Mpina: Mawaziri wapatikane kwa njia ya Ushindani siyo Uteuzi ili tupate Mawaziri Bora badala ya Bora Mawaziri!

Muendelezo wa Kauli za kukata tamaa ya kuteuliwa na pia kupigwa chini ubunge
 
Ila hamna watu wasahaulifu kama WANASIASA wa Tanzania, sasa sijajua au madishi yao yanayumba sometimes.
 

Lakini huyu hajielewi tu ila anataka Katiba Mpya.

Mfumo usipowapa asali huwa wanapata akili.
Akili zimerudi....yupo sahihi kwa alichokosema ila chama chake hakijawa tayari bado kwa hilo.
 
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amehoji bungeni kwanini Serikali isitumie njia ya ushindani kupata viongozi na watendaji wake wakiwemo Mawaziri badala ya uteuzi ili ipate wenye uwezo unaostahili. https://t.co/1qLj7Fs7rk
 
Refer Kenya wanavyofanya. Good idea any way.
 
Kwahiyo katiba mpya ni muhimu. Mta kuja tuu.
 
Mawaziri ni zao la wabunge, kwa mujibu wa katiba. Je, hao wabunge wenyewe wamepatikana kwa njia ya huo ushindani?
 
Ukiwa na akili pevu na za kimataifa utaelewa vizuri bila wasiwasi hoja ni nzuri sana
 
Jamaa ako na hoja ya msingi .

Ni kweli utaratibu wa uteuzi umepitwa Na wakati.

Inapelekea kuramba magalasa mengi tu!

Na wateuliwa wanaunda timu ya kusifu na kuabudu mteuzi.
 
Nadhani ametoa wazo hilo baada ya kugundua kuwa hata yeye aliteuliwa kwa bahati mbaya, hakustahili!
 
Anaye mpinga Mpina ni mpumbavu,

Katika mchakato wa ushindani hata yeye hana uhakika wa kuwa waziri ila wazi ni kupata mawaziri makini

Mpina ni mjinga fulani. Kwenye katiba ya Warioba mapendekezo ya wananchi ilikuwa ni waziri asiwe mbunge, bali aombe nafasi kisha usaili ufanyike. Cha ajabu utakuta anasema katiba haileti ugali mezani.
 
Mpina anashindwa kusema moja kwa moja anaungamkono hitaji la katiba mpya.
Kile chama chao kipya bado hakijapata usajili? Namuona akiungana na zito 2025
 
Luhaga mpina aache ujuaji mwingi usio na maana yoyote ,kakoselewa na Daktari wa uchumi aache kuupapalakia uchumi anaendeleza makasiriko.

Kila mtu akijiona ni mshauri na huku ushauri anaotoa ni wa hovyo unafanya Taaluma za watu zionekane bure
Daktari wa uchumi, madelu? Tz tumekwisha!
 
Mpina ni mjinga fulani. Kwenye katiba ya Warioba mapendekezo ya wananchi ilikuwa ni waziri asiwe mbunge, bali aombe nafasi kisha usaili ufanyike. Cha ajabu utakuta anasema katiba haileti ugali mezani.
Kweli kwenye ile rasimu ya warioba original ilielezea vizuri kabisa jinsi ya kuwapata mawaziri
 
Jadili hoja acha personal attack,
Hoja yake ina mashiko na inatukumbusha umuhimu wa katiba mpya
Chief, usidanganywe………,na achana na wachumia tumbo! Yeye alikuwa wapi asikemee haya wakati alipoteuliwa kuwa waziri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…