Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

Nimerudi equity aisee jamaa wapo[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]yaani nimekata kadi hapo hapo na kufanya miamala hapo hapo najuta week zangu 3 nilizopotewa na mpesa MasterCard nimekoma na sitorudia utopolo ule tena....
Habari wana-bodi, kwa Majina naitwa Lwifunyo Mangula, ni mmoja wa watu wanaopenda technolojia ikiwamo IT ninaifurahia na nina kautaalamu kidogo kuhusu online business maana ninapenda hivyo vitu. So hapa nipo kutoa ushauri kwa wadau wengine kuhusu MPESA MASTERCARD TANZANIA kulingana na UZOEFU wangu wa niliopitia.

Mwanzo walipoleta MPESA MASTERCARD nikasema yes… kitu kizuri na nikajaribu kuitumia kwa mara kadhaa, lakini baada ya huduma mbovu nilizopata (HUDUMA YA MTEJA na KITEKNOLOJIA) kutoka kwao hivi karibuni basi nikaona niwashirikishe wadau nanyi msije ingia ktk changamoto za malipo mtandaoni na kiuchumi ktk shughuli zenu.

Tarehe 06/07/2020 niliingia ktk website moja ya ughaibuni kununua software Fulani na nikafuata taratibu za kufanya malipo na nikachagua 2checkout payment gateway, kisha Master Card kukamilisha malipo. Baada ya kubofya kitufe basi Tshs. 471,016.73 zikakatika katika akaunti yangu ya Mpesa Mastercard na nikapokea ujumbe wa meseji kuwa pesa imekatika. Ila nilipoangalia ktk website hiyo pesa ilikuwa haijawafikia na ukatokea ujumbe kuwa ‘failed’ na wakasema nilirudie.
View attachment 1522205
Meseji ya Mpesa MasterCard kwamba pesa imekatwa kwa malipo

Kutokana na hilo nikajaribu kuwasiliana na pande zote tatu ikiwepo mmiliki wa website, 2checkout na Vodacom Tanzania. Ila baada ya kufuatilia nikaona Vodacom ndio watu wa kunisaidia maana kule wanasema malipo hayajawafikia. Huduma kwa mteja kwa hawa 2checkout na mmiliki wa website zilikuwa nzuri ila KASHESHE ILIKUWA KWA VODACOM TANZANIA.
View attachment 1522208
Majibu ya 2checkout.com ya awali kabisa, huyu ni mtu halisi

Mawasiliano na Vodacom Tanzania
Baada ya hayo nikapiga 100 kuongea na mtu wa Vodacom lkn sauti yao ikawa inanielekeza niende ktk mitandao yao ya kijamii kupata msaada na KWA KWELI HUDUMA YA KUONGEA NA MHUDUMU KWA SIMU 100 WAMEZIFICHA. Nikaenda Vodacom Facebook page, duu kuanza kuchat nao nikakuta nachat na BOT AMBALO HATA HALINIELEWI nini msaada ninao hitaji. Yaani swala la pesa kiasi hiki 471,016 wanakupa roboti uchati nalo sijui kuonesha kwamba kuwa hawathamini pesa zako?
View attachment 1522210
Vodacom Tanzania Facebook Messenger Bot Wanayemwita TOBI

View attachment 1522211
Huyu Bot amenisaidia nini hapa na Tshs. 471,016.73 yangu kama sio kunikosea UBINADAMU?

Nikaenda Vodacom website yao, huko nikaanza kuchat na alikuwa sijui mtu halisi na akasema kuwa swala langu haliwezi kutatuliwa online hivyo niende Vodashop; sababu kipindi hicho nilikuwepo Njombe mkoa basi nikajitahidi niende huko.

