MREJESHO (sikuwapa kwa muda mrefu)
- baada ya bandiko Hili kuliweka mitandao mbalimbali usiku,
Asubuhi nilivyoamka nikapigiwa simu na manager (wa high level) akiomba msamaha kwa yaliyotokea na akasema tayari wameshairejesha pesa yangu yote kwenye simu yangu
- nikamwambia sawa, ila mmenipotezea muda wangu na kunipa hasara maana nilikuwa nimeteka kulipia Tshs. 471,016.73 kununua software fulani huko ulaya ili niitumie kwajili ya kurun membership site ambayo tayari nilikuwa nimeshafanya maandalizi tayari... So mmenipa hasara kwa kunikwamisha, so nahitaji fidia.
Akajibu kuwa
Wenyewe walikuwa hawafikiria hilo swala la fidia,
So
Kama nimewaza hivyo basi niandike barua official kwajili ya swala langu la fidia.
- nikacheki salio na Kweli nikaona wameirudisha...
- nikaandika barua mwenyewe na kuiwasilisha kwao...
Then
Nikajibiwa kuwa wao "ni kama hawahusiki" ktk swala la hasara na fidia... ila kama mteja wao wanaweza niwekea kiasi sawa cha Tshs. 471,016.73 kama just pole tuu (ila sio fidia).
So
Kwangu nilikataa nikaona ni kunikosea heshima na adabu kama binadamu na mteja.
Na pia wao kama kampuni wanakimbia uwajibikaji Kwa kusema wao hawahusiki problem iliyotikea, yaani Kwa lugha nyingine hawawajibiki ktk hilo swala.
- kitu kingine kilichotokea, baada ya kuanza kudai fidia... Muda Si mrefu wakabadilisha terms and conditions za huduma za malipo [ambapo walituma SMS nadhani kwa wateja wote, including nami ilifika]... (Why, walifanya hivyo... Kwamba kuna kitu waliona hakipo sawa kwa zile za awali ambazo mimi muamala wangu ulizitumia hizo za awali)
- baada ya kukataa hiyo 'ofa' ya pole... Nikaona niangalie wanasheria... Sasa kuna Ndugu yangu nikamshirikisha ... in short baada ya kumwachia hilo swala... sasa Ndugu naye hakuweka priority...
Mwenyewe Hasira zangu zikapungua baada ya muda...
So
Swala likapotea hewani hivyo.
ILA LEO NI BAADA YA MIAKA 3!
Kwa ufupi
- Waliharibu kabisa uhusiano nami kama mteja... Mpaka leo siwakubali... Unajua ukiona mteja hakukubali, mfanyabiashara mzuri ataakaa chini na kujitafakari.... Maana mteja ndio anayekupa fedha, so kama humthamini au kufanya namna uwe na uhusiano mzuri na mteja basi biashara yako haitafikia kiwango kizuri.
- walifeli kurudisha uhusiano na mteja hata baada ya kupata fursa hiyo maana walikana kuwajibika na Hilo lkn hawakuchua hatua zaidi kurudisha uhusiano huo... Inawezekana pia pesa walirudisha Kwasababu tuu ya presha ya mtandaoni, ila sio kwa kutegemea mfumo na utaratibu wa Ndani wa kampuni ktk kutatua kero za wateja Mmoja Mmoja!
- Kama wafanyakazi wadogo wadogo waliweza nitreat vile... Ina maana mfumo wa kampuni ndio upo vile? Mtoto wa nyoka ni nyoka? Ina maana mfumo wa kampuni hauwezi kuhakikisha watendaji wake hadi hawa wa chini kuwa na huduma cha kumridhisha mteja? Kwanini wa chini wapo hivyo? Wa juu?
- Mtandao ninaoutimia sasa ni Tigo (sio kwamba hawana shida, but for me sijakutana na kero kubwa kama hii)... Voda natumia mara chache and I don't give priority to it, ila pale tuu ambapo sina namna, but transaction zangu na miamala online natumia haswa Tigo sometimes Airtel... Ukizingatia na ma gharama ya Voda and how they treated me, walishanipoteza kama mteja wao!
- Sijajua kuna raia wangapi ambao nao wanapata kero ya miamala au pesa zao kukwama na mwishoni wakakosa cha kufanya na kisha wakapotezea... Wale wamama wa vijijini au watu wasio weza kusema na kufatilia mambo Kwa nguvu!
Kuna kampuni mtu ananunua bidhaa zao sababu tu hana alternative nyingine... Ila pia kuna mtu anakwenda kununua bidhaa kampuni fulani sababu anahitaji bidhaa hiyo na pia anaipenda culture na kampuni Kwa ujumla na anajihisi ni sehemu ya kampuni kama mteja, yaani ni ambassador wa kampuni!