Mpina anarudia makosa yale yale ya kina Mrema, Membe na Lowassa

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
photo_2025-08-05_14-37-46.jpg

Aliyekuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina sasa amehamia CCM na anatajwa kuwa mgombea uraia s wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ilikuwa wazi kwamba Mpina asingepitishwa kwenye kura za maoni za CCM licha ya wananchi wa jimbo lake kumpenda. Hiyo ni kutokana na msigano wake na viongozi wa chama hicho, tangu mawaziri, Rais Samia Suluhu Hassan na hata viongozi wa chama hicho ngazi ya Mkoa wa Simiyu.

Licha ya kwamba Bunge la 12 lilikuwa limejaza wabunge wa CCM kwa asilimia 99, lakini Mpina ndiye aliyekuwa mbunge pekee aliyekuwa akiikosoa Serikali waziwazi bungeni, huku wabunge wengine wakiishia kuuliza maswali ya kawaida na kupiga meza.

Hata Rais Samia alipotembelea Mkoa wa Simiyu Juni mwaka huu, alisema Rais Samia amjibu Mpina, asema anarukaruka na kujitafutia umaarufu. Alisema pia Mpina anafaa kuwa Mbunge wa Taifa, kauli iliyotafsiriwa kuwa huenda Mpina akateuliwa kuwa Mbunge na jimbo akatafutiwa mtu mwingine.

Hata hivyo, Mpina hajawa na subira baada ya kutemwa kwenye mchujo wa awali wa CCM. Wananchi jimboni wanamlilia, kumbe yeye yuko Dar es Salaam anajiunga na ACT Wazalendo.

Kwa ACT Wazalendo, leo ni sherehe kubwa, lakini kwa wananchi wa Kisesa, bado haijajulikana watachukuliaje. Huenda wakamuunga mkono au wakatafuta mwingine wa kumuunga mkono kwenye ubunge.

Kosa la Mpina

Mpina sio mwanasiasa wa kwanza kuhama CCM na kwenda upinzani, hasa pale wanapokosa nafasi za kugombea. Mfano mzuri ni aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, ambaye mwaka 2015, baada ya jina lake kukatwa kwenye mchakatio wa urais, alihamia CHADEMA na kupewa nafasi ya kugombea urais.

Kwa kweli Lowassa alikuwa tishio kwa CCM alipoondoka, kwani aliondoka na kundi kubwa ambalo liliiwezesha CHADEMA kupata wabunge zaidi ya 40 wa kuchaguziliwa na Zaidi ya 30 wa viti maalum. Aliviwezesha vyama vingine vya upinzani vilivyokuwa kwenye Muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupata pia wabunge.

Licha ya kutoshinda urais, Lowassa alifanikiwa kuzishusha kura za urais wa John Magufuli hadi asilimia 58, huku yeye akipata Zaidi ya asilimia 39.

Lakini baada ya uchaguzi ule, Rais Magufuli aliweka mazingira magumu sana ya kidemokrasia ambayo imsingi ndiyo yanaugharimu mfumo wa siasa nchini mpaka leo. Ilipofika mwaka 2019, Lowassa akashindwa kuvumilia, akajirudia zake CCM.

Hivyo hivyo, yalimkuta Augustine Mrema, aliyefungua pazia la kuondoka CCM na kugombea urais mwaka 1995. Kweli Mrema alikuwa na nguvu ya kukipaisha chama cha NCCR Mageuzi, lakini yote yaliyofuata baada ya uchaguzi huo, kila mtu anajua.

NCCR Mageuzi mpaka leo imeshindwa kurudi kwenye ukali wake wa mwanzo na Mrema mwenyewe aliyetimkia TLP, alipoteza umaarufu wake.

Hivyo hivyo pia kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bernard Membe, ambaye baada ya kufukuzwa CCM mwaka 2020, alikimbilia ACT Wazalendo na kugombea urais.

Kwa hiyo ACT Wazalendo sio wageni wa kupokea vigogo wa CCM, wanajua tamu na chungu ya kupokea vigogo hawa. Utamu wake ni wa muda tu, halafu ukiisha yanaanza machungu.

