Mpesa Safaricom- Vodacom,

Nairoberry

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Posts
932
Reaction score
525
Juzi nilikuwa namtumia rafiki yangu hela uko Tz na mpesa bahati mbaya nikakosea nambari moja ya mwisho,nikawapigia safaricom wanirejeshee hiyo hela kwangu,haya sasa safaricom hawawezi nirejeshea hela manake uyo mteja wa vodacom uko tanzania asha toa hela kitamboo.. ni njia gani mtu uko Tz utumia kukabiliana na hawa wezi, cha kushangaza aliye toa ni mwanamke na sasa kazima simu yake kitambo.
 
Kwakuwa nyie ni mabingwa wa kuongea KIMALKIA, ungeandika tu kidhungu kuliko kuongea lugha vunjika.

Hata hivyo nimekuelewa.....
 
Kwa Tanzania ukiona umekosea na haphapo unapiga wanaizuia

Mimi nami nimekuja Kenya Leo ,so nataka nitume pesa flani Tanzania kwa mpesa nitakuwa makini sana

Ila safari com inabidi wawe makini pia waweke option ya jina la unayemtumia kabla ya Ku confirm
 
pole sana kaka!
 
kweli kabisa, wanafaa pia hela ikitumwa angalau ichukue ata dakika 30 kabla kumfikia anayepokea. kuwa makini sana ukituma hela, nimejifunza sasa. nimepoteza laki kadhaa za Tz.
 
Safaricom wanaeka detail zote za mtu ukimtumia hela. Kenya huwezi nunua line rejareja bila I.D au passport. PIA ukimtumia mtu pesa kuna prompt ya delay ya kitu sekunde ishirini za kusimamisha shughuli yenyewe kama umekosea. Ukishindwa na hayo yote pesa ziende unatuma hiyo text ya Mpesa kwa 456 hapo hata pesa ziwe zimeingia kwenye simu ya mtu hawezi zitoa. Zinakuwa freezed kwa simu.
 
kweli kabisa, wanafaa pia hela ikitumwa angalau ichukue ata dakika 30 kabla kumfikia anayepokea. kuwa makini sana ukituma hela, nimejifunza sasa. nimepoteza laki kadhaa za Tz.
Dk.30 seriously? Mtu amekaa anasubiria pesa kwa wakala au alipie huduma hospitali then aisubirie pesa kwa 30minutes???
 
Pole sana huku Tanzania saiv hali ni ngumu kuwa makini na hela zako.
Kawaida ukigundua umekosea unapiga simu mara moja kwa Vodacom wana reverse transaction.
 
Dk.30 seriously? Mtu amekaa anasubiria pesa kwa wakala au alipie huduma hospitali then aisubirie pesa kwa 30minutes???
jemeni ukipewa cheki si unasubiri ata siku 5 kwa benki, mbona mtu hawezi subiri dakika 30 pekee??
 
nafikiria sana ili jambo la "instant money" tunabidi tuliangazie tena, voda/safcom wanabidi wafikirie sana....maoni yangu lakini.
 
jemeni ukipewa cheki si unasubiri ata siku 5 kwa benki, mbona mtu hawezi subiri dakika 30 pekee??
Electronic money tunategemea iwe mbadala wa hayo makaratasi sio kuanza kupotezeana muda tena cha msingi wawe makini kurejesha pesa za watu pindi zinapohitajika kwakua zimetumwa kimakosa.
 
Kwani nyie mpesa yenu haiwapei jina la unakotuma, to confirm before hujatuma.
 
next time ukitongoza mrembo mitandaoni,muulize hata angalau jina lake halisi lililoko kwenye kitambulisho kabla ya kumtumia tikiti. kuwa careful next time
 
next time ukitongoza mrembo mitandaoni,muulize hata angalau jina lake halisi lililoko kwenye kitambulisho kabla ya kumtumia tikiti. kuwa careful next time
Hahaha. 😀 Jamaa yetu kapoteza hela bana acha mzaha. Ila p#ssy ina nguvu sana zaidi ya sheitwan! 🙂
 
next time ukitongoza mrembo mitandaoni,muulize hata angalau jina lake halisi lililoko kwenye kitambulisho kabla ya kumtumia tikiti. kuwa careful next time
acha upumba bana, hizi ni hela nilikuwa namrejeshea rafiki yangu alikuwa ananidai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…