Nilivyofika Njombe Vodashop (MKOANI) nikawaeleza tatizo langu na wakasema swala la MPESA MASTER CARD WAO HAWAWEZI LISHUGHULIKIA bali niwasiliane na makao makuu. Duuu! Nikawaambia nimewapigia 100 lkn simpati mtu wa kuongea naye maana wanasema niende ktk social networks zao kutatuliwa tatizo langu (kule nilikotoka kuwasiliana na roboti). Nikamwomba na kumbembeleza kuwa anisaidie kuwapigia basi hao 100 kwa simu yangu, akakubali na kunisaidia na akawapata akanipa niongee nao. Nikawaelekeza tatizo langu na yule mhudumu akasema swala langu litatatuliwa na pesa yangu ITARUDISHWA NDANI YA SIKU 3. Daah, siku 3, nikalalamika kwamba mimi siku 3 ni nyingi maana hiyo Tshs. 471,016.73 ni kubwa kwangu; nikambembeleza yule mtu ifanyike haraka na akasisitiza siku 3. Wakanitumia meseji ya support desk number ili niwasiliane nao kwa WhatsApp. Nikaenda WhatsApp kuwasiliana nao na kuomba tena muda usiwe siku 3 lkn kwa kuchelewa wakanijibu wakisisitiza zitarudi ndani ya siku 3 na watanitaarifu.
View attachment 1522212
Vodacom WhatsApp Support

View attachment 1522218
View attachment 1522219

Vodacom Tanzania Wameanza Kunipiga Chenga Mteja
Okey, nikawa mpole na nikasubiri siku 3 zikapita na sikupokea pesa wala simu wala meseji. Nikawapigia 100 tena kwa kuifukua walipoficha huduma nikawapata na wakaniambia lile swala inabidi niende Vodacom Shop nikaandike barua ya kuomba pesa yangu kurudishwa nikiwa na kitambulisho. Duuu, sura mpya hapa! Ikabidi nifanye hivyo na kwenda Vodacom Shop Njombe. Nilipofika pale wale wahudumu wakashangaa kuhusu barua, baadaye wakajaribu kufuatilia wakasema inabidi nijaze fomu. Wakanipa fomu nikajaza na kuweka nakala ya kitambulisho. Nilipokuwa pale nakumbuka kuna kaka mmoja alikuwa na tatizo la post-paid kwa simu, aliwawashia moto pale na baadaye nikaona wanapunguza spidi kunihudumua mimi na kumshuhurikia yule kaka maana amewasha moto.
View attachment 1522220
Fomu ya kuomba pesa irudi from Vodacom , niliandika kwa Kiswahili na wao hawakunipa maelekezo ya Lugha
View attachment 1522223

Nikasubiri baada ya siku kadhaa kwamba pesa yangu itakuwa imerudi… wapi bado. Nikawapigia simu 100 na nakumbuka alipokea mkaka, huyu alikuwa mwelewa kidogo na akasema swala langu litatatuliwa ndani ya masaa 24. Nikamweleza nimeandika barua, nimepiga simu, nimeenda Vodacom Shop mkoa ila bado… akaangalia taarifa zake akasema anaomba washughulikie na ndani ya masaa 24 pesa nitakuwa nimerudishiwa pesa zangu. Okey nikaongeza uvumilivu.

Hapa Ni Kama Siku 21 Bado Vodacom Wananizungusha
Baada ya siku kama 2 nikaamua kuwapigia tena baada ya kuona masaa 24 yamepita na pesa sijapata. Alipokea mdada na akasema sawa ngoja basi walishughulikie (kama hawafahamu vile nilianza hii kitu tangu siku nyingi, hawana connection), nikamsisitiza kuwa nimewasiliana na Vodacom kwa muda mrefu na hii ni kama siku ya 21 tangu nifanye malipo. Nikamwomba na kumbembeleza nionge na Mpesa MasterCard Manager, baadaye akakubali na akanisubirisha na kisha nikaongea naye! Yule kaka manager, akaomba anipigie kwa simu private. Baadaye akanipigia na kumweleza mkasa mzima na kumwambia barua tayari niliandika na akasema anafuatilia na atanirudia baadaye. Baadaye alivyonipigia akasema barua ameiona na majibu yalikuwa inabidi nirudie kuandika barua kwa lugha ya Kiingereza ila walikuwa wamesahau kunitaarifu (kwahiyo bila mimi kuwapigia na kufuatilia huo mrejesho nisingepata na pesa ingekuwa imepotea). Nikamwambia vipi kama sijui kuandika Kiingereza? Akasema naweza omba mtu anisaidie kuandika hiyo barua ya kiingereza. Ikabidi nikubali kufanya hilo na nikamwambia kwa namna huduma mbovu ninavyoipata basi nitaenda ktk mitandao ya kijamii kuwaambia umma wasitumie huduma yao ya Mpesa MasterCard maana naona sisikilizwi na ni bora niwataarifu wengine wasiangukie tatizo kama hili; akanijibu kwa kuniambia kuwa kwa kwenda kuongea ktk mitandao ya kijamii ndio itatatua swala langu?

