Mpina: Hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai ya utovu wa nidhamu dhidi ya Dkt. Nchimbi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Naibu Waziri Mkuu Kivuli kutoka Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema kuwa taratibu zilizotumika kumwondoa aliyekuwa Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, zilivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuipora mamlaka ya nchi na kuikabidhi kwa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mpina amebainisha kuwa madai kuwa Dkt. Nchimbi alikuwa mtovu wa nidhamu hayana udhibitisho kwani umma haujawahi kuelezwa tuhuma zake, wala hajawahi kushtakiwa bungeni au kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mujibu wa Katiba.

"Kuvuliwa uanachama wa CCM hakumuondolei kiongozi moja kwa moja nafasi yake ya Umakamu wa Rais kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 50(3) ya Katiba. Ukuu wa Katiba ya nchi umepokwa na Katiba ya CCM. Ufafanuzi uliotolewa Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Agosti 28, 2026 kuwa Dkt. Nchimbi alipoteza sifa baada ya kuvuliwa uanachama haukuwa sahihi na ulilenga kuupotosha umma," alieleza Mpina.

Soma Pia: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu
 
Huyu mtu anazidi kuweuka kila siku, ni kwamba huko ACT kunamfanya nini mpaka anakuwa kituko namna hii?

Hata asiyejua Sheria na kutafsiri vifungu vya katiba anajua kuwa Tanzania hakuna mgombea binafsi, wagonbea wote wanadhaminiwa na vyama vyao. Chama kina mamlaka ya kumsimamia na kumwajibisha mgombea aliyedhaminiwa naye kama amekiuka kanuni za maadili ya Chama hayo mengine katiba ya nchi itaeleza zaidi.

Kwenye suala la Nchimbi hauhitajiki upotoshaji wa kilichotokea. Kilichomuondoa ni kujiuzulu kwake sio kuvuliwa uanachama, lakini baada ya kujiuzulu na Chama kikaangalia kumuwajibisha kwa namna yake .
 
Naibu Waziri Mkuu Kivuli kutoka Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amesema kuwa taratibu zilizotumika kumwondoa aliyekuwa Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, zilivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuipora mamlaka ya nchi na kuikabidhi kwa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mpina amebainisha kuwa madai kuwa Dkt. Nchimbi alikuwa mtovu wa nidhamu hayana udhibitisho kwani umma haujawahi kuelezwa tuhuma zake, wala hajawahi kushtakiwa bungeni au kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa mujibu wa Katiba.

"Kuvuliwa uanachama wa CCM hakumuondolei kiongozi moja kwa moja nafasi yake ya Umakamu wa Rais kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 50(3) ya Katiba. Ukuu wa Katiba ya nchi umepokwa na Katiba ya CCM. Ufafanuzi uliotolewa Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Agosti 28, 2026 kuwa Dkt. Nchimbi alipoteza sifa baada ya kuvuliwa uanachama haukuwa sahihi na ulilenga kuupotosha umma," alieleza Mpina.

Soma Pia: Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu
Huyo mshamba wa kisukuma hajawahi kuwa na akili tunamfahamu
 
Back
Top Bottom