Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

Mm pia lakini sasa nimekua muhanga sina hamu na mastercard ya9
Pole sana Mkuu,
Ila mimi nimefanya transactions mingi tu kwa M-pesa MasterCard na sijakutana na shida yoyote.

Mara nyingi nimekuwa nikilipia manunuzi haswa AliExpress.
 
Tumieni benki kufanya malipo ya mitandaoni, huko kwenye makampuni ya simu siku ukipatwa na tatizo lolote hutamuona wa kukupatia msaada wa haraka.
 
Acha kulalamikia vodacom wakati tatizo ni wewe uliyetuma pesa kwa mtandao ambao sio genuine.

Vodacom wapo vizur mno kwenye hio huduma yao ya mpesa mastercard.
Nishawahi nunua kitabu ciscopress ikabaki kama laki moja hivi kwenye account ya mastercard nikawa nimeiacha hio pesa tu.
Juzi account yangu ime expire nikarudishiwa pesa yangu kwenye mpesa.

Aliyekupiga ni yule uliyemtumia pesa sio vodacom
 
Vodacom M-Pesa MasterCard ni mkombozi sana sijawahi kupata shida kwani nimelink Card na paypal kama jamaa ninwezi paypal unaweza kurudisha mhamala faster

Unaposema wewe Mtalamu wa IT sio peke yako tupo wengi na tupo makini kwanza kiochunguza hiyo website ,seller husika kusoma feedback yake kabla ya kufanya malipo

Hebu weka website tuone kweli ni trust au la kama umenunua kwa matapeli au laa,

Hata kama ungetumia card ya Crdb au benk yoyote tatizo hilo lingeweza kutokea jukumu la voda Na MasterCard ni kuhakikisha pesa inafika kwa mhisika je iliwa watakuhakikishia pesa ilifika kwa mhusika ujasemaje ?
 
Sio kweli hao uzoefu hawana .Pesa ikiondoka haiwezi elea angani.Ukiona salio limepungua hiyo ilishatoka na kutua ardhini inatakiwa uidai toka ilikotua Sio Vodacom

Halafu Vodacom haiwahusu wenye mtandao wa Master card Ndio waweza just what happened

Mleta mada wasiliana na Master card wenyewe

Usiwe na maneno mengi andika tarehe hii hapa nilifanya malipo kwa kampuni hi hapa kwa kutumia master card yenu namba hii.Hela wanasema hazikufika wakati kwenye card yangu namba hii hii hell kwangu ziliondoka .Watakusaidia chap chap.Nenda website ya master card.Ila andika kifupi Sio Hadith ndefu go direct to the point.Sababu hizo customer care zao huwa busy kuliko kawaida be short and clear usiandike hotuba

Kuhusu kuandika kwa hicho Cha kuchafua Vodacom kila eneo kwa kitu usichpjua kwa uhakika waweza ishia jela na kudaiwa mabilioni kwa kuchafua kampuni
Dai Hali yako kwa adabu na heshima na usijifanye una uhakika Sana kuwa tatizo liko Vodacom!! Pesa uruhusu wewe ziondoke Halafu. Uwakomalie Vodacom

Sema wao Wana huruma ningekuwa Mimi ndio MD saa hii ungekuwa unakiona Cha mtema kuni mahakamani

Acha kuwatetea hao vod!
Voda ni wezi, kuna haka kamfano kadogo tu una 1000/= kamili kama salio la muda wa maongezi, unanunua kifurushi cha 1000/= then unapata ujumbe salio halitoshi angali ipo hiyo 1000 kamili!
Ina maana gani hiyo...!?
 
Mkuu nadhani tatizo ni kwamba umepigwa na sehemu uliyonunua hio website na pesa imewafikia ila wamekutandika. Sidhani kama vodacom wana tatizo lolote.

Siku nyingine Tumia paypal kulipia vitu online kwa kutumia kadi hii itakuwa ni kama ngao,

Hapo hakuna msaada, Ni vyema tu labda ungeweka wazi ni softwarw gani ulitaka kununua katika website ipi maana kuna wevsites kibao ambazo ni feki.

Binafsi natumia hii huduma kwa muda mrefu tu nmeagiza vitu, Kulipia software, kulipia services kama website na vitu kibao bila tatizo lolote.

Sio kila mtandao wa kulipia kwa kadi bila paypal, Hakikisha unajiunga na paypal kulipia vitu, Ukilipia kwa kadi directly ukipata hasara hio ni juu yako wewe,

Ulinunua softwarw gani kwa hio lako 4 na website ni ipi???
Mnachoshindwa kuelewa ni kuwa Vodacom wanawajibika kwa kukubali kwao kuwa hela ipo pending na itarudi baada ya siku kadhaa, mpaka sasa hawajakataa kuwa hela haipo kwao.

Wangekataa mapema, mlalamikaji angetafuta namna nyingine ya kupata fedha yake.

Kwa hiyo awe ameibiwa na wanaijeria, wachina nk bado Voda wanawajibika kumlipa kwa kuwa wamekubali na kumuaminisha mlalamikaji kuwa kosa lipo kwao na fedha yake watamrejeshea.

Kwa hilo hawachomoki
 
Acha kulalamikia vodacom wakati tatizo ni wewe uliyetuma pesa kwa mtandao ambao sio genuine.

Vodacom wapo vizur mno kwenye hio huduma yao ya mpesa mastercard.
Nishawahi nunua kitabu ciscopress ikabaki kama laki moja hivi kwenye account ya mastercard nikawa nimeiacha hio pesa tu.
Juzi account yangu ime expire nikarudishiwa pesa yangu kwenye mpesa.