Tarehe 30 July 2020
Tarehe 30/07/2020 nikaenda Vodashop mkoa Njombe kuandika barua sasa iwe ya kiingereza. Nikafanya kama walivyotaka na kuiacha pale… bado nasubiri nione mrejesho wao utakuwaje; sijui watanipa pesa zangu au watazipotezea? Au sijui watanipigia simu au kutuma meseji kunipa hatua nyingine ya kufuata? Sijui ndio watakaa kimya bila mrejesho wowote mpaka nianze kufuatilia tena?
View attachment 1522228
30 July 2020 Fomu ya Kiingereza Niliyojaza

Nionavyo Mimi Na Ushauri Wangu Kuhusu Huduma Za Mpesa Mastercard Tanzania
  • Kulingana na huduma nilivyopata (Huduma ya Kiteknolojia na Huduma kwa Mteja) basi nina mashaka sana na uhakika wa HUDUMA ZOTE na MAONO mazima ya kampuni hili kama kweli limedhamilia KWELI KUWASAIDIA WATU ktk huduma mbalimbali maana HUDUMA KWA MTEJA inatupa picha juu ya FIKRA ZA KAMPUNI ktk kuhudumia WATU ambao ni wateja sisi. Mara nyingine ni bora teknolojia ifeli ila MAHUSIANO NA MTEJA YATUNZWE hii italeta maana ya kwamba huyu mtoa huduma ana NIA njema nawe, ila kwa mimi nilivyoona basi hawana hiyo NIA YA DHATI ya kumhudumia mteja labda wana malengo yao mengine.
  • Kama swala la pesa linatoka ktk simu yako ila mlengwa (muuzaji) aliye nje ya nchi haipati, basi kuna uwezekano labda mfumo wao haujakaa vyema ktk kumsaidia mteja kuweza kufanya biashara ya UHAKIKA na mtu mwingine wan je ya nchi. Hivyo inawezekana labda hakuna uhakika wa malipo ya MPESA MASTERCARD ktk biashar zetu. Okey sawa labda tatizo ni la muda, mbona zinakaribia siku 30 hakuna utatuzi wake pesa iende au irudi ktk simu yangu?
  • Swala la kuelekezwa niende ktk mitandao ya kijamii kupata msaada na nikaenda huko na kukuta Bot ndie anayenisikiliza kuhusu pesa yangu ya Tshs. 471,016.73 na mbaya zaidi ninamweleza huduma ninayohitaji wala hanielewi: Binafsi ninaona huku ni kukosa UTU na UBINADAMU kwa mteja maana sisi sio mashine bali ni watu wenye hisia na roho; kwa haraka haraka ninavyojua mimi Tshs. 471,016.73 ni pesa nyingi sana kwa mteja ambayo ni kama mshahara wa mtu ambaye ana majukumu ya kutunza familia. Pesa ina nguvu ya MOYO sasa hili wao sijui hawajali ktk wateja sisi? Kama pesa ya 471k unapuuzwa na kupewa roboti likusaidie, je ndugu yangu wewe mwenye kutuma Tshs. 5,000/= utaongea na nani? Ndugu unasubiri likukute lipi ktk pesa yako?
  • Mbona ile website ya ughaibuni na 2checkout waliweza kunihudumia kama mteja na kunipa mrejesho wa haraka wenye mwongozo ijapokuwa wao wapo mbali sana huko, lakini Vodacom ambao wapo hapahapa Tanzania wanaficha huduma za simu 100 kuongea nao; okey hata ukienda ktk mitandao ya kijamii online unaanza kuchat na Bot ambaye hakuelewi… daah. Okey Nikaenda VodaShop Njombe Mkoani na wakasema swala langu la Mpesa MasterCard wao hawawezi kulitatua mpaka makao makuu…Duu. Kwanini Nje waweze toa huduma nzuri, ila hapa hapa Tz washindwe? Inawezekana labda kampuni hili lina shida ya ‘MAHUSIANO YA KIJAMII NA HAWALIPI SWALA HILO UZITO KAMA THAMANI YA MTEJA’. Je, wafanyakazi wake wanafurahia kutoa huduma kwa wateja sisi au wanahasira na kazi hiyo?
