Mpenzi wangu ni mjamzito amekutwa ana Ectopic Pregnancy

Kwa sababu ndio mimba ya kwanza huwezi kuamini kila utakacho kiskia..
Nenda hospital nyingine usiseme kama mmeshapiga ultrasound, alafu fananisha majibu,nenda tena hospital nyingine kama majibu ni yale yale fata ushauri wa daktari kwa amani na roho nyeupe kama kweli unampenda mkeo..lasivyo utakosa vyote
 
Nashukuru kiongozi nitaufanyia kazi ushauri wako
Kwa sababu ndio mimba ya kwanza huwezi kuamini kila utakacho kiskia..
Nenda hospital nyingine usiseme kama mmeshapiga ultrasound, alafu fananisha majibu,nenda tena hospital nyingine kama majibu ni yale yale fata ushauri wa daktari kwa amani na roho nyeupe kama kweli unampenda mkeo..lasivyo utakosa vyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatujaenda hospitali nyingine ila tunampango wa kwenda Sinza Palestina pale juma tatu akafanye tena Ultrasound ili tushabihishe majibu ya hospitali hizo mbili.. maumivu aliyokuwa anayapata ni ya kawaida tu kama mama mjamzito mwingine yeyote anayapata na sio ya kukaa muda mrefu ni maumivu ya siku mbili tatu hadi nne yanakuwa yanapotea

Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri wangu, mkienda kwa dr msimueleze kama mshaenda hospital ingine na mmepewa majibu kama hayo uliyoyaeleza, mwache dr afanye uchunguzi wake halafu akupe findings zake then linganisha na majibu ya awali, ukiona ni tofauti mueleze dr kuhusu dr.mwanzo maelezo yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ectopic pregnancy ni utungwaji wa mimba nje ya mfuko wa uzazi (uterus)
Matokeo yake inategemea ni sehemu ipi imetungwa kama ifuatavyo
Tubal pregnancy -Hii ni mimba iliyotungwa kwenye mirija ya uzazi na mara nyingi haifikishi week 16 kwani mirija inapasuka
Ovarian pregnancy-hii utungwa kwenye mayai nayo pia hupasuka kabla ya wk 16
Intra-abdominal pregnancy-hii ni mimba inayotungwa tumboni (tumbo la juu) na inategemea na sehemu, zingine uendelea mpaka mtoto kuzaliwa kwa njia ya upasuaji
Nadhani hapo option ni kuwa na uhakika ni aina ipi ya Ectopic pregnancy but mimba ikiwa changa sana inaweza kuwachangamya sonographer

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa kiongozi tatizo daktari wake naye hakumwambia ni aina gani ya ectopic

Back
Top Bottom