PostGE2025 Mpina: Napinga Rais kuunda Tume Mpya ni Ujanja wa kukwepa ICC na Mahakama za Kitaifa

PostGE2025 Mpina: Napinga Rais kuunda Tume Mpya ni Ujanja wa kukwepa ICC na Mahakama za Kitaifa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Aliyekuwa Mbunge wa Kisesa na Mgombea Urais wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina ameyasema hayo Leo, 1, June 2026 alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo Maandamano ya Oktoba 29 2025, Ufisadi pamoja na Usimamizi Mbovu wa Rasilimali za Umma;


"Napinga kuanzishwa kwa tume nyingine chini ya mamlaka hiyo ya Rais. Kwani haitokei kuunda tume mbili kwa madhara yanayotokana na tukio moja. Hii ni kuwapotezea muda wananchi, kufuja fedha za umma, na ni ujanja wa kukwepa mchakato wa mahakama ya ni ujanja wa kukwepa mahakama ya uhalifu ICC na mahakama zingine za kitaifa.

Na, licha ya wezi wa fedha za umma kufahamika kwa majina na vyeo ndani ya serikali, lakini mamlaka za kushtaki, mamlaka za za mashtaka, upelelezi na uchunguzi za DPP, DCI na TAKUKURU zimeshindwa kuwakamata na kuwafungulia mashtaka, na inapobidi kutaifisha mali zao. Mamlaka tunazo.

Tunaye DPP, tuna DCI, tuna mwendesha mashtaka, tuna TAKUKURU; nimesema tuna DPP, tuna DCI, tuna TAKUKURU. Lakini wezi hao wanatangazwa tu, yote haya yanayotokea hapa hawaakamati.

Sasa unajiuliza kwa nini hawakamatwi? Na badala yake anaenda kofokewa mtumishi mmoja kule, sijui anadaiwa sijui milioni 500, sijui mie ngapi, anaenda kufokewa!
 
Back
Top Bottom