  • Kama Bot wa facebook messenger wao wameshindwa kum-program vyema kuweza kunitatulia shida yangu au kuniongoza cha kufanya, Basi je inakuwaje mifumo mingine mbalimbali inayomuhusu mteja ambayo sisi hatuoni au kwa harakaharaka sisi hatuifuatilii? Just Bot programing iweze nijibu swala langu? Wadau hili mnalionaje kuhusu mifumo mingine ambayo sisi hatuioni? Yale mahesabu yetu ambayo sisi hatuyaoni? Umewahi fuatilia kwa undani? Unaweza nipa mchanganuo wa in and out zako kwa mwaka mzima ktk simu yako? Je, kuna urahisi gani wa kupata na ku-question hesabu za in and out zako ktk simu yako na ukapata msaada huo kutoka kwao inavyotakiwa? Nakosa imani kutokana na hili nililolipata la Bot.
  • Kama pesa ya mtu niliambiwa inachukua siku 3 na sasa ni karibia siku ya 30 (almost 10 times) bado sijapata, je, wewe mwenzangu una uhakika gani wa pesa ambayo utalipia kwa Mpesa MasterCard? Embu fikiri mfano nilikuwa namtumia labda rafiki yangu ambaye anaumwa na inabidi apate huduma ya kiafya na yupo nje ya nchi na akikosa ndani ya siku 7 huduma hiyo anafariki, hivyo basi angeweza kuwa amefariki tayari! Kwahiyo ni KIFO! Je, kama ulikuwa unauza nyanya zako na pesa ikakwamishwa kwa muda wa siku 21, je nyanya hizo mtanzania mwenzangu zitakuwa bado zipo nzima au zimeshaoza? Uhakika wa biashara yako kwa MPESA MASTER CARD upo wapi? Maana biashara ni MUDA; mfano umechelewa kuwasilisha tenda document ya ujenzi dakika chache tuu basi automatic unakuwa umeondolewa ktk mchakato wa kushindania tenda; je Uhakika wa biashara na kampuni yako upo wapi hapo?
  • Swala la kupewa ahadi zisizotekelezwa kuwa ndani ya siku tatu, ndani ya masaa 24… utakuwa umepata pesa yako… linaleta ukakasi. Je, ahadi nyingine zinazotolewa ktk huduma nyingine zina ukakasi wa hivi hivi? Tuna uhakika gani wa kuzipata?
Ndugu zangu kulingana na maelezo niliyoweka hapa ambayo yamenitokea, baada pia ya kuunganisha dots za mawazo na niliyoyapata ktk huduma za Mpesa MasterCard basi ninaona HAKUNA UHAKIKA WA HUDUMA kwa Mpesa MasterCard. Tshs. 471,016.73 sio ndogo wala kubwa sana ila kama sijapewa huduma inayotakiwa kwa pesa yangu hiyo, Je, wewe una uhakika gani wa kufanya biashara vyema? Okey kama tatizo likitokea je, wanakusaidia swala lako a kipesa kwa muda gani? Bishara yako itaweza kukaa bila pesa hiyo kwa muda gani? Unataka kutuma milioni ngapi kupitia Mpesa MasterCard, una uhakika gani?

Kama kuna watu wengine wamekutana na shida kama yangu au inayoendana na yangu kupitia huduma hii ya Mpesa MasterCard au Vodacom Tanzania, karibuni kuweka yenu hapa chini. Yamekuwa yakisikika malalamiko mengi ya bunde kuisha haraka… Je, hili lipo? Tuna uhakika gani na huduma kupitia watu hawa?

