GE2025 Mpina: Bungeni Nimefukuzwa Kwa Kutetea Wananchi, wanataka Wabunge Wagonga Meza tu!

GE2025 Mpina: Bungeni Nimefukuzwa Kwa Kutetea Wananchi, wanataka Wabunge Wagonga Meza tu!

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema anaifahamu kwa kina mizigo ya Watanzania, ikiwemo changamoto za kilimo, ufugaji, biashara, uchimbaji madini, bodaboda na hata suala la kufungiwa makanisa, na kusisitiza kuwa amedhamiria kuyatatua mara atakapochaguliwa.

Akizungumza na wananchi wa Katoro, Mkoani Geita leo Agosti 20, 2025 katika zoezi la udhamini, Mpina amesema nia yake ni kuingia Ikulu na kuunda Serikali yenye viongozi waaminifu, watakaokomesha ubadhirifu wa fedha za umma na kuelekeza rasilimali hizo katika kutatua matatizo ya wananchi.

“Taifa letu tupo kwenye wakati mgumu. Najua matatizo waliyonayo wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara, bodaboda, mama ntilie, wachimbaji wadogo, machinga, na hata changamoto kubwa za utekaji pamoja na kufungiwa makanisa. Nimeamua kusimama kugombea ili kuyatatua matatizo haya,” amesema Mpina.
 
Back
Top Bottom