Mpiga picha akamatwa Kenya akipiga picha shamba la Rais Kenyatta .

Synod

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
4,143
Reaction score
4,180
Mpiga picha mmoja wa shirika la kimataifa amekamatwa na kushtakiwa mahakamani Jijini Nairobi, baada ya 'kuzuru shamba la Kenyatta' bila idhini.

Shirika la habari la AFP, limesema kwamba, mpiga picha wake mkuu wa Afrika Mashariki, amefikishwa Jumatatu mahakamani nchini Kenya na kushtakiwa kwa kosa la kuingia kwenye shamba linalomilikiwa na familia ya Rais Uhuru Kenyatta.

Mpiga picha huyo raia wa Japan Yasuyoshi Chiba, mwenye umri wa miaka 46, alikamatwa siku ya Ijumaa kwenye shamba la kampuni ya maziwa ya Brookside dairy, inayomilikiwa na familia ya Rais wa kwanza wa Kenya na wa sasa Bw. Uhuru Kenyatta.

Alikuwa amekwenda huko kupiga picha ya nembo ya kampuni hiyo ya maziwa, baada ya muungano wa upinzani nchini humo-NASA, kutoa wito wa kususiwa kwa bidhaa zote za vigogogo wakuu wa chama tawala cha Jubilee zikiwemo bidhaa za Brookside, kufuatia kumalizika kwa uchaguzi mkuu enye utata wa Urais.

Mpiga picha akamatwa Kenya akipiga picha shamba la Rais Kenyatta
 
Kuzuru? shambulio la kuzuru mwili... Rais kuzuru nchi ya uganda wiki hii.... kuzuru? kuzuru? kuzuru?
 
shambulio la kuzuru shamba... kazuru shamba... zuru...?
 
zuru? kazuru...? Dr Shika kazuru mnada wa majengo ya Lugumi...
 
Kuzuru ni kutembelea au visit kwa kiingereza, neno dhuru ndio linamaanisha kuumiza.
hapa sasa nimepata kuelewa zaidi... maana sisi ni waswahili lakini bado tuna endelea kujifunza kiswahili na hatupati maksi 100% ktk mtihani husika
 
Kupiga picha ni kosa? Or taking photos needs a license for journalists in Kenya?
 
Kuzuru? shambulio la kuzuru mwili... Rais kuzuru nchi ya uganda wiki hii.... kuzuru? kuzuru? kuzuru?
mkuu wewe naye kiswahili chenga kweli yaani, sasa hapo angetumia neno gani?

kuzuru = kutembelea (visit)
kudhuru = shambulia nk.

sasa hicho alichotumia 'zuru' ndo sahihi.
 
Je alifuata utaratibu? Hivi kuwa mwandishi wa habari ni kwenda kwenye maeneo ya watu na kupigapiga picha tu bila vibali, kwenye ulimwengu huu unaotawaliwa na ujasusi na ushushushu hatua zilizochukuliwa zilikuwa sahihi.
 
Hivi huyo mwandishi hakujua kwamba Kenya ni baba wa demokrasia, kwanini anataka kutuharibia baba wa demokrasia?, hawa wazungu sio bure, wanaionea wivu demokrasia ya East Africa
 
Kupiga picha ni kosa? Or taking photos needs a license for journalists in Kenya?
Kuna maeneo mengine ambayo hayaruhusiwi kupigwa picha/kupiga picha hata Tanzania yapo hata ulaya yapo... Nenda Urus au Israel upige picha ovyo ovyo kama hujapigwa risasi...
 
Kuna maeneo mengine ambayo hayaruhusiwi kupigwa picha/kupiga picha hata Tanzania yapo hata ulaya yapo... Nenda Urus au Israel upige picha ovyo ovyo kama hujapigwa risasi...
Korea kaskazini unapigwa bomu
 
Kupiga picha ni kosa? Or taking photos needs a license for journalists in Kenya?
Ndio ni kosa kupiga picha shamba au uwanja bila idhini ya mmiliki tena wanaweka na mabango kabsa
Huyo mjapani kesi anayo yakujibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…