Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, leo Oktoba 15, 2026, amezungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa maelezo na maagizo yaliyotolewa na Jumuiya ya Madola, AU, na Marekani hayajatekelezwa na mtawala bado anaficha ukweli.
Amefafanua kuwa muda uliowekwa na Jumuiya ya Madola wa siku 90, siku 30 za kuachiwa huru kwa Tundu Lissu, pamoja na siku 60 za kufanya majadiliano na maelewano ndani ya nchi zote zimeshaisha bila utekelezaji wowote au mazungumzo ya maana kufanyika.
Mpina ameongeza kuwa licha ya yeye kuwa mgombea urais ambaye kesi yake bado iko mahakamani, hakuna mjadala ulioendeshwa kutatua migogoro hiyo ya kisiasa nchini. Amesisitiza kuwa Tundu Lissu bado yuko gerezani hadi sasa na kesi yake haijaisha, huku muda uliopangwa ukipita bila serikali kuchukua hatua za dhati kutimiza maazimio ya kimataifa na ya ndani.
"Jumuiya ya Madola waliweka siku 90, siku 90 zishaisha. Siku 30 za kuachiwa Tundu Lissu zishaisha. Siku 60 za kujadiliana na kufanya maelewano ndani ya nchi zishaisha, hamna maelewano yoyote. Mimi hapa ni mgombea wa urais ambaye kesi yangu iko mahakamani. Hakuna mjadala wowote ulioendeshwa kutatua matatizo katika taifa hili. Tundu Lissu yuko gerezani mpaka sasa hivi kesi yake haijaisha "
Soma pia