Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Luhanga Mpina, ameibuka na kutoa tuhuma nzito dhidi ya Serikali, vyombo vya dola na taasisi za uchaguzi, akidai kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, mauaji na uonevu uliodaiwa kutokea wakati wa uchaguzi na maandamano yaliyofuatia.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mpina amesema matukio ya vurugu na vifo vya raia vinavyodaiwa kutokea siku ya uchaguzi "haviwezi kufumbiwa macho", na kuongeza kuwa dunia haiwezi kunyamazishwa na vitisho vinavyotokana na kile alichokiita maslahi ya watu wachache.
Katika hatua nyingine, Mpina aliishukuru jumuiya ya kimataifa, mashirika ya haki za binadamu na vyombo vya habari vya kimataifa kwa kulaani kile alichokiita ukiukwaji wa haki za binadamu, huku akizipongeza balozi 17 zilizotoa taarifa zao kuhusu matukio hayo.
Amedai kuwa familia nyingi zimekosa miili ya ndugu zao na wengine kupotea bila maelezo, akisema hatua hizo zinapaswa kuchunguzwa na vyombo huru.
Mpina amesema shauri lake la kupinga kuenguliwa kugombea hakujapewa mwelekeo na Mahakama Kuu, jambo alilolieleza kuwa limewafanya wananchi kupoteza imani na chombo hicho.
"Rufaa yangu ilitelekezwa. Uchaguzi umefanyika wakati shauri langu liko mahakamani. Je, kama angekuwa mgombea wa CCM ndiyo angeachwa hivyo?" amehoji.
Amesema sasa anatarajia kupeleka shauri hilo Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) ili kupata haki anayoamini alinyimwa.
Mpina amedai kuwa vurugu zilizodaiwa kutokea siku ya uchaguzi na maandamano zilizoripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini zinaonyesha "kiasi ambacho Serikali imeshindwa kulinda haki za msingi za wananchi".
Alisema matumizi ya nguvu na ripoti za wananchi kujeruhiwa na wengine kupoteza maisha ni mambo ambayo "yanadhoofisha taswira ya nchi na misingi ya demokrasia."
Chanzo: Nipashe