Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina amesema misamaha holela ya kodi katika bei za bidhaa ikiwemo biashara ya sukari imepelekea serikali kupoteza mapato na kwamba vitendo hivyo ni wizi kati ya wafanyabiashara na watumishi wa Serikali.
Mbunge huyo ameeleza kuwa inashangaza misamaha hiyo inayotolewa kwa upendeleo imekuwa ikitolewa kiholela huku serikali ikienda kukopa nje na kupendekeza tume hiyo iliyoundwa na Rais kufanya uchunguzi juu ya suala hilo
Mpina ameyasema hayo wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maoni yake kwenye Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi.
"Akiongea Mpina kwamba kuna misamaha ya kodi ya kiholela huko anaonekana mbaya, anaonekana anachongea watu na wengine wanaenda mbali 'hakipendi chama'", ameeleza.