Mpina kuwapeleka Mahakamani Waziri Bashe na Bodi ya Sukari kwa kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha Sheria

Luhuga Mpina ameyasema hayo katika Mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika jana tar 29 kuelekea 30, ikiwa ni mara ya kwanza kuzungumza baada ya kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao 15 vya bunge.

Kusoma taarifa hiyo zaidi ingia kwenye link hii: Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15

Akihitimisha taarifa yake Mpina alieza maadhimio yake kama ifuatavyo;

- Kupeleka malalamiko yake ya kuondolewa bungeni kwa uonevu na kutokutendewa haki na Spika wa Bunge Tulia Ackson kwenye vyombo vya sheria ili vikapime na kutoa haki kwa mujibu wa katiba ya Tanzania na sheria za nchi.

- Kumpeleka Mahakamani Waziri wa Kilimo Ndg. Hussein Bashe na Bodi ya Sukari chini ya ibara ya 26 na 27 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kitendo cha kutoa idhini ya vibali vya kuagiza sukari kinyume cha sheria na kulisababishia taifa hili hasara kubwa.

- Kuyafikisha Mahakamani makampuni yote yaliyojihusisha na ungizaji wa sukari nchini kinyume cha sheria.

===

Pia soma:

MwanaMpina
 
Kwann asihutumie muda huu kukaa karibu na wapiga kura wake ? Kuliko kushindana na serikali,anaamini ataishinda huko mahakamani? Kama wabunge wote pamoja na kwamba wa chama chake hawakumuunga mkono
 
CCM na chawa wengi hawajui kuwa Mpina amehukumiwa si kwa kupotosha au kusema uongo, ila ni kwa kulidharau bunge.

Ukweli wa yale yote aliyoyasema Mpina unabaki pale pale.
Bashe hajasafishwa na bunge tuhuma zote alizozitoa Mpina.
 
Nimesikia mwanzoni, katikati na dakika 15 za mwisho. My Take:-
1. Ana nguvu kubwa nyuma yake inayomsukuma. Kusema kuwa Luhaga Mpina anatetea raslimali za umma na kwamba ni mzalendo siyo kweli
2. Ana some facts ambazo amazisimamia japo ametawaliwa na unafiki pia. Kuna vitu vibaya sana walifanya akiwa kwenye Serikali ya Magufuli lakini hakuwahi kuhoji
3. Akienda Mahakamani ataishia kwa Msajili wa Mahakama. Yaani shauri lake linaweza lisipate namba
4. Kama litapata namba basi na DPP lazima aingie kwa ajili ya kuendesha kesi ya jinai. Hii itakuwa sawa na kesi ya Gekul vs yule wa kuwekwa chupa makalioni.
5. DPP akiingia mention ya pili tu anaomba nolle prosecui
Luhaga Mpina ana hoja sema yupo mbele ya wakati!
Sema Wabongo wa leo wanataka sukari... Ufisadi kwenye mchakato wa sukari
 
Back
Top Bottom