Mpenzi wangu haoneshi kumpenda Mtoto wangu

Mpenzi wangu haoneshi kumpenda Mtoto wangu

La mwisho mkumbushe Huyo mwanamke wako kuwa akipenda boga apende na ua lake, huyo binit ni damu yako hivyo anapaswa kumpenda kwasababu ametokana na wewe kama anavyokupenda.
Na hili ni muhimu sana. Aweke msimamo mapema ili huyo mwanamke aamue kusuka au kuonyoa. Na ashukuru Mungu ameiona hio tabia mapema.
 
Nimebahatika kuwa na mtoto na mwanamke niliyekua naye awali lakini hatukuweza kuendelea na mahusiano yale. Mtoto anasoma madarasa ya chini na nmemchukua kukaa naye na kwa sasa nina mwanamke tuna mwaka mmoja pamoja na ambaye tuna matarajio ya kusogea hatua za mbali ikiwemo kufunga ndoa.

Changamoto ninayoipata kwa sasa ni kwamba mpenzi wangu anaonekana kutompenda mtoto, na vitu vingi anafanya kuniridhisha mimi. Anavyoongea naye, anavyomtuma, vitu anavyomwambia afanye ilhali mtoto ana miaka 8 tu vinaniacha njia panda kwamba huyu ni mwanamke sahihi ambaye atamlea mtoto huyu ili apate makuzi mazuri na asi feel ananyanyaswa.

Nahitaji kufanya maamuzi mapema na ikibidi hata kusitisha mahusiano na mwanamke huyu ili mtoto asipate shida mbeleni. Naombeni ushauri kwa wadau mliopitia situation kama hii au kwa mtu mwenye insights/ushauri.

Rudi kwa mama mtoto wako mtunze mtoto wenu
 
Back
Top Bottom