Mpira ni Matokeo au Burudani ?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Ni kipi cha muhimu sana kwa washabiki ?, Je is football game of results ? au ni bora hata tukifungwa ila chenga twawala ?

Ni maneno mengi yamesemwa hata The GodFather of Boring (Jose Maurinho) alisema kwamba Westham inacheza 19th Century Football !!! ila tukiangalia ile Chelsea iliyoshinda ile Champions League kwakweli ilikuwa a sad day in football..

Swali langu ni kwamba Timu haina wajibu wa kuhakikisha kwanza inaburudisha ? Nina uhakika bila Brazil, Barcelona and Arsenals of this world..., mpira usingekuwa unaitwa the Beautiful Game...., Mpira ambao ni Negative utakupeleka so far ila baada ya kushinda Kombe hata mwaka mmoja mashabiki watachoka na kudai zaidi.., na ukiendelea hivyo unaweza kujikuta watu wanaacha kuangalia..For the good of Football ni bora mashabiki wakakemea hii cancer ya kupaki mabasi (Turudi kwenye Imani ya Kwamba Attack is the Best Defense)
 
kwa kuanza we nishabiki wa timu gani?!

Nashabikia / Supporter wa Timu ya mtaani kwangu haijapanda daraja lolote..., ila mimi ni muumini wa Mpira ninaangalia mipira yote na hufanya hivyo ili kuburudika.., na nikiona Timu ya Kitaa inadefend tu bila ku-attack hata kama wakishinda sifurahishwi na kile wanachokifanya
 


it's your faith.. you should not force me to just believe what you say...
my question to you..why say it now?
 


Njoo kule CHELSEA FC THREAD lete hii hoja kule..si umemtaja CHELSEA FC 'coach', njoo kule..tuongee vizuri.🙂
 
it's your faith.. you should not force me to just believe what you say...
my question to you..why say it now?

I say it now because there is a tendency of results by all means.., na ni ukweli usiopingika kwamba haina hii ya negativity itafanya watu wasipende mpira.., kuna sababu kwanini Italian Football haiangaliwi sana (defensive) na kuna sababu Timu kama Ajax, Barcelona, Real Madrid zinapendwa hata na Neutrals.., Ni ukweli usiopingika kwamba Negativity in the long run inaua mpira na kupoteza mashabiki..

Ndio unaweza ukashinda Makombe kwa kuwa Negative (Hata Greece ilishinda Kombe la Ulaya) lakini kila mtu akitumia hii negativity (sio kwamba hawawezi) watu wataacha kuangalia mpira..
 
Njoo kule CHELSEA FC THREAD lete hii hoja kule..si umemtaja CHELSEA FC 'coach', njoo kule..tuongee vizuri.🙂

Hii kitu inakwenda zaidi ya Chelsea..., (ingawa kwa mwaka huu na huyu Maurinho hata alivyokuwa Inter na pesa anazotumi hautendei haki mpira) ningeelewa timu kama Crystal Palace wakitumia Route One Football ili waweze ku-survive nitaelewa ila sio Timu yenye talented footballers na inayotumia mapesa kama Chelsea
 
By the way agosti 8

Ni rahisi kusema unafurahia huku ukiwa Bar/Counter unapata maji baridi unashangilia.., swali langu ni hivi kweli unaweza ukatoa at least 45 pounds huku unapigwa baridi kuangalia wanaume Kumi wote wana-defend na kungojea kaupenyo ili wafunge ?
 
Last edited by a moderator:

sasa kama unashabikia timu ya mtaani kwenu, morinho hapo ameingiaje?! .......... uliangalia game la atletico vs barcelona?!
 
sasa kama unashabikia timu ya mtaani kwenu, morinho hapo ameingiaje?! .......... uliangalia game la atletico vs barcelona?!

Kwahio wewe kama unashabikia Chelsea mechi za Simba na Yanga huangalii ? Hapa point sio Chelsea wala Timu yangu ya Kitaa (naishabikia sababu ya attachment na connection)..., Point hapa ni Je Timu za mpira zinawajibu wa kutoa Burudani kwa mashabiki au wajibu ni kushinda/kutokufungwa hata kama wanaboa watazamaji ? Kumbuka hata kama watu wakiwa wanaboreka kila mara wakipunguza kuangalia hata sponsorship itapungua na mapato kupungua pia.

