GE2025 Mpina: Utekaji pamoja na kufungiwa makanisa. Nimeamua kusimama kugombea ili kuyatatua

GE2025 Mpina: Utekaji pamoja na kufungiwa makanisa. Nimeamua kusimama kugombea ili kuyatatua

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Akizungumza na wananchi wa Katoro, Mkoani Geita leo Agosti 20, 2025 katika zoezi la udhamini, Mpina amesema nia yake ni kuingia Ikulu na kuunda Serikali yenye viongozi waaminifu, watakaokomesha ubadhirifu wa fedha za umma na kuelekeza rasilimali hizo katika kutatua matatizo ya wananchi.

“Taifa letu tupo kwenye wakati mgumu. Najua matatizo waliyonayo wakulima, wavuvi, wafugaji, wafanyabiashara, bodaboda, mama ntilie, wachimbaji wadogo, machinga, na hata changamoto kubwa za utekaji pamoja na kufungiwa makanisa. Nimeamua kusimama kugombea ili kuyatatua matatizo haya,” amesema Mpina.

 
huyo jamaa kama bosi wake, na yeye anasoma tu anachoandikiwa ...
 
Siku akiapishwa tu na utekaje unaisha.Wtz tumchangie mzalendo ambaye atamaliza utekaji ili tufanye kazi bila hofu ya kutekwa
 
Huyu aliwah kemea akiwa bungeni?
 
Back
Top Bottom