Aliyekupiga ni yule uliyemtumia pesa sio vodacom
Waambie voda ili wampe jamaa hilo jibu
 
Hivi who told you Mpesa Mastercard ni salama? Nyie watu, hivi ukipata tatizo unajua bank ya Mpesa Mastercard iko wapi? Sbb tatizo la fedha ukipata unaenda bank na unapata utatuzi, sasa kuwa na Mastercard wakati hujui bank iko wapi ni kosa sana, au wengi mlijua Mastercard ni kama Mpesa au tigopesa ya kawaida tu? Muwe na Mastercard za bank plz.. Mtalizwa sana msipokuwa makini.
 
Hata Mpesa nimeacha kutumia kabisaa,..na lain nishaiweka jikoni..hawawez kunizimia laini kizembe zembe tu..
 
Hivi kwani huko mikoani hakuna BancABC au Exim bank ukanunue Cash Card uanze kulipia vitu mitandaoni mkuu?
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Pole mkuu.

Next time nashauri utumie bank. Malipo yanaweza fail hilo ni kweli, ila angalau wale wapo kwenye field yao hivyo ni rahisi kusaidiwa.

Ni tofauti na customer service wa mitandao ya simu ambao wapo trained kusikiliza shida yako tu na kui push forward, sio kuitatua.

Cash card ya BancABC inapiga kazi mubashara kabisa in case ukihitaji recommendation.

ABSA pia wapo safi sana + customer service yao ni top class
 
Tumieni benki kufanya malipo ya mitandaoni, huko kwenye makampuni ya simu siku ukipatwa na tatizo lolote hutamuona wa kukupatia msaada wa haraka.
Card zangu zote za crdb MasterCard na VisaCard zinagoma zinataka nijaze securecard nazo crdb huduma kwa wateja hawaelewi naambiwaga utapokea sms yenye code ndio hakuna lazaidi....Yan ile kwenda kwenye tawi pia kwangu ni changamoto.
images.jpg
View attachment 1523422
 
Mnachoshindwa kuelewa ni kuwa Vodacom wanawajibika kwa kukubali kwao kuwa hela ipo pending na itarudi baada ya siku kadhaa, mpaka sasa hawajakataa kuwa hela haipo kwao.

Wangekataa mapema, mlalamikaji angetafuta namna nyingine ya kupata fedha yake.

Kwa hiyo awe ameibiwa na wanaijeria, wachina nk bado Voda wanawajibika kumlipa kwa kuwa wamekubali na kumuaminisha mlalamikaji kuwa kosa lipo kwao na fedha yake watamrejeshea.

Kwa hilo hawachomoki
Hakunaga hela inayoganda hewani kweny hio miamala, Imepewa tu jina la mpesa master card lakini mwenye nayo ni benki inaitwa banc abc. Kwa ambao tuna uzoefu na hizi ishu kwa miaka mingi tunajua tatizo lipo kwa alienunua hivyo vitu.

Mzoefu hawezi nunua vitu kwa njia kavu kadi ichajiwe direct lazima atymie ngao ya paypal,

Hakuna pesa pending hapo, matapeli washaichomoa

Nampa pole aliefanya muamala siku nyingine ahakikisha anatumia paypal, Pia nina wasi wasi kwanini haweki wazi software aliyotaka knunua na website yake, Yawezekana kabisa haio software ilikua wameaminisha watu inatengeneza pesa bila jasho ukiinunua 😁😁 ndio njia wanazotumiaga kunasa wengu
 
Card zangu zote za crdb MasterCard na VisaCard zinagoma zinataka nijaze securecard nazo crdb huduma kwa wateja hawaelewi naambiwaga utapokea sms yenye code ndio hakuna lazaidi....Yan ile kwenda kwenye tawi pia kwangu ni changamoto.View attachment 1523423View attachment 1523422
Hao crdb wana mlolongo mrefu sana, kuna kipindi mwaka 2014 nilizungushwa miezi mingi sana mpaka mwaka 2015 hamna kitu zaidi ya kwenda tu ofisini kwao na kusainishwa fomu kila nikienda.

Cha kufanya nenda equity bank au bank abc unatengenezewa kadi ndani ya dakika kumu na utaweza kufanya miamala mtandaoni kwa haraka na usalalama...
 
Hivi who told you Mpesa Mastercard ni salama? Nyie watu, hivi ukipata tatizo unajua bank ya Mpesa Mastercard iko wapi? Sbb tatizo la fedha ukipata unaenda bank na unapata utatuzi, sasa kuwa na Mastercard wakati hujui bank iko wapi ni kosa sana, au wengi mlijua Mastercard ni kama Mpesa au tigopesa ya kawaida tu? Muwe na Mastercard za bank plz.. Mtalizwa sana msipokuwa makini.
Tofauti ya bank na mitandao ya simu ni aina ya kadi na matumizi yake tu.Bank inatoa Solid Card ambayo unaweza kuitumia mtandaoni, ATM na kwenye mashine zingine zakuchanja card.Mitandao ya simu inatoa virtual card ambayo huegemea matumizi ya mtandaoni tu online.Upatapo tatizo utaenda kwenye ofisi zao kumbuka hata kuhamisha miamala ilikuwa ni dhughuli za bank tu now simu ndio njia mbadala...Tatizo la hawa mitandao ya simu Huduma kwa wateja hawajawaweka watu wa Kibank wanaojua mambo hayo ya MasterCard VisaCard.Mtu aliyesomea mambo ya telecommunication ndio huyo anatakiwa atatue mambo za Bank hili ni tatizo....Pia hii mambo ya online Shopping/payment hata hao Bank hawana wataalamu wa kutosha yan mhudumu anakuuliza PayPal ni nini.Hili suala la ni geni kwa watoa huduma taasisi na kampuni zote tz pia ni geni kwa wateja wao ambalo ndio huishia kwa mteja kuwa MHANGA.
 
Back
Top Bottom