Makala hizi nitaendelea kuandika ktk mitandao kama Facebook, Twitter, Medium, Quora, YouTube, Instagram, Reddit, Trustpilot. Pia nitaomba media mbalimbali kuniruhusu kuandika kama: Businessinsiders, Techcrunch, IT forums, IT professional journals, Finance & Bankers professional journals, Investors professionals journals, blogs, magazeti ya ndani na nje ya nchi. Ninaandika ili kuwataarifu watu wengine wawe makini na huduma ya Mpesa Master Card maana wasije wakapitia matatizo ya fedha kubwa pengine zaidi ya mimi. Nitaacha kuandika makala hizi mpaka pale ambapo Tatizo na Kero niliyoipata itakapotatuliwa pamoja na wao kujirekebisha ktk hili!

Nina sisitiza watu tuandike zaidi yale ambayo tunatendewa na makampuni haya maana wewe mwenyewe ni shahidi wa kero unazozipata. Hivi, je kama bundle lako likiisha ghafla in unrealistic way na ukawapigia simu na wasitatue, huwa unaenda polisi kufungua kesi yako? — Tuandike makala hizi kuisaidia jamii yetu, watajirekebisha au biashara itawashinda kwa SAUTI YA UMMA…
 
Hao crdb wana mlolongo mrefu sana, kuna kipindi mwaka 2014 nilizungushwa miezi mingi sana mpaka mwaka 2015 hamna kitu zaidi ya kwenda tu ofisini kwao na kusainishwa fomu kila nikienda.

Cha kufanya nenda equity bank au bank abc unatengenezewa kadi ndani ya dakika kumu n autaweza kufanya miamala mtandaoni kwa haraka na usalalama...
Hata Nmb MasterCard yao ipo vizuri
 
Na nimuhakikishie tu hio pesa haigandi hewani kusema ni pending, ishachomolewa na kwa vile hakutumia paypal inakua vigumu kabisa kurudishiwa pesa

Ok,

Lets assume pesa ishachomolewa kama unavyosema.

Meaning 3rd part/merchant ameshaipata ila anafanya utapeli kwa mwana.

Then, kwa misingi hiyo hiyo....utumiaji wa PayPal ungesaidiaje kurudisha pesa ambayo umesema tayari 'imechomolewa'?
 
Paypal wanaruhus miamala ambayo imehakikishiw ipo na sio ya utapeli, Endapo paypal ingetumika hapa basi paypal wangekuwa hawana budi kumrudishia pesa alielipa na wao kumchunguza huyo tapeli na kumchukulia hatua za kisheria, Paypal ni kama bima
 
Na wamefanya makusudi kabisa,
Usimtishe jamaa.
Vodacom wana wajibu wa kuweka miongozo na mifumo ya kuwalinda wateja wao wasiibiwe.
Vodacom na mitandao karibu yote kwa sasa wameharibu utaratibu wa mawasiliano kwa huduma kwa wateja, siyo kila mteja wao ana uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii au kwenda kwenye tovuti yao.

Wote wameondoa urahisi wa kupiga na kuongea na mhudumu wao na hii ni kero kubwa kwa wateja wao. TCRA na wale watetezi wa walaji wa bidhaa wanatakiwa wawalazimishe mitandao ya simu kuondoa huu urasimu. Tunatumia pesa zetu siyo mawe.
 
Paypal wanaruhus miamala ambayo imehakikishiw ipo na sio ya utapeli, Endapo paypal ingetumika hapa basi paypal wangekuwa hawana budi kumrudishia pesa alielipa na wao kumchunguza huyo tapeli na kumchukulia hatua za kisheria, Paypal ni kama bima
Hapana mkuu

Nakushauri ukasome tena PayPal Disclaimer Policy.

PayPal ni digital payment platform, only that.

Haihusiki na kuchunguza kama huyu mtumiaji ni scammer ama ni muungwana.

Jukum lao ni moja tu, kuhakikisha mteja wao amefuata requirements zote zinazotakiwa kufungua hiyo account yake.