Je tunahitaji kina Real Madrid na Barcelona zaidi au hata kina Chelsea na wapaki mabasi wanatosha.., ili mradi mtu anashinda.
 
we tatizo lako thread yako imekaa kinafik nafiki zaid!" ungeanzisha bila kutaja chels cjui wamapaki basi final, ndio mana nikauliza gemu la atletico vs barcelona uliangalia?! uliona atletico walivyocheza?! siyo unashupalia chels chels!" 2achane na hay0 ........... nikuulize swali jingine " je unafikiri ni kw nn Moyes amefukuzwa?" na timu ilikua inacheza vizur hata hao chels hawaoni ndani.
 
sasa kutakuwana ladha gani endepo timu zote zitacheza mpira wa aina moja? hao aseno unaowasifia kwa soka safi mbona washabiki wake bado wana malalamiko ya kutaka vikombe? kilka timu ina falsafa yake katika soka
 
Hapa hakuna unafiki ndio maana nikataja maneno aliyosema Jose mwenyewe kuhusu West Ham kwamba wanacheza 19th Century Football au msemo wa kupaki basi aliuleta Jose mwenyewe siku walivyocheza na Spurs wakatoa draw akasema kule Ureno hii huwa tunaita kwamba Timu inakuja na basi lao wanalipaki golini..., sasa na mimi kama Neutral nikiangalia soka lao je nakatazwa nikisema Jose ni Godfather of Boring ?

Na unavyosema kwanini Moyes kafukuzwa kazi ?, ni kwamba performance yake imekuwa mbovu sana kuliko expectations Man United haijawai kufanya vibaya hivi kwa miaka mingi sana, alafu si kweli kwamba Moyes anacheza free flowing football kama Man United walivyozoea ni kwamba na yeye yupo Negative.., ndio maana wengine walilalamika anakata kuibadilisha Man United iwe kama Everton yake.., Game kama waliyocheza na Bayern nyumbani au ile waliyocheza na Chelsea nyumbani inaweza ikakupa jibu ninamaanisha nini na Boring...

Pia sijasema Burudani inamaanisha kushindwa game.., unaweza mwisho wa siku ukafungwa lakini umejaribu.., na hata magoli mkitufunga ila chenga twawala (msemo wa ndugu zetu wan Zanzibar)
 
sasa kutakuwana ladha gani endepo timu zote zitacheza mpira wa aina moja? hao aseno unaowasifia kwa soka safi mbona washabiki wake bado wana malalamiko ya kutaka vikombe? kilka timu ina falsafa yake katika soka

Sisemi kila timu icheze mpira wa aina moja bali timu zikiwa attacking minded mpira unavutia zaidi.., hivi unajua kwamba zamani mpira ulikuwa na points 2 draw point 1 na ukishinda points 2; hadi kuweka point 3 timu ikishinda ilikuwa ni ili kushawishi timu kuwa na mashambulizi.

Pia hivi unajua Arsenal kabla ya Wenger ilikuwa inaitwa Boring Boring Arsenal ? au One Nil to the Gunners ?, Hii ilikuwa sababu jamaa wakikufunga moja wanadefend mpaka mwisho na kwa taarifa yako Arsenal then ilikuwa haipendwi kama leo na washabiki hawakuwa wengi kama leo.., Pia timu kama Brazil ndio zimekuwa kama mabalozi wa kutangaza soka na kufanywa ipendwe kama inavyopendwa sasa.

Ndio maana hapa sijasema upende aina fulani ya Timu bali nimekuuliza, je Timu ikiwa effective inashinda na inashinda kwa winning Ugly, je inatosha ? au ina wajibu zaidi ya kushinda ?
 

Kwanza nakushauri ungebadili heading ya uzi wako.

Ukimaliza, jaribu kutupa definition/maana ya negative football na ukiweza mbadala wa hiyo negative football

Una vigezo vipi kusema Italian football haiangaliwi sana (defensive)?
Haiangaliwi na nani na wapi?

Unaweza ukaweka data hapa kwa Ajax inapendwa sana kuliko AC Milan au Juventus?

Halafu wewe ni nani au unakibali gani kuwasemea watu kuwa "na ni ukweli usiopingika kwamba haina hii ya negativity itafanya watu wasipende mpira"?
Unapata wapi huu ujasiri wa kuwasemea watu hata usiowajua?

cc; juve2012 shifta Ziroseventytwo
 
Last edited by a moderator:
Kwanza nakushauri ungebadili heading ya uzi wako.

