Leo asubuhi nilikuwa nasindikiza wageni kuelekea bara (mkoani). Nikiwa ndani ya stendi ya mabasi ya Ubungo kiasi cha saa 11:15 (kumi na moja na robo alfajiri) nilikumbana na mpiga debe wa kichina akiniaambia 'lipo basi la Obama hapa linakwenda Mbeya hadi Tunduma" (lafudhi ya kihuuhii). Sikuamini ilibidi nisimame nihakikishe anayoyasema.
Baada ya kudadisi nikaambia hao wachina (walikuwa watatu) unaowaona wanamiliki hilo basi (pembeni yetu) lenye rangi za bendera ya USA linalofanya safari zake Dar-Tunduma.
Jamani, hivi kweli mchina ananunua basi na anaajiri mpiga debe mchina, mkata tiketi mchina, vibari vya kufanya uhuni huu wanapata wapi?
Kweli mtanzania unaweza kwenda nchi za watu ukafanya hivi?