Jukumu la kujua mtu ni tapeli or not lipo kwa mlipaji, yeye ndo anatakiwa kujiridhisha.

Pia, PayPal hai act kama bima, no...inachofanya ni kukuongezea tu security kwa bank account yako.

Kwamba badala ya account yako ya bank/card kuwa exposed online kwa website ambazo huziamini sana...Paypal inaingia kati, yenyewe ndo inakua exposed.

PayPal ni mfumo tu wa malipo kama ilivyo Skrill, Neteller ama Google Pay
 
Mimi nafanya miamala kwa paypal tangu mwaka 2013 kabla hata ya hizi master card za voda kufika, nina uzoefu wa miaka 7 mpaka sasa na ninajua nachoongea.

Nimekuwa refunded zaidi ya mara kumi kwa bidhaa ama huduma nilizoagiza mitandaoni na kulipa kwa paypal ambazo hazikunifikia.

Tupo kwenye hii sekta muda mrefu sana, Paypal ni kama bima tu inayokuhakikishia endapo ukiitumia kufanya malipo na hutapata ulicholipia ama kipo chini ya kiwango basi utarudishiwa pesa yako kama ambavyo mimi binafsi nilivyorudishiwa pesa karibu maea kumi.

Nisingetumia paypal ningekua sina pa kilalamika na pesa ingeenda.
 
Sio Vodacom tu, tatizo ni mitandao yote ya Tanzania, banks zote za Tanzania, mambo mengi wanafanya kienyeji kwa kalamu na karatasi, alafu wafanyakazi wengi vilaza, na wengi wavivu, yaani wao mishahara inaingia kila mwisho wa mwezi kwa hiyo hawajali chochote wafanye kazi wasifanye mshahara uko palepale.
Ukweli customer care Tanzania ni tatizo kubwa mno, kampuni nyingi washenzi sana watu wameridhika na maisha. Vodacom ukiwa na tatizo unaweza watafuta mwezi mzima wanakuzungusha, email ukituma hua hawazisomi, mfanyakazi anaingia ofisini hadi anatoka hajafungua email ya kazi anafika anagusa document mbili tatu, anapiga soga na wenzake siku imeisha. Stupid assholes. Tanzania haiwezi kuendelea ina mijitu mivivu sana kwenye kila sector.

Alafu kama software developer experienced miaka zaidi ya 10 ngoja nikwambie kitu, software hizi za mitandao kama vodacom siwezi tumia mwenyewe kwa kua nishaziona najua walivyotengeneza nyiingi ni ovyo mno, yaani zinafanya kazi basi tu tatizo lolote mnaweza poteza hela zenu zote, hua nawaambia watu msitunze hela kwenye mitandao ya simu, siku ikishut down hawawezi hata kurecover wakajua nani alikua na kiasi flani, yaani data zote zinapotea mtabaki mkose wa kulaumu maana hata serikali itakua haina la kufanya. Use at your own risk kwa kweli
 
Mimi nafanya miamala kwa paypal tangu mwaka 2013 kabla hata ya hizi master card za voda kufika, nina uzoefu wa miaka 7 mpaka sasa na ninajua nachoongea.

Nimekuwa refunded zaidi ya mara kumi kwa bidhaa ama huduma nilizoagiza mitandaoni na kulipa kwa paypal ambazo hazikunifikia.

Tupo kwenye hii sekta muda mrefu sana, Paypal ni kama bima tu inayokuhakikishia endapo ukiitumia kufanya malipo na hutapata ulicholipia ama kipo chini ya kiwango basi utarudishiwa pesa yako kama ambavyo mimi binafsi nilivyorudishiwa pesa karibu maea kumi.

Nisingetumia paypal ningekua sina pa kilalamika na pesa ingeenda.
Kuna kitu hujaelewa

Kwanza, sikatai kwamba wewe ni mzoefu.

Lakini pia sikatai kwamba umewahi kuwa refunded.

The issue is;

Ukinilipa pesa sasa hivi mimi through PayPal and sina refund policy yoyote na hiyo pesa nikaitoa....PayPal hawaendi kutoa pesa yao mfukoni kuku refund wewe.

