Uchaguzi 2020 Mpiga kura aliyehama mahali alipojiandikisha atatakiwa kusafiri kwenda kituoni alipojiandikisha ili aweze kupiga kura

Uchaguzi 2020 Mpiga kura aliyehama mahali alipojiandikisha atatakiwa kusafiri kwenda kituoni alipojiandikisha ili aweze kupiga kura

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Jaji Msataafu Thomas Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amesema kuwa mpiga kura aliyehama sehemu aliyojiandikisha kupiga kura atatakiwa kusafiri kwa muda ili apate haki ya kupiga kura kinyume na hapo hatoweza kupiga kura

====


 
Jaji Mihayo mjumbe wa Tume ya uchaguzi asema utapiga kura ulipojiandikisha kama umehama panda basi ukapige ulikojiandikisha. Mwisho wa kunukuu.

Mfano ulikojiandikisha ukapata kitambulisho cha kupiga kura ni Kilimanjaro unatakiwa upande basi la Kilimanjaro express ukapige kura huko.Kama ulijiandikisha kinondoni ukahamia Ilala itabidi upande daladala ukapige kura Kinondoni.
 
Mimi nitajiandikisha hapa Dar maana nilihamisha taarifa kura yangu kwa jpm ni kitu cha msingi sana mimi na familia yangu
 
Uchaguzi Afrika hauna tofauti na ufujaji wa Raslimali na Muda ,wizi / vitisho/ Uongo uonevu/ uvunjwaji wa Sheria na mengine ya kufanana na hayo.Binadamu anapo fika mwisho huamua lolote na hapo ndipo machafuko hutokea na kupelekea waliomo na wasio kuwepo kuwekwa ktk kapu moja la Athari..
 
Utopolo kwenye Ubora wao
uichoelewa hapo nini? Mfano mdogo tu wanafunzi wengi wa vyuo na shule za kilimanjaro 2015 walijiandikisha na kupiga kura kilimanjaro wakapiha kura kule sasa wengi wamehamia mikoa mingine.

Pia kuna wafanyakazi waliokuwa Dar wamehamia Dodoma.

kuna wafugaji wa kimasai nk wanaohama hama.

kuna wanavyuo waliopo sasa wengi walijiandikisha kwingine tofauti na wanakosoma sasa nk
 
Jaji Mihayo mjumbe wa Tume ya uchaguzi asema utapiga kura ulipojiandikisha kama umehama panda basi ukapige ulikojiandikisha.Mwisho wa kunukuu...

Huyu naye yupo tu NEC kulinda mambo ya ukanda
 
Na yule mgombea anaye lala na miwani kule Mbeya,na yeye atapanda basi kwenda Dar akapige kura alikojiandikisha?
 
Hiyo ni kwa nafasi zote? au udiwani na ubunge maana hilo ndiyo hufanyika hivyo ila kwa urais unaweza kupiga kama ulihama eneo lako kama sikosei
 
Huo ni utaratibu mzuri sana. Hongera tume kwa maamuzi sahihi, wakati sahihi na muda sahihi.
 
Jaji Mihayo mjumbe wa Tume ya uchaguzi asema utapiga kura ulipojiandikisha kama umehama panda basi ukapige ulikojiandikisha.Mwisho wa kunukuu....
Hakika ccm inambinu 1000,hiyo ni moja tu,bado 999[emoji23][emoji23][emoji23],watatosha wanaotaka kushindana na hii taasisi kubwa na bora barani afrika
 
Wazanzibari watoka bara kwenda kupiga kura zanzibar safari hii hakuna
 
Ila Jane upo kwa ajili ya kukera tu watu, au?
😆😆😆😆.
Ila Ni vyema ukajua lolote litakalotokea kwa kumdhulunu haki za watu. Litakuathir na wewe au watu wako wa Karibu.

Tusiwabane Sana watu Kuna mda huwa wanachoka. Sio vyema watu waanze kuchoka. Mambo ya kufanya watu wachoke na kuanza kufanya vurugu hatuyataki. Waachieni tu watu wapate haki yako.

Kwa nini tusipende amani?
Hata vitu hivi vidogo kwani katiba si ipo wazi. Kila mtu anahaki yankumchagua kiongozi wake. Ama Kuna ajenda gani. Kwani Raisi wa Tz si wa watu wote?
Au Ni Mimi sijaelewa lililosemwa?
Huo ni utaratibu mzuri sana. Hongera tume kwa maamuzi sahihi, wakati sahihi, na muda sahihi.
 
Back
Top Bottom