DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,256
- 4,647
Salaam kwenu nyote!
Aisee kuna wakati hapa duniani binadamu tunajikuta katika mazingira magumu sana.
Hoja iko hivi, huyu binti (dada) tulikutana naye 2004 Novemba, tukapendana yeye wakati huo alikuwa anajiandaa kwenda A level, mimi nikaingia mitaani bongo kuzisaka. Baadae kulitokea mengine ya kawaida katika mahusiano yaliyopeleka yeye kunipiga kibuti. Nikiri kwamba huyu binti nilimpenda sana na kuniacha kule kulinichanganya sana. Ilinichukua miaka miwili kupona majeraha lakini sikuacha kumpenda.
Ilipita muda ila kama 2008 tukajaribu kurudisha majeshi kambini lakini kulikuwa na ukosefu wa imani kati yetu. Mimi baadae 2009 nikakutana na mwanamke mwingine nikaanzisha mahusiano na kufunga ndoa 2011. Kipindi hicho sina mawasiliano na ex wangu kimapenzi ila mazoea tu ya hapa na pale, nakumbuka nilimpa na mchongo mmoja akaenda UK kupitia programu moja hivi. Hivyo tulikuwa tu marafiki maana mimi tayari nilikwisha oa.
Yeye hajawa na mahusiano mazuri kama wengine so mara kwa mara amekuwa akinishirikisha mengi yanayotokea kwenye mahusiano yake. Mara ya kwanza alinishirikisha mkasa wake na aliyekuwa mchumba wake. Huyo kaka ni kwamba walipendana sana mchaga ila changamoto jamaa alikuwa na uraibu wa kujichua, huu uraibu ulimpelekea kukosa ufanisi kunako 6*6, jambo ambalo lilimsumbua ex wangu sana. Kwamba kuna wakati wangeweza kujiandaa kwa ligi hata masaa ila ikifika hatua ya nyoka kuzama pangoni, anasinyaa. Kwa mujibu wa maelezo yake, ile hali ilikuwa inamuumiza mwanaume zaidi mpaka anaishia kulia ila ndo hivyo. Cha kushangaza ni kwamba mwanaume alikuwa na uwezo wa kujichua mwenyewe fasta na kufikia kileleni ila ngono ndo hivyo.
Ikafika wakati ikabidi waachane. Baadae akakutana na jamaa mmoja alitokea sijui Marekani mtoto wakishua, huyu wakakutana jamaa akampanga sana, huyu ex wangu ni mtu wa kanisani sana sasa kwa msimamo akataka washiriki tendo baada ya kufunga ndoa. Maandalizi yakafanyika baada ya kuchunguzana kipindi cha uchumba ila baadae akaanza kuona dalili ambazo hakuzielewa kama vile mume kutokuwa na hisia za kimapenzi naye. Akanishirikisha, nikamshauri aendelee kujenga mahusiano yake kwa kumuelewa mwenzake. Kumbe alianza kumchunguza kwa undani zaidi, akagundua jamaa ana movements ambazo hazielewi, hususani mahusiano yake na wanaume wengine. Siku moja akagundua mumewe ana mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine, mume anapigwa miti.
Mke akaghafirika, ugomvi ukaanza ndani ya ngumba, haukusuluhishwa mpaka sasa, leo amenipigia simu kunifahamisha ni mwaka sasa toka ameondoka kwenye ile ndoa, anaishi peke yake, ana kazi nzuri inamlipa hivyo ameamua kuvunja ndoa na amewashirikisha wachungaji waliomuelewa na kusign nyaraka za kuruhusu ndoa kuvunjwa kwa misingi ya kwamba mume ni shoga, hii ndoa imedumu miaka kama 5 sasa.
Kwa upande wangu ndoa yangu ya kwanza ilivunjika muda sana na kwa sasa nina maisha mengine kabisa, wake zaidi ya mmoja na huyu ex wangu anafahamu hilo sema sasa mchana huu ananiambia anataka turudiane, niachane na wake zangu wote nimchukue yeye tu.
Hapa ndo nimeshindwa kumuelewa, nimemuambia kwa sasa hana jeuri ya kunipa masharti maana yeye ndo anatafuta tulizo mimi nipo sawa tu na wake zangu. Niweke wazi, nilichopewa na Mungu simuachii shetani, ni yeye tu kukubali kuunga tela hapo mume anaye. Ila masharti ya yeye kuwa peke yake siwezani nayo.
Hebu waangwana mnisaidie maoni.
Uzi tayari.