO yeye husema ananipenda hata kama haniambii.

3.Mawasiliano. hana ile akutafute asubuhi mchana na jioni. Bali mnaweza kuongea hata saa 11 jioni, hiyo ndiyo imetoka, usiku hataki mzungumze tena au kutakiana usiku kwema. Kwake mkiongea mara moja tu kwa siku inatosha. Kiufupi hapendi sana mawasiliano ya KILA mara.

4. Hayuko romantic sana. Neno pekee analolijua ni "mpenzi" hajawahi niita kwa neno nje zaidi ya hilo. Hata tu mpenzi wangu, mchumba wangu, or even mume wangu sijawahi sikia masikioni mwangu. Simply hana kabisa yale mambo ya kihindi

5. Haonyeshi wivu wowote wala hofu au wasiwasi juu yangu, siyo mdadisi juu ya maisha yangu kabisa

6. Usipomtafta, lazima atakutafta sana tu ila shida zake ndio hizo hapo 1-5

. UBORA WAKE. 1. Mchapa kazi, mcheshi, charming and disciplined na mkarimu
2.Anavaa vizuri/Anajua kujistiri, hababaiki, etc.
3. Siyo mlalamishi au mtu wa kupenda kesi kesi
4. Ni mwepesi sana kusamehe na kupotezea vitu, hata kama utamkosea
5. Ni mchakarikaji siyo mtu wa kubweteka.

She is 22 hasomi, yupo home since 2018 after completing form 4, I am 27, nampenda sana, ila yeye sielewi kama ananipenda kweli kulingana na sababu hapo juu.

Wazoefu naombeni mnisaidie niendelee naye au nishike hamsini zangu . Kulingana na hayo niloyaeleza hapo juu. Wakuu nipo njia panda karibuni kwa mchango wenu wadau situation kama hiyo hapo juu innakua na maana gani?
Hongera mimi naona hapo umeramba dume strengths zake ni nyingi kuliko weaknesses.Hayo mambo ya kutokuita baby ni minor anaonesha kuwa na upendo wa dhati na wa kutoka moyoni.Huo uchapakazi wake nimeupenda na mtu asiye na makuu mkuu vuta huyo binti faster ukizubaa utajikuta wenzako wameshaweka sera za kuvuta ndani.
 
watu watarukaruka hapa na coments zao lkn ukweli halisi ndo huo

wife material wengi hawanaga mbwembwe

aanze kukutafta asbh, mchan na jioni ili iweje?

kutwa akuimbie nakupenda ili iweje??

upendo unakaa moyoni na siyo mdomoni..

hakufatilii uko wapi , unafanya nini kwa kuwa anakuamini.
we kama umempenda muoe, hayo mengine yatajiset yenyewe
Braza nashukuru umenena kwa niaba yangu😃😃mpka sahiv nlkuwa najiuliza haya yote ya nini

Hala me mwanamke kunifanyia hayo yote namuona tapeli tu
 
Hongera mimi naona hapo umeramba dume strengths zake ni nyingi kuliko weaknesses.Hayo mambo ya kutokuita baby ni minor anaonesha kuwa na upendo wa dhati na wa kutoka moyoni.Huo uchapakazi wake nimeupenda na mtu asiye na makuu mkuu vuta huyo binti faster ukizubaa utajikuta wenzako wameshaweka sera za kuvuta ndani.
Endeleeni na ulofa wenu, mwanamke huwa hafichi hisia zake za mapenzi kwa mtu ampendaye.
 
Kuna uwezekano mkubwa huyo anaishi mume wake nyumbani, yupo njiapanda , ukimuoa kweli atamkimbia mumewe [emoji23]
 
Ningekua wewe ningemuoa faster,ana sifa zote za wife material.
 
we kama umempenda muoe, hayo mengine yatajiset yenyewe

Mwanzo umeshauri vizuri sana ila hapa mwisho umeharibu...
Kauli ya kinyonge sana hii,,, na ndio Kaburi la watu wengi huanzia kuchimbwa hapo
 
Mwanamke ni ngumu sana kuficha hisia zake kama anakupenda,,, Yaani utajua tu kuwa unapendwa,,hata ajifiche vipi utafahamu... Wanawake wa humu wote ni mashahidi kwenye hili,, kama kuna binti anabisha aje anipe mkono...

Mkuu kuna namna hupendwi,, au huenda ndio mapenzi yanaanza so Jipe muda....BUT make sure una Exit plan ili usirudi kulia lia humu baadae..

Grow up Men,,, Hizo Fairy tales za kwenye movies huku kwa Ground huwa haziwi applicable...

Note: Acha kujipendekeza sana kwake as if huna options,, sometimes Masela mnaopendaga sana mademu huwa mna behave namna flani hivi kiwaki sana hadi mademu wanawaona kero,, achana na hilo kama upo hvyo,, usimuoneshe kwamba yeye ndio speeeesho... hii itasaidia kujua kitu fulani hivi..

Asante
 
Back
Top Bottom