Kwa hiyo, muda mfupi tu, Membe akaanza kuchoka katikati ya kipindi cha kampeni na hata ushiriki wake ukadorora, kabala hata ya kuanza kulalamikia figisu za CCM.

Kwa hiyo utaona waliomtangulia Mpina kwenda upinzani wote kwanza, walifanya kosa la kufanya siasa za hasira, halafu hata hiyo hasira yenyewe walishindwa kuilinda ijenge uhalali wanapokuwakwenye upinzani. Ndio maana karibu wote waliishia kufilisika kisiasa.

Sasa Mpina naye anafuata nyayo zilezile za kina Mrema, Membe na Lowassa, ataweza kugombea urais na CCM? Kwanza ieleweke kwamba unapofika uchaguzi, kwa CCM unaoshindana ni mfumo, sio umaarufu wa mtu.

Ndiyo maana wapo wanaoona kuna haja ya kuwa na mabadiliko kabla ya uchaguzi, kwa sababu bila hayo mabadiliko, hata wapinzani wasimamishe malaika kutoka mbinguni, hawezi kuishinda CCM.

Bila kubadilisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano, bila kupata mfumo bora wa uchaguzi, bila kupata Tume Huru ya uchaguzi, bila kuviweka huru vyombo vya ulinzi na usalama, ni ndoto kuishinda CCM.

ACT Wazalendo wanakiri haja ya kuwepo kwa mabadiliko, lakini wamesema watashiriki uchaguzi uchaguzi huku wakidai hayo mabadiliko, jambo linaloibua maswali mengi: kwamba watapataje mabadiliko wakati tayari mfumo huo unaolalamikiwa umeshajiweka tayari kutoa malalamiko ambayo hayatawafurahisha? Watatumia mbinu gani kubadilisha?

Kwa hiyo Mpina anaposema anagombea urais, ajue, hashindani na Rais Samia, ajue anashindana na mfumo mzima unaolalamikiwa. Je, ameagana na nyonga? Wengine wameshauri kwamba angalau angeishia kugombea tu ubunge, pengine angelinda lile jimbo na akaendeleza mashambulizi yake kule bungeni.

Lakini kuutaka urais kwa sasa litakuwa ni kosa la kimkakati, sio kwake tu, bali pia kwa ACT Wazalendo. Atakuwa anarudia makossa yale yale ya kina Lowassa, Membe na Mrema. Atatumia kambi ya upinzani kutema nyongo zake wakati huu wa uchaguzi, lakini uchaguzi ukiisha, ataweza kuvumilia njaa kali ya upinzani?
 
View attachment 3432362

Ulitaka afanyeje sasa wakati chama kimetekwa na wahuni
 
aisee bora angeenda CDM tu kuongeza nguvu na kupambania NRNE.
ACT ya ZZK ni yaleyale tu maana ZZK hawezi kusimamia harakati zozote dhidi ya mabosi wake.

ndani ya mitaa ya Kabul, Afghanistan.
 
Inahuzunisha sana
Ila ndio mambo ya siasa yalivyo
 
Aliyekuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina sasa amehamia CCM na anatajwa kuwa mgombea uraia s wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hana washauri wazuri. Urais aachan nao, haendi popote. Agombee Ubunge amkabiri samia bungeni
 
Uchambuzi safi kabisa unaoweza kuwa nuru kwa wanasiasa vijana. Watanzania waliowengi wanaunga mkono Chama Cha Mapinduzi, na waliosalia hawapo tayari kulipa gharama ya mabadiliko. For this very reason personal political popularity may not help
 
Kashapoteana huyo, ningemuona wa maana angedai mabadiliko coz naye muhanga wa kunyimwa haki ya kuchaguliwa..!!
 
Kama tungekuwa na tume huru Lazima mpina angeshinda urais mapema kabisa.Lakini Kwa Sasa itakuwa ngumu maana wajumbe wote wa hiyo NEC japo wahuni wa Samia wanaiita INEC wote wanateuliwa na mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni mgombea urais.
 
Bila kubadilisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano, bila kupata mfumo bora wa uchaguzi, bila kupata Tume Huru ya uchaguzi, bila kuviweka huru vyombo vya ulinzi na usalama, ni ndoto kuishinda CCM.
huu ndio ukweli
 
Back
Top Bottom