Mpigie makofi mjinga

sili SG

Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
22
Reaction score
26
MJINGA
Mjinga akimaliza la saba anaanza biashara ya mkaa halafu atachoma mahindi halafu atauza miwa, atalima viazi.
Baada ya miaka miwili atafungua duka la nguo atasafiri kwenda Dar kufunga mzigo....
Kila hela atakayopata ataitunza kwa nidhamu kuu.
Matokeo yake meneja wa benki atavutiwa na nidhamu hii atamuita na atamuuliza kama atapenda mkopo na malengo yake.
Mjinga atajieleza wazi kua akikopeshwa atapanua duka lake, atainunua nyumba aliyopanga duka na atanunua fuso la kusomba mzigo wake badala ya kukopa kwani hela anayotumia kulipa kodi na kukodi mafuso ni mara nne ya hela ya kulipa mkopo.
Baada ya miaka miwili mjinga kamaliza deni na kachukua mkopo mwingine kanunua mabasi manne ya kwenda Dar Mbeya Songea na watu watasema ni mchawi kaua wazazi wake wakati walikufa wakiwa na umri wa miaka kati ya 85 - 99
MJANJA WA MJINI
Huyu atapiga mesheni town na kufanikiwa kuchukua mkopo mkubwa huku akiweka hati ya nyumba ya urithi kama dhamana....
Akiishapata mkopo atanunua BMW X6 ya kupigia misele, mchepuko vogue range na ataitisha bonge la pati kujipongeza kupata mkopo....
Atatesa sana mjini kila kona .
Hela itakapokaribia kuisha atainvest kwenye biashara ya madini atauziwa vichupa akiambiwa almasi.....
Baada ya miaka miwili atafilisiwa na nyumba itapigwa mnada na atasema karogwa
MSOMI
Huyu atafanya kazi weee lakini hakuna savings kwani kila anachoingiza kina matumizi yake kisomi.....
Atakapochoka kuteswa mjini atachukua mkopo......
Atanunua gari ya familia....
Ataezeka nyumba yake
Atabaki na deni la kulipa mpaka amalize huku akiandamwa na barua za default..
Huyu hana wa kumlaumu ila ujuaji wake...
Wakuu
Tumheshimu mjinga
Ana nidhamu ya hela na kipaji cha biashara.
Kupata hela sio kazi bali kuitunza na kuiheshimu.
 
hii kali umetisha mkuu
 
Umeandika kitu poa sana ingawa umerahisisha sana namna MJINGA alivyotoboa kirahisi rahisi,lakina kuna ujumbe mzuri.
 
Maisha haya jawa kirahisi rahisi kama unavo simulia.......wasinge soma wengi bali la saba ingelikua tosha kwa kila mtanzania...asante kwa hadith nzuri
 
Mtoa mada umeeleweka sana japo kuna watu wanadhani ulivyoqndika ndiyo maisha yapo rahisi hivo
 
Duh mkuu umewaza nini mzee?Tanzania hapa kuna wajinga wengi sana wamewaacha wasomi mbali.

Huyu meshen town hana tabu sana maana yeye mambo yake mengi anayafanya kiujanja ujanja shida ni huyu ofisa mf:wa bank mtu kabisa anamshirikisha wazo lake la kupata pesa yeye na elimu yake yote badala aibe japo 40% ya wazo lile akalijaribu anampa pesa yeye anarudi kukaa kwenye kiti akisubiri siku huyu mjinga a-fail akamfurushe huko aliko.
 
Maisha haya jawa kirahisi rahisi kama unavo simulia.......wasinge soma wengi bali la saba ingelikua tosha kwa kila mtanzania...asante kwa hadith nzuri

Sijui kama nitakuwa nimekuelewa vizuri ila najaribu tu kuona wazo lako lipo sawa sawa?nikuulize mkuu,unadhani kwa Tanzania ya sasa ni muhimu sana kila mtu kupigana kusoma hadi kufikia kupata vyeti kisha kurudi mtaani kulikowa hakuna kazi kukaa akisubiri kulishwa na wazazi wake kesho yake akiwa haijui?

NB;Simaanishi kupinga kusoma naomba nisieleweke vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…