Tetesi: Mpina agonga hodi ACT Wazalendo na yupo tayari kugombea urais

Saa za aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutua katika Chama cha ACT-Wazalendo zinahesabika, baada ya kiongozi huyo kubisha hodi huku akieleza kuwa yuko tayari kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais, Jambo TV imedokezwa.

Uamuzi huo wa Mpina, ambaye ameondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa na CCM kuwania Ubunge wa Kisesa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni misimamo yake ya kuikosoa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu, unatajwa kuwagawa viongozi wa ACT-Wazalendo. Baadhi yao wanahofia misimamo hiyo, huku wengine wakieleza kuwa anapaswa kupewa jukwaa hilo.

Katikati ya mjadala huo juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, inadaiwa kumeibuka upinzani mkubwa ndani ya chama, huku viongozi wakionesha kutokuwa tayari kumsimamisha kwenye nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa mbunge huyo wa zamani haendani na aina ya siasa ya chama hicho.

Mpina anasifika kwa siasa ngumu zenye kujikita katika kuikosoa serikali kwa ukali, tofauti na utamaduni wa ACT-Wazalendo unaosifika kwa kufanya siasa za masuala na ujenzi wa hoja.

Taarifa za Mpina kujiunga na ACT-Wazalendo zimechagizwa zaidi na taarifa za kuongezwa muda kwa watia nia wa nafasi ya ubunge ndani ya chama hicho. Katibu Mkuu, Ado Shaibu, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza juu ya chama hicho kuongeza muda, pasipo kufafanua zaidi ni katika nafasi gani.

Wakati kukiwa na mvutano juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, baadhi ya wanachama waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika chama na Baraza Kivuli la Mawaziri, akiwemo Mwalimu Philbert Macheyeki, wamesikika wakieleza kuwa Mpina ni turufu kubwa ya kukijenga chama hicho na kukipatia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Macheyeki amesema kuwa hadi sasa chama hicho kimewatangaza watia nia wawili katika nafasi ya urais—Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Aroon Kalikawe—na kwamba ujio wa Mpina utakuwa ni chachu zaidi kwa ajili ya mafanikio ya chama chao.

“Luhaga Mpina amejizolea sifa za kuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Awamu ya Sita na kinara wa kuibua kashfa mbalimbali nzito za ufisadi...
Asipoteze muda wake, hivi hajui kama ACT ni chama cha mfukoni cha CCM.
 
Inawezekana ni mkakati wa CCM kutengeneza upinzani utakaoleta hamasa na msisimko angalau kidogo kwenye uchaguzi.
 
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
😂 Kazi iendelee... ya kufungia mikutano ya siasa, ya kugawa vyeo kwa wakwe na watoto, ya kupamba majukwaa huku gharama ya maisha zinapaa!

Kazi iendelee… ya "Mama kuwafikia" kwa mkono wa dola polisi, usalama wa taifa na msajili wakipiga marufuku upinzani.

Huu si utumishi uliotukuka, ni utumishi wa kufukuza demokrasia hadi porini!
Kama kugusa maisha ya wanyonge ni kuwaumiza kwa kodi na propaganda, basi kazi kweli kweli! 🙃

#MamaWaMaamuziMazitoYaKuminyaDemokrasia
#FamiliaFirstWananchiLater
 
Saa za aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Luhaga Mpina wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutua katika Chama cha ACT-Wazalendo zinahesabika, baada ya kiongozi huyo kubisha hodi huku akieleza kuwa yuko tayari kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais, Jambo TV imedokezwa.

Uamuzi huo wa Mpina, ambaye ameondolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa na CCM kuwania Ubunge wa Kisesa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni misimamo yake ya kuikosoa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu, unatajwa kuwagawa viongozi wa ACT-Wazalendo. Baadhi yao wanahofia misimamo hiyo, huku wengine wakieleza kuwa anapaswa kupewa jukwaa hilo.

Katikati ya mjadala huo juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, inadaiwa kumeibuka upinzani mkubwa ndani ya chama, huku viongozi wakionesha kutokuwa tayari kumsimamisha kwenye nafasi hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa mbunge huyo wa zamani haendani na aina ya siasa ya chama hicho.

Mpina anasifika kwa siasa ngumu zenye kujikita katika kuikosoa serikali kwa ukali, tofauti na utamaduni wa ACT-Wazalendo unaosifika kwa kufanya siasa za masuala na ujenzi wa hoja.

Taarifa za Mpina kujiunga na ACT-Wazalendo zimechagizwa zaidi na taarifa za kuongezwa muda kwa watia nia wa nafasi ya ubunge ndani ya chama hicho. Katibu Mkuu, Ado Shaibu, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza juu ya chama hicho kuongeza muda, pasipo kufafanua zaidi ni katika nafasi gani.

Wakati kukiwa na mvutano juu ya ujio wa Mpina ndani ya ACT-Wazalendo, baadhi ya wanachama waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika chama na Baraza Kivuli la Mawaziri, akiwemo Mwalimu Philbert Macheyeki, wamesikika wakieleza kuwa Mpina ni turufu kubwa ya kukijenga chama hicho na kukipatia kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Macheyeki amesema kuwa hadi sasa chama hicho kimewatangaza watia nia wawili katika nafasi ya urais—Kiongozi wa Chama Dorothy Semu na Aroon Kalikawe—na kwamba ujio wa Mpina utakuwa ni chachu zaidi kwa ajili ya mafanikio ya chama chao.

“Luhaga Mpina amejizolea sifa za kuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Awamu ya Sita na kinara wa kuibua kashfa mbalimbali nzito za ufisadi...
Atatangazwa na nani hata akishinda!?
Kura zitalindwa na Polisi.✍️📌
 
Mnabadili lini mgombea bwana chawa mana Pole Pole kawakaba wanakutuma wewe unakuja kubwabwaja kama umekatwa kichwa na Chai Jaba kapigwa jab leo ile inaitwa kelebu hatapanua kinywa tena mana hajui lolote kwenye huu mchezo
Kunguni wa mama hao
 
Sio mpina, ni wananchi ndo wanamtaka… sema nyinyi hamumtaki kwa sababu ana akili, mnataka wasio na akili
 
Kila mtu afanye anachoona kinamfaa.

Au umeumia kisa hajaja kwenu chadema na mlimshangilia kuwa ni mwanamapinduzi wa kweli baada ya kuongea mliyotaka kuyasikia?
 
Back
Top Bottom