Mpira ni Biashara kubwa Duniani, ogopeni kukabidhi wahuni timu

Mpira ni Biashara kubwa Duniani, ogopeni kukabidhi wahuni timu

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Mpira umekuwa Biashara kubwa sana Duniani, ukitoa biashara ya mafuta, gas, Madini na silaha, mpira ni moja ya Biashara kubwa, ni hatari kukabidhi timu wahuni, wasio jua thamani ya dhamana walizopewa.

Kwenye tatizo linalohusian na uvanjaji wa kanuni, taratibu na sheria, hata kama umeonewa hutakiwi kupambana kwa mabavu, Kuna vyombo vipo vya kusimamia taratibu, kanuni na Sheria kuhakikisha haki yako unapata.

Uongozi ni zaidi ya kuwa na akili tu, uongozi unahitaji busara, hekima, unyenyekevu.

Kwa namna hii tutegemee mengi yanakuja.

Mwisho, ni hekima sasa Serikali kutengeneza utaratibu wa kufanya special audit kwa vilabu vya Tanzania.
# Mungu ibariki Tanzania
#Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, SSH
#Tujiandae kuhesabiwa...Sensa law Maendeleo ya Taifa
 
Asikwambie mtu , Yanga ni tamu . Sekunde ya ishirini tu vipers kapiga bao la kwanza.
20220807_071103.jpg


Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Na ndiyo maana Senzo kaamua kusepa. Jamaa hapendi ubabaishaji hata kidogo
 
Kupitia bifu zao watu wanatengeneza noti nyie mnakalia kuwaita wahuni. Mtashituka kumekucha
 
Kupitia bifu zao watu wanatengeneza noti nyie mnakalia kuwaita wahuni. Mtashituka kumekucha
Uhuni ni uhuni tu haijalishi unatengeneza noti, jua kabisa kuna sehemu wanaharibu na impact itakuwa kwa club, hakuna hela inayotengenezwa bila kuwepo na nidhamu, huwezi ukawa unatukana viongozi, unadharau Mamlaka halali, unadhalilisha watu na ukadumu milele kwenye hiyo nafasi ya kutengeneza noti unayosema, no way Mr Q
 
Back
Top Bottom