Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Nakiri kupokea barua yako yenye Kumb. Na. SAE. 3511527/L ya tarehe 21 Januari 2026, ikinitaka kufika kukutana na Tume tarehe 31 Januari 2026, kuanzia saa 2:00 mchana hadi saa 9:00 alasiri katika Ukumbi wa Manyara, Benki Kuu – Dar es Salaam.
Ninakushukuru kwa ushirikiano.
- Utakumbuka kuwa mnamo tarehe 18 Novemba 2025, Chama changu cha ACT Wazalendo kilitoa taarifa kwa umma kwamba kinapinga na kinakataa kabisa Tume iliyotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuchunguza matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025 na siku zinazofuata.
- Chama cha ACT Wazalendo kiliweka wazi kwamba hakitashiriki kwa namna yoyote ile katika uchunguzi utakaofanywa na Tume hii. Hatutatoa ushahidi wala kutoa ushirikiano wowote, kwani tunatambua kuwa ni chombo kisicho huru na kitakachotegemea maagizo ya Serikali.
- Hata nilipozungumza na vyombo vya habari tarehe 6 Desemba 2025, niliunga mkono msimamo wa Chama kwamba Tume hiyo siyo huru na imeundwa bila kuzingatia kanuni na taratibu za Usuluhishi wa Migogoro (Conflict Resolution Strategies and Guidelines).
- Hivyo basi, kwa heshima kubwa, nakujulisha kwamba sitaweza kuhudhuria wito huo kwa ajili ya majadiliano.
- Pamoja na barua hii, nimeambatisha nakala ya Tamko la Chama cha ACT Wazalendo.
Ninakushukuru kwa ushirikiano.
