Mpina: Nusu ya Bajeti ya Serikali inaenda kutumika katika matumizi yasiyo ya uhalisia, matumizi mengine ni utapeli tu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amekosoa vikali muundo wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akidai kuwa kiasi kikubwa cha fedha za umma kinapotea kwenye matumizi yasiyo na uhalisia na ukopaji usio na tija.

Akizungumza leo Juni 23, 2026 wakati wa uwasilishaji wa uchambuzi wa Chama cha ACT-Wazalendo wa bajeti Kuu ya Serikali , Mpina amesema serikali inavyotumia fedha nyingi kugharimia kampeni za propaganda na machawa kwa lengo la kuficha ukweli wa hali halisi ya kiuchumi na kijamii nchini.

Mpina alinyooshea kidole ripoti za taasisi za ukaguzi kama CAG, PPRA, na FIU, akisisitiza kuwa zote zinathibitisha uwepo wa wizi, rushwa, na ufisadi mkubwa wa rasilimali za taifa. Alishangazwa na hatua ya Bunge kukutana kuidhinisha bajeti mpya wakati fedha zilizopita zimepotea kwenye ubadhirifu.

Amebainisha kuwa kati ya jumla ya bajeti iliyowasilishwa ya shilingi trilioni 62.33, matumizi halali yenye maslahi kwa nchi ni shilingi trilioni 30 tu, huku kiasi kilichobaki kikiteketea kwenye matengenezo makubwa ya magari, ukarabati wa majengo ya serikali na matumizi mengine aliyoyaita kuwa ni utapeli unaoendelea kuwanyonya walipa kodi wa Kitanzania.

Ikumbukwe leo Juni 23, 2026, Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 ambayo ni Jumla ya shilingi trilioni 62.33 , imepitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura asilimia 97.96

Yes,
hayo ni maoni na mtazamo wako huru ndugu mpina.

Bajeti ni ya waTanzania wote ina maslahi mapana ya Taifa zima.

Wivu, hasira, porojo na uzushi wako hauna maana wala athari zozote kwenye utekelezaji wa bajeti hiyo muhimu sana ya waTanzania.🐒
Mwenzako anajenga hoja mbele ya kamera. Jitokeze na wewe tupime sincerity ya maneno yako!
 
Yes,
hayo ni maoni na mtazamo wako huru ndugu mpina.

Bajeti ni ya waTanzania wote ina maslahi mapana ya Taifa zima.

Wivu, hasira, porojo na uzushi wako hauna maana wala athari zozote kwenye utekelezaji wa bajeti hiyo muhimu sana ya waTanzania.🐒
We boya hata maiti zitaficha kichwa kuskiliza upumbavu wako .
 
Bajeti inaenda kulipa mikopo na matumizi ya hovyo kama kununua V8 mpya kila miaka mitatu kwa maelfu ya watu, kuwaongezea posho wenza wa viongozi na kutumika kuwateka, kuwauwa Watanganyika.
 
Naibu Waziri Mkuu Kivuli wa chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amekosoa vikali muundo wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akidai kuwa kiasi kikubwa cha fedha za umma kinapotea kwenye matumizi yasiyo na uhalisia na ukopaji usio na tija.

Akizungumza leo Juni 23, 2026 wakati wa uwasilishaji wa uchambuzi wa Chama cha ACT-Wazalendo wa bajeti Kuu ya Serikali , Mpina amesema serikali inavyotumia fedha nyingi kugharimia kampeni za propaganda na machawa kwa lengo la kuficha ukweli wa hali halisi ya kiuchumi na kijamii nchini.

Mpina alinyooshea kidole ripoti za taasisi za ukaguzi kama CAG, PPRA, na FIU, akisisitiza kuwa zote zinathibitisha uwepo wa wizi, rushwa, na ufisadi mkubwa wa rasilimali za taifa. Alishangazwa na hatua ya Bunge kukutana kuidhinisha bajeti mpya wakati fedha zilizopita zimepotea kwenye ubadhirifu.

Amebainisha kuwa kati ya jumla ya bajeti iliyowasilishwa ya shilingi trilioni 62.33, matumizi halali yenye maslahi kwa nchi ni shilingi trilioni 30 tu, huku kiasi kilichobaki kikiteketea kwenye matengenezo makubwa ya magari, ukarabati wa majengo ya serikali na matumizi mengine aliyoyaita kuwa ni utapeli unaoendelea kuwanyonya walipa kodi wa Kitanzania.

Ikumbukwe leo Juni 23, 2026, Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 ambayo ni Jumla ya shilingi trilioni 62.33 , imepitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura asilimia 97.96

Ila hiki nacho kina drama, eti kina naibu waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom