Mpina: Kwanini kwenye nchi yetu watu wanyamazishwe? Kwanini ukihoji Serikali iwe ni makosa ya uhaini na ugaidi?

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Naibu Waziri Mkuu katika Baraza Kivuli la Mawaziri la Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina amehoji kwanini kwenye nchi yetu watu wanyamazishwe? kwanini ukihoji serikali iwe ni makosa ya uhaini na ugaidi?

Wakati akiongea na waandishi wa habari August 9 Mpina amesema kuwa,

"Sasa huku nchi nzima watu wanafunguliwa kesi za ugaidi, alafu huku tena mnatoa statement ya kwamba hapa nchini kwetu hakuna ugaidi. Kwa sababu gani? Hawawezi kuwa na maelezo ya kufanjana kwa sababu swala la ugaidi ni swala ambalo linatengenezwa tu kwa ajili ya kuwakomoa wananchi wanaotaka kuiwajibisha serikali kutokana na maovu inayoyafanya kwa wananchi."

Your browser is not able to display this video.
 
Huyu naye awache kutuvurugq,alikuwepo kwenye utawala wa Magufuli akawa kama Mungu wa wizara I kwake.

Mbona kipindi hicho watu walikuwa wanakamatwa na kufunguliwa hizo kesi?
 
Sio sababu.
Kwa hiyo yanayoendelea kufanywa ni sahihi?.
siyo sahihi na hayakubaliki kabisa,lkn je yeye hayajui?
vinginevyo atwambie kuwa alipokuwa kwenye utawala huu alikuwa anaychukia ila sasa aliogopa au kuyafumbia machi
 
Kwani Mpina anauliza kwamba hajui au anajifanyisha kua hajui

Yeye kama anataka kusema kitu aseme aache kunzunguka zunguka
 
Huyu naye awache kutuvurugq,alikuwepo kwenye utawala wa Magufuli akawa kama Mungu wa wizara I kwake.

Mbona kipindi hicho watu walikuwa wanakamatwa na kufunguliwa hizo kesi?
100% lazima uwe,mnufaika sio bure! harafu sisi watz kwanini tunapenda kujibu changamoto kwa changamoto za awali? Aya kinachosemwa ni kweli au si kweli? ni sahihi kiendelee kufanyakia?
 
100% lazima uwe,mnufaika sio bure! harafu sisi watz kwanini tunapenda kujibu changamoto kwa changamoto za awali? Aya kinachosemwa ni kweli au si kweli? ni sahihi kiendelee kufanyakia?
Kinachoendelea ni hakikubaliki kwa asilimia zote
 
Sababu ya haya yote ni; 1:Ukosekana wa ukomavu wa kisiasa. 2:Elimu 3:Maslahi binafsi 4:Kukomoana kisiasa 5:Visasi 6:Udini, ukanda na jinsia. 7:kiburi na ujeuri. 8:Mifumo kuingiliana mfano, siasa na serikali. 9:Tamaa ya madaraka 10:Rushwa 11:Mmomonyoko wa maadili 12:Usaliti(kusalitiana) NINI KIFANYIKE KUONDOA YOTE HAYA: 1:Kutanguliza maslahi ya taifa 2:Maridhiano ya Kitaifa(viongozi wa dini,wanasiasa,wananchi wasiofungamana na upande wowote Na makundi yote ya kijami. 3:KATIBA MPYA (japo mchawi yupo hapa sio kazi rahisi) 4:Kufumuo mifumo ya upendeleo mfano, kama tutaendelea na mifumo yetu hii ya kisiasa japo mimi nilitamani ifumuliwe.Pawepo na usawa kama Raisi atatoka CCM makamo awe chama pinzani na kinyume chake iwe hvo mpaka ngazi za chini. 5:Kupendana na kuthaminiana katika utu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…