Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, amesema ana matumaini kuwa Bunge lijalo baada ya uchaguzi litakuwa chombo makini chenye hoja nzito, kitakachohoji mambo ya msingi kwa maslahi ya wananchi, badala ya kuwa jukwaa la lelemama.
Akihutubia wananchi wa Mwandu Itinje, Jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu leo Juni 1, 2025, Mhe. Mpina amesema amekerwa na kuenea kwa vitendo vya ufisadi, wizi na rushwa, huku wahusika wakishangiliwa badala ya kuwajibishwa.
“Wananchi wanyonge wanahitaji huduma bora za kijamii. Wengi wanaishi maisha magumu, halafu watu wasio na uchungu na nchi wanabadhirifu mali za umma na kupongezana wao kwa wao. Hili haliwezi kuvumilika,” amesema.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Ameongeza kuwa taifa haliwezi kuendelea ikiwa viongozi watabaki kuwa wasemaji wa mapambio au washiriki wa makongamano bila kuchukua hatua dhidi ya maovu.
“Hatuwezi kuwa viongozi wa kusimama na kuongea mapambio tu, hatuwezi kuwa wa makongamano tu, wakati fedha za wananchi zinaliwa. Mbunge aliyechaguliwa na kuapa analeta vigelegele kwa wezi! Kwa kumwogopa nani? Hatuhitaji kupongezana" amesisitiza Mpina kwa ukali