Kwanza mtu ukishakuwaga waziri halafu baada ya kuukosa unakuja kubwabwaja uraiani ni kukosa hekima. Mengine pengine ameyajua ndani ya baraza la mawaziri ambayo uliapa kulinda km siri za baraza la mawaziri leo unataka uonekane unajua mambo ni ushamba tu. Mpina hafai tena kuwa kiongozi mkubwa nchi hii.
Akajifunze hekima kutoka kwa George Simbachawene. Ni wananchi wachache watakuamini tena kuwa unatetea wananchi zaidi ya tumbo lako. Ukishakuwa mserikali unatakiwa uendelee kuzungukia mlemle. Mbona Dr. Medard Kalemani ametulia? Huyu hajafunzwa vizuri au ana upungufu wa malezi. Ni mtoto wa single mother au ushamba tu wa kinyantuzu?
Lakini anachokijadili ni siri za baraza au vitu vilivyowekwa wazi na CAG?
Hakuna sheria ya kulinda confidentiality ya taarifa uzipatazo ukiwa nafasi fulani kisha ukatoka?
Ukizungumza maadili una maanisha nini?
- Tume ya maadili ina maadili?
- TAKUKURU ipo namba ngapi kati ya taasisi zinazoongoza kwa rushwa na ubadhirifu?
- Polisi haikutajwa kwenye rushwa na uvunjifu wa haki?
- Mahakama si ndo mama lao kwa kila kitu?
Ni kina nani waliitwa STUPID, WAPUMBAVU?
Leo unajua kuwa Mwigulu kakopa 1.28trillion kiholela tu bila idhini ya Bunge, 1.7 trillion kalala nazo mbele kwa mujibu wa Mpina, kutokana na taarifa ya CAG.
Sasa, nani bora, yule anayekwapua na kusubiri nafasi nyingine kukwapua, au aliyekwapua, hana nafasi, anawajuza na kuanika ukwapuaji hadharani?
- Waziri walioiba na kusema ni VIJISENTI au HELA YA MBOGA? Au anayetaka BUNGE lijadili waganga wa kienyeji?
- Raisi aliyekopa Tzs trilioni 7 na hazikuingia serikalini kwa mujibu wa BBC, CAG hana habari!
Ukumbuke hiyo pia ni hulka ya Watanzania wezi wengi, Lowasa hakutoka tu hivi hivi, waligombana ndani huko, wenyewe kwa wenyewe, sis tukaijua Richmond mpaka akina Ruge.