Ukimaliza, jaribu kutupa definition/maana ya negative football na ukiweza mbadala wa hiyo negative football

Mkuu kama hujui negative tactics, / negative football / defensive football kimantiki ya mpira sijui niseme nini mkuu

Una vigezo vipi kusema Italian football haiangaliwi sana (defensive)?
Haiangaliwi na nani na wapi?

Ukilinganisha watu wanaongalia mpira worldwide utaona kwamba premier league inaangaliwa kutokana na pace na magoli ni mengi, na ukilinganisha na audience ya Premier League ni kubwa kuliko Serie A, hizo ni data ambazo zipo wazi, pia ukiangalia results za serie A magoli yanayofungwa huwa ni machache.., Italians Team nyingi zinatengezwa defensively, tofauti na Premier League Pace na build up ya haraka haraka au Spain Technical Ability ni kubwa zaidi those are the facts, tafuta uone ni League ipi inaangaliwa sana globally kati ya Premier League, Serie A na La Liga...

Unaweza ukaweka data hapa kwa Ajax inapendwa sana kuliko AC Milan au Juventus?
Sasa hapa uninilisha maneno, nimesema Timu kama Ajax zinapendwa hata na Neutrals nikimaanisha aina ya mpira wanayocheza.., ukiachana na hii Ajax ya sasa kuna Ajax ambayo watu walikuwa wanasema ndio walioleta Total Football, pia sijasema AC Milan ni boring (the best Team of so many years, mfano ya Kina Gullit, Weah n.k.) au Juventus bali nimesema mpira wa Italy ni defensive as a whole sio AC Milan wala Juventus as a Unit.., ingawa Premier League ina Pace lakini bado kuna Teams za kina Sam zinazocheza Route One Football

Halafu wewe ni nani au unakibali gani kuwasemea watu kuwa "na ni ukweli usiopingika kwamba haina hii ya negativity itafanya watu wasipende mpira"?
Unapata wapi huu ujasiri wa kuwasemea watu hata usiowajua?

Kwanini watu wanapenda kuangalia Barcelona kila inavyocheza ? Neutrals au sio Neutrals..; Kwanini watu huwa wanasema dah ile fainali ilikuwa nzuri au ile ilikuwa mbaya ? watu huwa wanaangalia mpira ili wapate nini mwisho wa siku ushindani na kujitahidi kushinda au matokeo mwisho wa siku kwamba hawakufungwa ? Kwanini baadhi ya Timu kila zikicheza uwanja unajaa na nyingine uwanja unakuwa mtupu ? Ukijibu hayo utagundua kwamba aina ya mpira inavutia watu kuangalia soka ndio maana Brazil always ikicheza watu wengi ulimwenguni wanawaangalia (Attractive Football)
 

big up kwa mada nzuri wewe kweli mtu wa mpira
 
KeyserSoze
Huwezi kuongelea negative football halafu ushindwe hata kutuambia maana yake (definition)
Sasa tutatambuaje kama hili soccer ni negative na hili ni positive? Kwa vigezo vipi?

Na kama unashindwa inawezekana kabisa hii term "negative football" ni subjective, hata mimi naweza kuwa na maana yangu kama maana ya jumla haipo.
Kwa mfano; Wakati wa Euro 2012, Spain wazee wa tikataka walizomewa na washabiki kwenye moja ya mechi yao kwamba mpira wao ni boring kwa sababu wanapiga pass nyingi sana zisizo na manufaa yeyote.
Na juzi hapo tumemsikia Franz Beckenbauer akisema Bayern are unwatchable kwa sababu wanaboa, hawachezi soccer la "kijerumani"

Miaka ya 80 mwishoni na miaka ya 90 soccer la Ulaya lilitawaliwa na serie A, kimafanikio, kipesa, washabiki na wachezaji manguli duniani walikua wanacheza huko( sihitaji kuwataja kwa sababu hata mungu wa soka D10S alivuma huko) sasa utaniambiaje kuwa soccer la Italy haliangaliwi sana kwa sababu ni negative? Limekuwa negative toka lini?

Kama Barcelona, Madrid na Ajax ndio zinacheza mpira unaopendwa na wengi, kwanini EPL ndio inawatazamaji wengi? Kwanini isiwe La Liga na Eredivise?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…