By the way wala hawatakiwi kukulipa. Why?.....kwa sababu hawajafanya kosa lolote.

Wewe ndo una jukum la kujiaminisha ubora wa product unayonunua & ubora wa seller.

Ndo maana kuna reviews kuhusu products na sellers mbalimbali.

Unacho confuse wewe ni refund policy ya merchant (anayekuuzia bidhaa).

Kama seller wako amesema ataku refund full, ama partial in case of any error, yeye ndo ata authorize hiyo refund.

Na kama mlifanya transactions zenu kwa PayPal refund itatumia same way. Hii ni kutokana na Paypal business account kuwa option inayoitwa 'Refund'

Anyways, tufanye hivi...simple;

Hivi hicho unachosema wewe kingekiwepo huoni watu wangefanya deals watumiane pesa then baadae mmoja aka play victim kwa PayPal na kusema ametapeliwa ili apewe hiyo refund unayosema?
 
Mbona hii michezo inatajirisha watu hadi leo, Watu wanakula refund mpaka basi, Kama ulikuwa hujui basi ndo nakujuza hivi vitu vipo, karibu ulimwengi wa paypal.

Maama usipopewa ulicholipia wewe na uliemlipa mnapewa muda fulani mjue mtatuaje tatizo, zikiisha hizo siku na uliemlipa anakuzungusha, kakiri kos aau kapiga kimya unalipwa.

Hakunaga janj janja huku paypal
 
Mimi mwenyewe wamenipiga elfu56 zangu tarehe 26/7/2020 kunakitu nilitaka kununu Alibaba nilipojaribu kuweka pesa kwenye account ya m pesa master card nilirudishiwa ujumbe kuwa failed! nilipo angalia salio kwenye m pesa yangu pesa ikawa tayari imekatwa nilipo angalia salio upande wa MasterCard ikawa inasoma 00,niliwapigia simu huduma kwa wateja kilasiku wananizungusha wameshindwa kabisa kurudisha pesa yangu mwisho nimekata tamaa nimeamua kuwachia hiyo pesa jamaa ni wezi sana,nainaonyesha wanatufanyia makusudi kutuibia pesa zetu wateja.
 
Mbona hii michezo inatajirisha watu hadi leo, Watu wanakula refund mpaka basi.

Hakunaga janj janja huku paypal

Duh!

Unaji contradict;

Umesema hakuna janja janja PayPal...yet ukadai michezo ya janja janja through PayPal refund imetajirisha watu.

Hivi inakuaje unaamini watu wanaweza endesha biashara ludicrously namna hiyo?

Kwamba negligence yako ya kutokufanya research vizuri kuhusu service & service provider iicost smart company kama PayPal?

Na hiyo bima unayosema ya PayPal inafanyaje kazi while huilipii? Kwamba they're doing you a favor?

Mbali na fees zao zinazoanzia 2% hadi 4% ya transaction kuna mahali wamewahi kuku charge bima?

Nirudie, tafuta tena PayPal disclaimer policy uisome vizuri
 
nachomaanisha ni kwamba paypal ni salama kwa mlipaji ila kwa upande wao wana risk ya kupoteza pesa kwasababu kuna watu huwa wanapokea vitu ila wanadanganya havijafika na wanalipwa hii inakuwa hasara kwa paypal.

Ila kwa mteja mqenye nia njema hawezi kutumia usalama wa paypal kwa kujinufaisha yeye kwa kiwadanganya paypal mizigo aliyolipia haijafika au ni feki.

Binafsi kuna kipindi mzigo wangu haukufika zaidi ya miezi miwili nika rudishiwa pesa ila mizigo ilifika baada ya kupokea hela, hii ni loophole kwa matapeli na watu wanafanya hii michezo.

