jifunze kumuacha ukiweza muache.hilo penzi litakutesaKuna kitu kinaniumiza sana kwenye mahusiano yangu, lakini sijui kama mimi ndiye ninayefikiria sana au kweli kuna tatizo.
Mpenzi wangu siku hizi hanipi muda kabisa. Nikimpigia simu mara nyingi anasema yupo busy. Nikimtumia ujumbe anaweza kunijibu baada ya muda mrefu sana, wakati mwingine hata siku nzima inapita bila kuongea naye vizuri.
Kinachonichanganya zaidi ni kwamba nikifungua WhatsApp namkuta online. Anaonekana kupost status, kuangalia status za watu na wakati mwingine anaonekana kwenye mitandao kwa muda mrefu.
Nikijiuliza, kama ana muda wa kuwa online, kwa nini hana hata dakika chache za kuongea na mimi?
Nimejaribu kumuuliza kama kuna tatizo au kama amechoka na mimi, lakini ananiambia sina sababu ya kuwa na mashaka na kwamba ana mambo mengi ya kufanya.
Lakini ukweli ni kwamba nimeanza kujisikia kama sina umuhimu tena kwake.
Kitu kinachoniumiza zaidi ni kwamba zamani alikuwa mtu wa kunitafuta. Angeuliza nimeamkaje, nimefika salama au siku yangu imekwendaje. Sasa mimi ndiye ninayelazimika kuanzisha mazungumzo karibu kila mara.
Sijui kama mapenzi yamepungua au labda nimekuwa nikimlazimisha mtu ambaye tayari ameshaanza kuniacha moyoni.
Nimefika mahali najiuliza kama niache kumtafuta kabisa nione kama atanisikia au atanitafuta mwenyewe.
Kama ungekuwa kwenye nafasi yangu, ungefanya nini? Ungeendelea kumtafuta, ungekaa kimya mpaka yeye akufuate, au ungeamua kuachana?
View attachment 3654176
Mahi ❤️Nakupendaa
😍 U're the Queen of my lifeMahi ❤️
My King💃🏽😻😍 U're the Queen of my life
Nakupigia simu tuongee mamiiMy King💃🏽😻
AiseeKuna kitu kinaniumiza sana kwenye mahusiano yangu, lakini sijui kama mimi ndiye ninayefikiria sana au kweli kuna tatizo.
Mpenzi wangu siku hizi hanipi muda kabisa. Nikimpigia simu mara nyingi anasema yupo busy. Nikimtumia ujumbe anaweza kunijibu baada ya muda mrefu sana, wakati mwingine hata siku nzima inapita bila kuongea naye vizuri.
Kinachonichanganya zaidi ni kwamba nikifungua WhatsApp namkuta online. Anaonekana kupost status, kuangalia status za watu na wakati mwingine anaonekana kwenye mitandao kwa muda mrefu.
Nikijiuliza, kama ana muda wa kuwa online, kwa nini hana hata dakika chache za kuongea na mimi?
Nimejaribu kumuuliza kama kuna tatizo au kama amechoka na mimi, lakini ananiambia sina sababu ya kuwa na mashaka na kwamba ana mambo mengi ya kufanya.
Lakini ukweli ni kwamba nimeanza kujisikia kama sina umuhimu tena kwake.
Kitu kinachoniumiza zaidi ni kwamba zamani alikuwa mtu wa kunitafuta. Angeuliza nimeamkaje, nimefika salama au siku yangu imekwendaje. Sasa mimi ndiye ninayelazimika kuanzisha mazungumzo karibu kila mara.
Sijui kama mapenzi yamepungua au labda nimekuwa nikimlazimisha mtu ambaye tayari ameshaanza kuniacha moyoni.
Nimefika mahali najiuliza kama niache kumtafuta kabisa nione kama atanisikia au atanitafuta mwenyewe.
Kama ungekuwa kwenye nafasi yangu, ungefanya nini? Ungeendelea kumtafuta, ungekaa kimya mpaka yeye akufuate, au ungeamua kuachana?
View attachment 3654176
Naunga mkono hoja.Tafuta kazi ya kukuweka busy! mtu asiwe online kidogo ushatuma msg ushapiga video call.
Muda mwingine mtu yupo online anawasiliana na wateja.
Kabisaa🥰Nakupigia simu tuongee mamii
Kwahiyo mleta mada wakati anaomba msaada kuhusu mpenzi wake kutompa muda, nyie ndo mkapata muda wa kupenzika hapo hapo 😆, hii dunia kweli haipo fairNakupigia simu tuongee mamii
Mtoto anataka muda tu na mapenzi basiKwahiyo mleta mada wakati anaomba msaada kuhusu mpenzi wake kutompa muda, nyie ndo mkapata muda wa kupenzika hapo hapo 😆, hii dunia kweli haipo fair