Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

VodaCom nathibisha ni wezi !
Jana nililuwa na Tsh.61000. Nikatuma elfu 30 kutoka Voda kwenda Mtandao mwingine wa Airtel,wakaniambia muamala haujakamilika.

Nikatuma tena wakaniambia Sina salio la kutosha. Nilipo angalia salio nikakuta imebakia Elfu 30430.

Nikaenda kwa wakala kulizia namba ya kuwatafuta wakasema ni 100.

Lakini nilipo waelezea tatizo langu pale kwa wakala akaniambia kuna tatizo la kimtandao hasa kutuma pesa kwenda mtandao mwingine, lakini baada ya muda pesa itafika tu. Ilikuwa usiku SAA moja.


Mpaka hivi Leo naandika bado pesa haijafika kule nilikotuma. Nikipiga simu 100 nambiwa niwasiliane na kwa social Media zao.

Imeniwiya ni vigumu sana. Nataka niende Vodashop.
 
Huwezi amini kilichomponza ni kuuliza "Ukisema kwenye mitandao swala lako ndiyo litakua limetatuliwa?" Angeweza ongea vizuri mpaka mleta uzi angeridhia
 
Kuna jamaa yangu wamekwapua laki 2 yake mwezi sasa..kibaya zaidi hakufanya malipo yeyote, yeye alihamisha toka M-Pesa kwenda MasterCard then akaghairi kulipia huduma, kuja kucheki airudishe pesa kote haionekani!!

Kiujumla voda wana customer care mbovu sana, wale jamaa hawajui wanachofanya hata sijui wana elimu gani, unawaambia hili wao wanajibu lile yan hawaeleweki hata kidogo!

Kuna siku nimenunua bundle, nawasha data hakuna kinachosoma..100 kuwapigia hata huwapati, naenda whatsapp wananipa majibu ya kipuuzi tu, lile bundle liliisha hivi hivi kifupi waliniibia.
 
Hii nenda huku nenda kule gharama za pesa na muda anafidia nani? Kama kuna kitu sipendi ni kuhangaishwa kwa makosa ya mwingine.

Hongera mleta mada kwa kuwakumbusha wana jamii, na unajua kuandika habari katika mtiririko mzuri.
 
Tatizo customer care ya hizi kampuni za hovyo kabisa ndio maana watu wanakimbilia social media kulalamika.
 
Usimtishe jamaa.
Vodacom wana wajibu wa kuweka miongozo na mifumo ya kuwalinda wateja wao wasiibiwe.
Vodacom na mitandao karibu yote kwa sasa wameharibu utaratibu wa mawasiliano kwa huduma kwa wateja, siyo kila mteja wao ana uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii au kwenda kwenye tovuti yao.

Wote wameondoa urahisi wa kupiga na kuongea na mhudumu wao na hii ni kero kubwa kwa wateja wao. TCRA na wale watetezi wa walaji wa bidhaa wanatakiwa wawalazimishe mitandao ya simu kuondoa huu urasimu. Tunatumia pesa zetu siyo mawe.
 
Wewe utakuwa mnufaika wa wizi huo wa voda,mimi nimeweka 1000 nijiunge,nilivyojaribu kuunga ikasema pesa haitoshi,nikacheki salio nikakuta 700/= nikaweka tena 1000,nikajaribu kujiunga ikasema salio halitoshi,nikacheki salio nikakuta ni ileile 700,nikaweka tena 1000,kujiunga ikasema tena salio halitoshi!!! Nilipocheki salio tena nikakuta 200/=tsh! Nikajaribu kupiga 100 wanieleze kulikoni,ikaishia kunipa maelezo ya bonyeza moja_2_3bila faida,sikuweza kabisa kuongea na mshauri badala yake niende facebook au whatsap,huko nako hakuna msaada wowote niliopata,nilichoamua ni kuchomoa hicho ki laini kutoka kwenye simu yangu na kukitafuna,sasa hivi nimefanikiwa kufuta matumizi ya voda kwa wanafamilia wangu wote
 
Pole sana Mkuu,
Ila mimi nimefanya transactions mingi tu kwa M-pesa MasterCard na sijakutana na shida yoyote.

Mara nyingi nimekuwa nikilipia manunuzi haswa AliExpress.
 
Hii mpesa mastercard ni utopolo, yani usijidanganye kufanya transaction kubwa zaidi ya elfu 50.
Week kadhaa zilizopita huduma haikupatikana kama week hivi, ukiingia kwenye website yao wanakupa cjui Tobi uchati nae, huyo tobi ni fala tu haelewi unachomweleza.
Bora nirudi kutumia ABSA tu kama mwanzo.
 
Tatizo customer care ya hizi kampuni za hovyo kabisa ndio maana watu wanakimbilia social media kulalamika.
Wanawatumia wanafunzi wa chuo wanaosoma certificates na diploma. Wanafanya part-time. Yaani wanachukua tu mtu wa fani yoyote na kumkaririsha maelezo na kumpa onyo la kuongea na mteja kwa dakika 3-5 na kukata simu. Wanapewa muda wa dakika za kuongea na mteja, zikifika wanatakiwa kukata simu bila kujali tatizo limesuluhishwa ama la
 
Kuna kitu inaitwa the doctrine of estoppel. Huwezi kukataa sasa kitu ulichokubali wajibu wake kabla na huku ukiwa na muda na facility za kujiridhisha kuwa kweli unawajibikwa kwa hicho kitu au jambo.

Kisheria mpaka sasa voda ndio wanapaswa kumlipa hela jamaa hata kama kiuhalisia amepigwa na watu wengine.

Doctrine hiyohiyo itamtoa mlalamikaji hapa ikiwa Voda watalazimisha au watashauriwa vibaya kumshtaki kwa 'kuchafuliwa'.
 
Mimi nilokosea kutuma pesa Airtel ikaendavkwa mtu mwingine nikajaribu kurudisha kumbe aliitoa chapchap Sasa Happ nawachafua Airtel kwa lipi? Sababu nilifanya procedure zote Hadi kwenda sio kazi ya Airtel kuhangaikia kule zimeenda Baada ya Mimi kukamilisha procedure zote za kulipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…