Nimesema paypal ni kama bima sijasema ni bima mkuu uwe unasoma na kuelewa, Yes ni kama bima maana ukilipia kwa kadi directly upo tayari kwenye risk ya kupoteza pesa ndio maana mabenki mengi yakikupa kadi wanakupa tahadhari usi tumie kadi direct maana hizo number na kadi yako zikivuja kwa hackers basi kama kuna hela imebaki kwenue kadi wao wataitumia bila ridhaa yako na utaingia hasara

Haya yasingemkuta mwenzetu kama angetumia paypal na inawezekana kabisa muuzaji wa hio softwarw hakuwa na vigezo vya kutosha kukubaliwa na paypal, yawezekana ni mnaijeria
 
Sio kweli hao uzoefu hawana .Pesa ikiondoka haiwezi elea angani.Ukiona salio limepungua hiyo ilishatoka na kutua ardhini inatakiwa uidai toka ilikotua Sio Vodacom

Halafu Vodacom haiwahusu wenye mtandao wa Master card Ndio waweza just what happened

Mleta mada wasiliana na Master card wenyewe

Usiwe na maneno mengi andika tarehe hii hapa nilifanya malipo kwa kampuni hi hapa kwa kutumia master card yenu namba hii.Hela wanasema hazikufika wakati kwenye card yangu namba hii hii hell kwangu ziliondoka .Watakusaidia chap chap.Nenda website ya master card.Ila andika kifupi Sio Hadith ndefu go direct to the point.Sababu hizo customer care zao huwa busy kuliko kawaida be short and clear usiandike hotuba

Kuhusu kuandika kwa hicho Cha kuchafua Vodacom kila eneo kwa kitu usichpjua kwa uhakika waweza ishia jela na kudaiwa mabilioni kwa kuchafua kampuni
Dai Hali yako kwa adabu na heshima na usijifanye una uhakika Sana kuwa tatizo liko Vodacom!! Pesa uruhusu wewe ziondoke Halafu. Uwakomalie Vodacom

Sema wao Wana huruma ningekuwa Mimi ndio MD saa hii ungekuwa unakiona Cha mtema kuni mahakamani

hebu acha upumbavu ww unadhan alichoandika hapa niuongo watu tumepoteza sana hela kwa mtindo huo lakini tumekaa kmya tuu bora yeye amekuja kuwaambia ukweli hapa
 
Mimi nina ishu na Airtel MasterCard tatizo kwa simu 100 lilishindikana so nikaenda shop kwao....Nimeacha maelezo yote now nasubiri muamala uingie..Wasipo tatua suala langu nami naja kuwachafua humu mapovu kama yote 400000+ sio kitu ndogo kuibiwaView attachment 1522841
NAWASHUKURU AIRTEL KWA REFUND YANGU
WhatsApp Image 2020-08-03 at 14.35.13.jpeg
 
Sio kweli hao uzoefu hawana .Pesa ikiondoka haiwezi elea angani.Ukiona salio limepungua hiyo ilishatoka na kutua ardhini inatakiwa uidai toka ilikotua Sio Vodacom

Halafu Vodacom haiwahusu wenye mtandao wa Master card Ndio waweza just what happened

Mleta mada wasiliana na Master card wenyewe

Usiwe na maneno mengi andika tarehe hii hapa nilifanya malipo kwa kampuni hi hapa kwa kutumia master card yenu namba hii.Hela wanasema hazikufika wakati kwenye card yangu namba hii hii hell kwangu ziliondoka .Watakusaidia chap chap.Nenda website ya master card.Ila andika kifupi Sio Hadith ndefu go direct to the point.Sababu hizo customer care zao huwa busy kuliko kawaida be short and clear usiandike hotuba

Kuhusu kuandika kwa hicho Cha kuchafua Vodacom kila eneo kwa kitu usichpjua kwa uhakika waweza ishia jela na kudaiwa mabilioni kwa kuchafua kampuni
Dai Hali yako kwa adabu na heshima na usijifanye una uhakika Sana kuwa tatizo liko Vodacom!! Pesa uruhusu wewe ziondoke Halafu. Uwakomalie Vodacom

Sema wao Wana huruma ningekuwa Mimi ndio MD saa hii ungekuwa unakiona Cha mtema kuni mahakamani

Sasa unamchimba mkwara mtu aliyeibiwa na wakati amewasiliana na wahusika na mekubali kuwa atarudishiwa, wewe ni nani mpaka ukatae? achaVoda wenyewe wajibu
 
Back
Top Bottom