Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akizungumzia malalamiko ya watu kutekwa na kuuawa na watu wasiojulikana, leo Agosti 14 jijini Dares Salaam, mgombea urais wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina amesema hakuna kitu cha thamani kama maisha ya watu.
“Haiwezekani watu waendelee kutekwa na kuuawa. Haiwezekani uhai na thamani ya maisha ya mwananchi yakachezewa. Hatuwezi kukubali hoja dhaifu kwamba kufa ni kufa tu, kwamba Kifo ni kifo tu, hili halikubaliki. Haiwezekani vifo hivi vinatokea, halafu waziri, IGP, DCI, OCD na makamishina bado wako ofisini. Huu mfumo mzima lazima ufumuliwe, lazima wasiojulikana wajulikane na waliopotea tuwapate,” amesema.